mwambelablog

Friday, 23 December 2022

MAKUMBUSHO YA TAIFA YAWAAGA WASTAAFU

 

Pichani: Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga akimpatia Bibi Darila Yasini cheti cha utumishi.

Na Mwandishi wetu.


Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt Noel Lwoga amewapongeza wastaafu waliokuwa watumishi wa Taasisi hiyo kwa utumishi uliotukuka.


Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wastaafu kutoka katika vituo vya Dar es Salaam na Arusha amewataka kuendelea kutoa mchango wao kwa Taasisi.


"Ninyi ni wataalamu katika maeneo mbalimbali hivyo muendelee kutoa ushauri juu ya kazi mbalimbali za Makumbusho" alisema Dkt Lwoga.


Amesema Taasisi yake itaendelea kuboresha mazingira ya kazi ya watumishi na kuhifadhi historia ya viongozi walitumika Makumbusho ya Taifa.


"Zawadi tulizotoa ni ishara na alama ya kuthamini mchango wenu katika Taasisi hii kwamba ulipita Makumbusho ya Taifa" alisema Dkt. Lwoga.


Pichani: Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga akimpatia mmoja wa wastaafu, Bw. Adrian Samagwa.

Mwakilishi wa wastaafu hao, Bw Adrian Samagwa ambaye alikuwa Mhasibu Mkuu  ameushukuru uongozi wa Makumbusho ya Taifa kwa kuandaa hafla ya kuwaaga.


Ameuomba uongozi wa Makumbusho kutoa semina ya kujiandaa kustaafu kwa watumishi miaka mitano kabla ili wastaafu watarajiwa waweze kujiandaa.


Vile vile amewataka watumishi kufanyakazi kwa juhudi na maarifa na kwa uwajibikaji ili viongozi waweze kufikia malengo ya Taasisi

Thursday, 22 December 2022

KIJANA WA MIAKA 17 AWAJENGEA UWEZO VIJANA 70 MKOANI KAGERA JUU YA KUFUATA NDOTO ZAO WAKIWA KATIKA UMRI MDOGO.

Pichani: Mgeni rasmi katika semina ya Vijana ya kuwajengea uwezo wa kufuata ndoto zao, mchungaji Joas Kahesi.


Pichani: Doreen Ngemera Kijana Mwenye umri wa miaka 17 akiwajengea uwezo vijana juu ya kutambua ndoto zao.

Pichani: Mwemezi Ngemera mfadhili wa mafunzo hayo akizungumza na vijana.
Pichani: Ni Sehemu ya vijana hao wakifuatilia mafunzo kea ukaribu sana.


Na Lydia Lugakila, 

Kagera.


Jumla ya vijana 70  kutoka shule za sekondari na msingi katika kata za Kanyigo na Kashenyi wilayani Misenyi mkoani Kagera ambao ni kati ya umri wa miaka 12- 18 wamenufaika na elimu ya  kuwajengea uwezo juu ya kufuata ndoto zao wakiwa katika umri mdogo ili wajitambue na kufikia malengo yao.


Akiendesha semina  hiyo iliyofanyika katika shule ya sekondari Kanyigo Doreen Ngemera mwenye umri wa miaka 17 mwanafunzi wa kidato cha tano amesema kuwa wameamua kuwajengea uwezo vijana hao ili kufuata ndoto zao wakiwa katika umri mdogo kwa kuwafanya  watambue ndoto zao mapema jambo litakalo wasaidia kuweka bidii ili watimize ndoto hizo bila vikwazo.


Doreen amesema vijana wengi wana uwezo mkubwa ila bado hawajatambua waanze wapi ili kufikia ndoto zao zitakazo wasaidia kwa maisha ya baadae.


"Mimi ni kijana mdogo nina umri wa miaka 17 nimeona niwalete pamoja vijana hawa wapate elimu ya kutambua ndoto zao na kuzifanyia kazi wakiwa wadogo ili kwa baadae wasiwe wategemezi katika familia zao" alisema Doreen.


Ameongeza kuwa kwa mwaka 2021 walifanya semina ya namna hiyo ya utambuzi wa vipaji walivyonavyo vijana  ambapo waliwafikia vijana 100 na hadi sasa wametambuliwa na wengine kupata fursa mbali mbali huku akiwaomba wazazi kutokuwa sehemu ya kukatisha ndoto za vijana hao.


Aidha kwa upande wake mfadhili wa semina hiyo Bwn Mwemezi Ngemera amesema wamelenga kundi la vijana ili kuwano kabla ya kuelekea uzeeni na kuwa baada ya kugundua baadhi ya wazazi kutokaa na kuwasikiliza vijana wao katika kutambua na kutimiza ndoto zao wameamua kuja na muarobini huo wa kuwanoa.


Ngemera amempongeza Doreen kwa kuwaleta pamoja vijana hao ambapo amewahimiza wazazi kutambua majukumu yao kwa watoto ikiwa ni pamoja na kutowakatisha tamaa katika kufikia malengo yao huku akiahidi kutenga muda mzuri kuwakutanisha vijana hao katika awamu ijayo ili kuwa na wasomi wengi kwa baadae.


Naye mgeni rasmi katika semina hiyo ambaye ni mchungaji kutoka Kanisa la kiinjili la Kilutheli Tanzania KKKT dayosisi ya kaskazini Magharibi Joas Kahesi amesema kuwa vijana wasipotambua ndoto zao wakiwa wadogo mbeleni kuna shida.


"Kujitambua kunatokana na kuwa na mtizamo chanya na kutokatishwa tamaa jijengeeni msingi wa kuacha uvivu jamii haihitaji vijana wawe mzigo kwa baadae, hivyo ni lazima kila kijana awe na matamanio akiwa na umri mdogo kwa kutunza ndoto yake"alisema mtumishi wa Mungu.


Hata hiyo Maraika Gedi,Shafiu Faki na Fatiha Yunus ni moja kati ya wanufaika wa mafunzo hayo wamepongeza wawezeshaji na kukiri kupata uelewa kwani wamejua namna ya kutotegemea ndoto moja, kufuata ndoto zao, kujiamini, huku wakiahidi kuwa mabalozi kwa vijana wenzao na pia kuwaomba wazazi kujenga utamaduni wa kuwaruhusu watoto kushiriki mafunzo mbalimbali yanapotolewa na wafadhili mbalimbali.

Sunday, 18 December 2022

KONGAMANO LA BUKOBA WOMEN GALLA LALETA FARAJA UPATIKANAJI DAMU SALAMA.

 Na Lydia Lugakila

Bukoba


Jumla ya unit 25 za damu zimepatikana kupitia kongamano la Kibeta women Galla lililolenga kuwajengea uwezo wanawake kujitegemea kiuchumi.


Akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika katika kata ya Kibeta Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, mratibu wa damu salama mkoa Boniphace Meza amesema kuwa kongamano hilo limesaidia kwa kiasi kikubwa kuwakutanisha wanawake walioamua kuchangia unit 25 za damu.

"Ninamshukuru diwani wa kata ya Kibeta kupitia kongamano hili lilowezesha upatikanaji wa damu, uchangiaji huu ni muhimu sana kwa wenye uhitaji niwapongeze wananchi wa Kagera kutokana na kuwa na muitikio mzuri katika uchangiaji wa damu kwa sasa sina upungufu wa damu katika katika kapu langu alisema Meza."


Aidha amewapongeze pia wanafunzi wa shule ya sekondari Ihungo ambayo imekuwa ikichangia pakubwa  kupatikana kwa wastani wa chupa za damu 150 hadi 200.


Nao baadhi ya wachangiaji wa damu hiyo akiwemo bi Oliva Godwin na Judika Kalumna wamesema kuwa wameamua kuchangia damu hiyo kutokana na wanawake kupata matatizo ya upungufu wa damu wakati wa kujifungua.


Aidha kwa upande wake diwani wa kata ya Kibeta Anastella Alphonce ambaye ni muandaaji wa kongamano hilo amesema kuwa wamelenga kuwajengea uwezo wanawake hao kuondokana na utegemezi kiuchumi huku akiwahimiza kujenga utamaduni wa kuchangia damu salama ili kuokoa maisha ya watu wenye huhitaji 


Bi Anastella amesema kuwa kongamano hilo litakuwa endelevu kila mwaka ili kuwakumbusha wanawake kuwajibika vyema katika nafasi zao sambamba na uchangiaji  wa damu salama.


Naye katibu wa wamachinga manispaa ya Bukoba Eliana Elias mmoja kati ya waandaaji wa kongamano la Kibeta Women Galla amesema kuwa wanawake wamenufaika na elimu ya ujasiriamali na kuwa lengo lao ni kumuunga mkono Rais Dokta Samia   mbapo  KAULI MBIU NI "MWANAMKE INUKA SONGA MBELE MWINUE NA MWENZAKO.

KASEKENYA AACHA MAAGIZO NYUMBA YA JAJI KUKAMILIKA KWA WAKATI KAGERA.

 

Pichani: Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi mhe, Godfrey Kasekenya akiwa ziarani mkoani kagera kukagua mradi wa Ujenzi wa nyumba ya Jaji unaosimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania 

Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi mhe, Godfrey Kasekenya ameagiza wakala wa majengo Tanzania (TBA) Mkoa wa Kagera kukamilisha nyumba ya jaji wa mahakama  mkoani Kagera  kwa wakati ndani ya miezi 6 ikiwa ni pamoja na kuzingatia ubora kwa kuwasimamia wanaojenga nyumba hiyo.


Agizo la naibu waziri wa ujenzi  na uchukuzi limekuja baada ya  kufanya ziara ya kukagua mradi wa Ujenzi wa nyumba hiyo unaosimamiwa na Wakala wa Majengo  Tanzania (TBA) na kujionea shughuli mbalimbali  zinavyoendelea.


Mh, Kasekenya amesema kua hivi karibuni wizara ya ujenzi na uchukuzi  ilitoa kiasi cha shilingi milioni 360 katika mradi huo na kuwa mradi umefikia asilimia 13 hivyo anategemea kuona ndani ya miezi 6 unakamilika.


"Naomba muisimamie ahadi hiyo muitekeleze na naomba hilo lifanyike zingatieni ubora,wasimamie wanaojenga kamilisha kazi hiyo kwa wakati sababu nyumba hii inahitajika sana ili ianze kutumika alisema Kasekenya."


Aidha amewapongeza Wakala wa Majengo Tanzania kwa hatua waliyofikia katika ujenzi huo na kuongeza kuwa mradi huo utakuwa mkombozi kwa  watumishi.


Kwa upande wake kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania TBA mkoa wa Kagera Adam Malimi amesema nyumba hiyo itakuwa ya ghorofa moja lenye vyumba vinne vya kulala, sebule, chumba cha kusomea, sehemu ya kulia chakula, maliwato na vibaraza na vyumba na vyumba vya  vya wasaidizi.


Malimi Ameongeza kuwa hadi sasa wanaenda awamu ya pili ya mradi huo ambapo awamu ya kwanza ilianza tarehe 1 mwezi machi, 2022 hadi June 30,2022 buku awamu ya pili ikianza desemba 10 mwaka huu na utakamilika juni 12, 2023.

 

Hata hivyo amesema kuwa licha ya mradi huo kukabiliwa na changamoto ya upandaji bei wa vifaa vya ujenzi pamoja na mvua watahakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili ikamilike kwa muda uliopangwa.


miradi aliyoitembelea ni pamoja na daraja la kitengule wilayani Misenyi, mradi wa barabara wa  Bugene - Burigi wilaya Karagwe Nyakasimbi



  

Wednesday, 14 December 2022

UZALENDO NI TUNU KWA TAIFA KATIBU MKUU MMUYA

 

Pichani:Katibu Mkuu Mteule Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Bwa. Kaspar  Mmuya akizungumza katika sherehe ya Mahafali ya 40 ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare kilichopo Wilaya ya Musoma Mkoani Mara.

Na Mwandishi wetu- Mara

Wasomi na vijana wamekumbushwa umuhimu wa kuwa wazalendo, kujenga ,kuiendeleza na kuilinda Nchi na watu wake kwaajili ya maslahi ya Maendeleo ya Taifa.

Akizungumza katika sherehe ya Mahafali ya 40 ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare kilichopo Wialaya ya Musoma Mkoani Mara Katibu Mkuu Mteule Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Bwa. Kaspar  Mmuya amesema mustakabali wa Maendeleo ya Taifa lolote Duniani unategemea mchango wa Taasisi za mafunzo katika kuandaa wataalam wenye weledi ambao ndio chachu ya kuleta mageuzi ya kifikra na maendeleo Jumuishi na endelevu kwa Jamii.

"Wizara inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Chuo hiki katika kuandaa wataalam wa fani ya maendeleo ya jamii ambao ndiyo injini ya kutafuta suluhisho la changamoto za maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kiteknolojia, kiutamaduni, kisiasa na kimazingira kwa kutumia rasilimali zinazoizunguka jamii, hivyo mafunzo yanayotolewa hapa sharti yaakisi mipango ya nchi na vipaumbele vya jamii ili kuleta matokeo chanya ya maendeleo" Amesema Katibu Mkuu huyo.

Pia  Bwa. Mmuya amekipongeza Chuo hicho kwa kuanzisha programu ya uanagenzi ambayo imesisitizwa katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) ya mwaka 2020/2025 ambapo hadi kufikia sasa baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya uanagenzi wamepata ajira katika taasisi na makampuni mbalimbali Nchini.



Aidha Mmuya ametoa rai kwa Chuo kuhakikisha kinafanya utafiti kwa lengo la kuishauri serikali kuhusu changamoto zinazohitaji mabadiliko ya kisera ,kimkakati au kisheria.

"Kwa upande mwingine tafiti zinaweza kuwa na msaada mkubwa katika kubuni na kuboresha zana na mbinu shirikishi za kuhamasisha jamii kUshiriki katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathimini shughuli au miradi ya maendeleo, hivyo jitahidini sana kutekeleza jukumu hilo kwa kiwango kikubwa"Ameeleza.



SERIKALI YAENDELEA NA MIKAKATI YA KUDHIBITI MAGONJWA YA MLIPUKO

 

Pichani:Dkt. James Kengia aKizungumza kwa niaba ya  Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais -TAMISEMI  katika kikao kazi cha Tathmini ya Programu  ya utoaji wa Elimu  ya Afya.

Kutoka Tanga

Serikali inaendelea  kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya, kutoa elimu kwa jamii na kuweka mikakati  thabiti ili kudhibiti  magonjwa ya  mlipuko katika jamii.


Hayo yamesemwa  leo Disemba 14, 2022 na Dkt. James Kengia alipozungumza kwa niaba ya  Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais -TAMISEMI  katika kikao kazi cha Tathmini ya Programu  ya utoaji wa Elimu  ya Afya na Ushirikishwaji wa Jamii katika Majanga mbalimbali ya magonjwa ya mlipuko kinachofanyika mkoani Tanga.



Dkt. Kengia amesema lengo la kikao hicho kinachofanyika chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ni kuwajengea uwezo washiriki,  kufanya tathmini, kubaini changamoto pamoja na  kuweka mikakati  ya namna bora  ya kudhibiti majanga yanayosababishwa na magonjwa ya mlipuko.  


"Nitoe rai kwa wataalam wa afya  kwa ngazi ya jamii, kuendelea kutoa elimu ya magonjwa ya mlipuko kwa wananchi ili mwananchi aweze kujikinga na magonjwa hayo, katika Ugonjwa wa UVIKO-19  tulishirikiana sana na viongozi wa dini katika kutoa  elimu ya tahadhari, tuendelee kushirikiana  nao ili tuwe na uwelewa wa pamoja" amesema Dkt. Kengia


Aidha, amesema  Serikali inaendelea kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa  kuimarisha  miundombinu  ya kutoa huduma za afya, kununua  vifaa tiba pamoja na  kuendelea kuajiri wataalam  wa afya ili kutoa huduma bora kwa wananchi.


Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Idara ya Afya kutoka Idara ya Kinga Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma Wizara ya Afya  Bw. John Yuda amesema, Serikali inao wataalamu ambao wanafanya utafiti katika kutafuta  kinga na tiba sahihi ya magonjwa ya mlipuko ili kudhibiti maambukizi katika jamii hivyo amewataka wananchi kuendelea kuwasikiliza wataalamu wa afya  kwa kuchukua tahadhari  na kujikinga na magonjwa ya mlipuko ukiwemo  ugonjwa tishio wa Ebola ambao upo katika nchi jirani.


Naye Mwakilishi kutoka Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais – TAMISEMI Bi. Chipole Mpelembe amesema mafunzo hayo  ya siku tatu yatasaidia  kuongeza weledi na mbinu bora za kuongeza uwajibikaji katika kudhibiti  magonjwa ya mlipuko.



Kikao kazi hicho kimewashirikisha, Wizara ya Afya kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, Waratibu Afya Jamii kutoka mikoa 13 ya Tanzania Bara iliyopo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola, Wadau wa Maendeleo na Watafiti.


UTAFITI WA MBEGU UZINGATIE HALI YA HEWA DKT.JINGU

  

PichaniKatibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu wakati akifungua  warsha ya kuelimisha wadau.

Kutoka Dodoma

Watafiti wa masuala ya kilimo nchini wametakiwa kutumia matokeo ya utafiti wao wanaofanya  katika kuboresha mbegu bora za mazao zinazoendana na mabadiliko ya tabia nchi ili  kuwa na tija katika sekta .


Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu wakati akifungua  warsha ya kuelimisha wadau kuhusu Kazi za Muunganiko wa Taasisi za Kimataifa za Utafiti wa Kilimo (CGIAR) Jijini Dodoma.


Dk. Jingu amesema  lengo kuu la warsha hiyo ni kuongeza kasi ya utekelezaji wa programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) kwa kuboresha uratibu wa miradi ya OneCGIAR kwa kuzingatia utafiti utakaongeza uzalishaji.



“Kupitia Mkakati  wa Utafiti na Ubunifu wa Mwaka 2030  CGIAR imeanzisha  mkakati unaojulikana kama OneCGIAR ambao unalenga kufanya utafiti na maendeleo sasa ili tukuze sekta zetu za kilimo, mifugo na uvuvi lazima tuwekeze katika utafiti na maendeleo hivyo  mkakati huu utasaidia katika uzalishaji na tija,” Amesema Katibu Mkuu huyo.


Pia alihimiza kwamba utafiti wa mbegu unaofanyika  usaidie  kuleta tija na faida katika shughuli za wakulima, wavuvi na wafugaji pamoja na kuendeleza ugunduzi wa mbegu mpya hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya hali ya hewa.


“Hivi karibuni  kumekuwa na mabadiliko ya hali ya hewa hivyo utafiti tunaoufanya uendane na hali ya hewa ya kipindi husika ukizingatia  sasa hivi misimu ya mvua imebadilika  kwahiyo tunahitaji mbegu zinazoendana na mazingira na namna ya kukabiliana na wadudu waharibifu,”Alieleza .


Katika hatua nyingine alisisitiza ushirikishwaji wa vijana katika sekta ya kilimo akisema licha ya uwepo wa sekta zingine kilimo kitaweza kustawi na kuleta matokeo chanya kwa wananchi endapo vijana watawezeshwa kikamilifu.


“Vijana ili washiriki vizuri  kilimo wanahitaji elimu , mafunzo kwa vitendo na namna ya kutumia fursa ya ukuaji wa teknolojia katika shughuli zao za uzalishaji wenye matokeo chanya na wafanye kwa tija itasaidia vijana kujikwamua kiuchumi wao wenyewe na kushiriki katika pato la Taifa,”Alisisistza Dk. Jingu.



Tuesday, 13 December 2022

JITIHADA ZA SERIKALI KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA KWA WAZEE MULEBA ZALETA TIJA CHANJO YA COVID 19.

Pichani:Mratibu wa chanjo halmashauri ya wilaya ya Bukoba Yohana Buluba.


Na Lydia Lugakila, 

Kagera.


Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera imepongeza jitihada za serikali na mashirika mbali mbali kwa juhudi za kutoa elimu ya chanjo ya Covid 19 kwa makundi ya wazee, vijana na wanawake katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba na Muleba.


Alielezea hatua iliyofikiwa na halmashauri ya wilaya ya Bukoba mratibu wa chanjo wa wilaya hiyo  Yohana Buluba amesema wamefanikiwa kuwachanja watu  laki1, 92, 384 sawa na asilimia 92 ya watu ambao wamelengwa kupatiwa huduma hiyo kwa mwaka 2022.


Akizungumza na vyombo vya habari Buluba amesema kuwa halmashauri hiyo ililenga kutoa chanjo ya UVIKO 19 kwa watu laki 207,656


 amesema hadi sasa wamefanikiwa pakubwa kutokana na mikakati ya serikali juu ya uhamasishaji wa chanjo hiyo  kwa kushirikiana na wadau mbali mbali likiwemo shirika la kwa wazee wilayani Muleba chini ya ufadhili wa help Age Germany kupitia Help Age international hapa nchini.


Amesema kuwa hadi sasa wanaume ambao tayari wamejitokeza kuchanja ni elfu 84, 649 wanawake 107, 735 ambapo malengo yao  kufikia Desemba 31 mwaka huu wawe wamechanja watu 207,656.


Ameongeza kuwa kupitia njia mbali mbali ya kuelimisha kuhusu umuhimu wa chanjo ya ZUVIKO 19 kwa kushirikiana na viongozi  wa dini serikali za vijiji na mitaa, vitongoji pamoja na viongozi wengine wa serikali, na mashirika ndo jambo lililopelekea mafanikio makubwa.


Aidha amesema kuwa katika halmashauri ya wilaya Bukoba kwa sasa muitikio kwa wanaopata chanjo hiyo ni mkubwa tofauti na ilivyokuwa awali kwani wananchi walikuwa hawajapa uelewa wa kutosha ambapo kulingana na elimu iliyotolewa wananchi wamepata uelewa kuhusiana na chanjo hiyo.


Kufuatia hali hiyo mratibu huyo ameipongeza mradi wa UVIKO 19 unaotekelezwa na shirika la KWA WAZEE wilayani Muleba mkoani hapa ambao umeendelea kuongeza utayari kwa wananchi kupata chanjo dhidi ya UVIKO 19 katika kata mbali mbali za halmashauri ya wilaya ya Bukoba.


 Akitoa mafunzo dhidi ya UVIKO 19 afisa mradi kutoka shirika la kwa wazee Jovinary Frances  amesema kuwa wanafanya shughuli ya kutoa elimu ya UVIKO 19 kwa kusaidiana na serikali bado huku akitaja kuwa wanakumbana na changamoto kutokana na baadhi ya wananchi ambao bado hawajachanja kuhitaji elimu zaidi kwa kushirikiana na Halmashauri.


Kwa upande wa wazee walioshiriki katika mafunzo hayo kutoka kata ya Bujugo wakiwemo Merrynes Revelian, Adelitus Bitegeko wameishuku  Help Age international Tanzania kwa utoaji elimu uliosaidia kuwaondolea hofu  huku wakiitaka jamii kuondoa dhana potofu pale serikali na wadau wanapoonyesha jitihada kuleta mabadiliko katika jamii.


 Hata hivyo Naye Diwani wa kata ya Bujugo Anatory Mwoleka ameishukuru serikali kwa hatua zilizochukuliwa za kuwaelimisha wananchi kwani awali hawakuwa na elimu sahihi hivyo kupitia mashirika  mbali mbali amewashauri wananchi kuendelea kupata chanjo huku akiiomba serikali kuendelea na mwendo huo huo ili kuelimisha wananchi kuchanja zaidi ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na kutopata chanjo dhidi ya UVIKO 19.

KAIRUKI ATOA ANGALIZO UTEKELEZAJI MRADI WA BOOST

Pichani:Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angela Kairuki.


Kutoka Arusha

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki  amesema hatasita kuwachukulia hatua stahiki kwa  wale wote watakaovuruga, kufuja fedha za ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Shule za Awali na Msingi kwenye utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji wa Elimu ya  Awali na Msingi (BOOST)  

 

Ameyasema hayo leo tarehe 13 Disemba, 2022 wakati akifungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa timu za utekelezaji wa mradi wa BOOST  katika Mikoa ya Singida, Manyara na Arusha, uliofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari ya Ilboru mkoani Arusha. 


“Serikali inapimwa kwa vigezo katika kutekeleza Mradi wa BOOST nchini sitakuwa tayari  kuona fedha  zimetolewa kiasi cha shilingi trilioni 1.15 na kupelekwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa lakini miradi haitekelezwi kwa wakati na fedha hizo kurudishwa, tutakuwa hatujatenda haki kwa wananchi” amesisitiza Waziri Kairuki


Waziri Kairuki amewataka Wajumbe wa mradi huo kuhakikisha fedha zinazotolewa katika utekelezaji wa miradi zinakamilisha miradi iliyopangwa ili kuepusha miradi mingi kutokukamilika huku fedha zikiwa zimekwisha 


Amewataka wajumbe hao kuhakikisha wanaimarisha ushirikiano na jamii katika utekelezaji wa mradi na kutekeleza afua zote za mradi kwa wakati ukiwemo ujenzi wa miundombinu ili kufikia matokeo yaliyokubalika; 


Aidha, amewaagiza Wajumbe hao kuwahamasisha wazazi/walezi kuwapeleka watoto wenye umri wa kuanza shule ili waandikishwe na kuanza shule kwa wakati ili  kuwaepushia  mzigo walimu wa kulazimika kurudia kufundisha mambo yale yale kutokana na wanafunzi wengine kucheleweshwa kuanza shule.

MRADI WA UVIKO 19 KAGERA WAONGEZA UTAYARI WA WANANCHI KUCHANJA.

 

Na Lydia Lugakila, 

Kutoka Kagera.

Pichani:Afisa mradi shirika la kwa wazee Abdon Daud akizungumza katika mdahalo na wazee pamoja na makundi mbalimbali katika utoaji elimu ya UVIKO19 katika kata ya Mikoni halmashauri ya wilaya ya Bukoba.


Mradi wa UVIKO 19 unaotekelezwa na shirika la KWA WAZEE wilayani Muleba mkoani Kagera kwa ufadhili wa Help Age ya Germany kupitia Help Age international hapa nchini umeendelea kuongeza utayari kwa wananchi kupata chanjo dhidi ya UVIKO 19 katika kata ya mikoni halmashauri ya wilaya ya Bukoba.


Akiongoza mdahalo uliolenga kuwapatia elimu na mafunzo dhidi ya UVIKO 19 na uondoaji wa dhana potofu dhidi ya chanjo ya UVIKO 19, afisa mradi kutoka shirika la kwa wazee Abdon Daud amesema kuwa mradi huo umelenga  kuwapatia elimu ya UVIKO 19 wazee, vijana, na wanawake kutokana na makundi hayo kutopata taarifa sahihi kwa wakati  jambo linaloonyesha kupunguza utayari wa kupata chanjo hiyo kwa baadhi ya makundi hayo.


"Utayari huu utaongezeka endapo wananchi watakuwa na uelewa mkubwa kuhusiana na chanjo hiyo ukizingatia kundi la wazee watu, wenye ulemavu na wanawake wanapata changamoto kufika katika vituo vya afya wakati mwingine taarifa huwafikia kwa  shida", alisema Daud.


Mwezeshaji  huyo ameishukuru serikali kwa jitihada za kupambana na janga la UVIKO 19 kwa kuweka mikakati ya kuwawakinga wananchi wake katika kipindi chote licha ya uwepo wa dhana potofu juu ya kinga hiyo ambapo kupitia elimu hiyo makundi hayo yameweka utayari wa kuhitaji huduma hiyo papo hapo.


Naye afisa miradi kutoka shirika kutoka shirika la kwa wazee Edmund Revelian amesema wanafanya shughuli za utekelezaji wa mradi wa UVIKO 19 katika wilaya 2 za mkoa huo ambazo ni Muleba na Halmashauri ya wilaya ya Bukoba huku matarajio yao yakiwa ni kuifikia jamii nzima.


"Lilipokuja suala la chanjo kila mmoja alitafsiri yake sisi kama wadau tunaofanya kazi kwa wazee kwa kushirikiana na halmashauri mbili tunatumia wataalam,maafisa chanjo wa maeneo husika ili kuwawezesha kupeleke elimu sahihi katika jamii"alisema Revelian.


Amewapongeza wazee kwa namna walivyoweza kushiriki katika kuchanja kwa baadhi ya awamu zilizopita na kipindi hiki cha awamu ya mwisho walivyoonesha utayari  baada ya kupata elimu hiyo.


Kwa upande wake muhudumu wa afya ngazi ya jamii katika kata ya Mikoni Eugenius Laulian amesema ni muda sasa kwa wazee kupitia mabaraza yao kuchanja huku akiahidi kuendelea kutoa elimu kwa wale ambao hawajapata chanjo hiyo huku akiwaomba viongozi wa serikali ya kijiji kutoa ushirikiano ili kila mwananchi afikiwe huduma hiyo bila usumbufu.

Pichani:Sehemu ya wazee waliopata mafunzo hayo kutoka kata ya mikoni mkoani Kagera wakimsikiliza mwezesha wa mafunzo hayo.


Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo  baadhi ya mzee hao wakiwemo Alfred Rubagumya, Robert Kambibi, Agnes Christopher na Maria Fabian mwenye umri wa miaka 75 wameishuku  Help Age international Tanzania kwa uwezeshaji uliosaidia kuwafikishia elimu hiyo kupitia maafisa hao.


 Aidha kundi hilo baada ya kupata elimu hiyo wameahidi kuwa balozi wazuri huku wakieleza kuwa tangu wapate chanjo hiyo hakuna aliyepata madhara yoyote kiafya.


Mradi huo unatarajia kuzitembelea kata za Bujugo, Mugajwale, Nyakato, Kaibanja Buendangabo ambapo unatarajiwa  kumalizika mnamo mwezi April mwaka 2023.

Friday, 9 December 2022

MAVUNDE AWATAKA WAJASIRIAMALI WADOGO KUWA WANYENYEKEVU KWENYE SHUGHULI ZAO.

 

      Na ELIZABERTH PAULO DODOMA

Naibu waziri kilimo ambaye ni mbunge wa jimbo la Dodoma mjini amewaasa wajasirimali wadogo wadogo kujifunza Unyenyekevu pindi wanapokua katika shughuli zao. 

Mavunde amesema Hayo leo katika ziara aliyoifanya pamoja na wajasirimali (Mama Lishe ) mkoani Dodoma walipotembelea katika mashamba ya Waziri Mkuu Mstaafu Peter Pinda na kuishukuru familia hiyo kwa Ukarimu wao wa Kutenga muda na kuwapokea.

Ziara hiyo ni katika Kuisherehekea siku maalumu ya kuadhimisha Miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika na sherehe hizo zinafanyika bila kuwepo Kwa shamrashamra zozote kama ilivyo zoeleka na badala yake Mavunde ameitumia siku hii kwa kusaidia kuongezea mama lishe ujuzi katika ujasiria Mali wao.

"Lipo jambo la kujifunza kwa sisi viongozi na kwenu nyie mliofika hapa leo hii tujifunze Unyenyekevu jamani Ukiagalia mzee Pinda kwanafasi alizozishika Ameshawahi kuwa kiongozi mkubwa lakini leo Amekubali nimekuja na mama lishe


na akakubali kututembeza shamba lote kwahiyo hapa ndipo tunajifunza Unyenyekevu.


"Ukiwa kiongozi ukiona watu hawaji kwako hata kuuliza maji ujue unashida kwani kiongozi maana yake ni kupokea watu hivyo mzee Pinda na familia yake wana mioyo ya kipekee na ukarimu mkubwa sana ni wazi kuwa katika hali ya kawaida sisi Wenyewe tu ambaye unaweza kuwa na Ukarimu mkubwa wa kiasi cha familia ya Mzee Pinda ni ukarimu mkubwa sana na ni upendo mkubwa sana". Alisema Mavunde

Aidha Mavunde ametumia ziara Hiyo kutangaza January kufanyika kongamano kubwa la siku ya MWANAMKE DODOMA JIJI ili kutathimi makubaliano ya mwaka mzima Yalipofikia.

" Mimi nimejiitolea kulilea hili kundi ili nione mafanikio Yao kila mmoja kwa nafasi yake nataka nione wanapiga hatua kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine, Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Rais Samia imefanya kazi kubwa ya Kuendeza Dodoma inakua makao makuu Fursa zipo nyingi nataka nione akina mama wa Dodoma wakichangamkia hizi fursa" 

 "Siyafanyi haya ili mnichague kuwa mbunge wenu,Sifanyi siasa nafanya haya kwasababu niliomba dhamana ya kuwa kiongozi Nina wajibu wa kuwasaidia watu wangu".Alisema 

Akizungumza na umati huo Waziri mkuu Mstaafu Kayanza Peter Pinda Amewasihi kushirikiana kuifanya Dodoma kuwa ya Kijani kwani kila mtu mmoja akipanda mti Dodoma itakua na mwonekano mzuri hiyo hudhihirishwa baada ya mvua kunyesha Dodoma inakua na muonekano mzuri hivyo kila mtu alichukue Hilo.

" Niseme tu Tushirikiane katika kupanda miti ili tuifanye Dodoma yetu ipendeze kwani mji ukiwa na kijani kingi ni mji unaovutia sana na kitu kingine mimi huwa napenda kusema mjasiri wa mali na siyo mjasiriamali kwani ukishakua mjasiri wa mali utakua mbali kimaendeleo".

"Anthony naomba niwepo kwenye Hilo kongamano lako unalotaka lifanyike January ili niweze kuhamasisha washiri Hao kupanda miti ." Alisema Pinda

Nao baadhi ya wajasirimali waliozungumza kwa nyakati tofauti wametoa shukrani zao kwa Mavunde kwani hakuna mbunge aliyeifanya tukio kama alichofanya yeye kwa kuwakutanisha na kuwapeleka katika mashamba ya mzee Pinda kwani wamejifunza vitu vingi na kuahidi kwenda kufanyia kazi.

SHULE YA MAKI BRILLIANT YAWATAKA WAZAZI KUSHIRIKI SHEREHE ZA WATOTO ILI KUJIONEA MAENDELEO YAO




Kutoka Dodoma

Shule ya MAKI BRILLIANT iliyopo Kata ya Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma inawakaribisha Wazazi na Walezi wote Siku ya Jumamosi Disemba 10,2022 kushiriki sherehe maalum itakayofanyika Shuleni hapo.


MAKI BRILLIANT PRE AND PRIMARY ENGLISH SCHOOL imesajiliwa  Feb 28 ,2022 ikiwa na wanafunzi tisa (9) ambapo hadi kufikia sasa wana jumla ya wanafunzi 60 kuanzia darasa la kwanza mpaka darasa la Sita.



Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Desemba 8,2022, Jijini Dodoma kuelekea Sherehe hiyo ,Afisa Masoko na Mawasiliano wa Shule hiyo Bi.Josephine Uriyo amesema kuwa lengo la Sherehe hiyo ni kuwakutanisha kwa pamoja wazazi,Walezi,Walimu na wanafunzi ili wapate kujua na kujionea maendeleo ya Watoto wao ikiwemo vipaji mbalimbali.


"Wanafunzi watakuwa na michezo mbalimbali ambapo watapata nafasi ya kuonesha mbele ya wazazi kwa sababu kuna baadhi ya wazazi hawajui kabisa vipaji walivyonavyo watoto wao ila kupitia Sherehe kama hii itakayofanyika Jumamosi ukweli wazazi watafurahia sana,"Amesema Josephine


Bi.Josephine ametoa wito kwa Wazazi na Walezi kutambua umuhimu wa siku hiyo kwa kushiriki na watoto wao ili kujua maendeleo yao ya msingi ya kielimu pamoja na kimaadili.


"Moja ya sifa ya shule yetu inawalea Watoto katika maadili ya Dini na Uzalendo na imekuwa ikifanya vizuri katika matokeo na ufaulu na tuna nyongeza ya kufundisha watoto Kifaransa na Kichina,"


Na Kuongeza kuwa 'Shule yetu pia inatoa Elimu ya awali,yaani Nursery School (Baby,Middle na Pre-Unit) na inapokea watoto kuanzia umri wa miaka mitatu (3) na shule yetu inafuata mtaala wa Wizara ya Elimu,SayansinaTeknolojia ,"Amesema Bi.Josephine


Pia Bi.Josephine amesema kuwa Shule ya MAKI BRILLIANT inapokea watoto kuanzia miaka Mitano (5) na kuendelea kwa darasa la kwanza (01) hadi darasa la sita (6).


Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Buigiri ,Kenneth Yindi amesema kuwa Kata yake Imefungua milango kwa Wawekezaji kwa kiasi kikubwa huku akitolea mfano Shule ya MAKI BRILLIANT kuwa imeongeza idadi kubwa ya Wanafunzi na hayo ni mafanikio ya baadae katika kata yake na taifa kwa ujumla.


"Baada ya Serikali kutangaza kuhamia rasmi Dodoma,  Wawekezaji nao  wakafunguka na kutaka kuwekeza Dodoma hasa katika Wilaya yetu ya Chamwino ambapo ndipo ilipo Ikulu ya Tanzania na kwa bahati nzuri kata yangu nayo ipo Chamwino hivyo kwa sasa Wawekezaji wengi wanakuja na Mimi kama Diwani nawakaribisha na milango ipo wazi,"Amesema Yindi



Uwekezaji Uliofanyika katika kata yake ikiwemo Ujenzi Wa Shule ya MAKI BRILLIANT umeleta maendeleo makubwa kwa Watoto wa kata hiyo kwani wengi wao sasa wanapata elimu bora na yenye maadili hivyo kikubwa ni kuendelea kuwaunga mkono Wawekezaji wanaoendelea kuwekeza katika miradi ya maendeleo ikiwemo hizi shule kwa sababu ni msingi wa watoto kupata elimu.


Lengo la Kuanzishwa kwa shule ya MAKI BRILLIANT katika Kata ya Buigiri Wilayani Chamwino ni kuwasaidia watoto wa kika na wakiume kupata elimu Bora ili kuibui vijana walioelimika na wenye maadili mema pamoja na kuwafundisha ujasiriamali hali ambayo itawasaidia katika maisha yao ya baadae.

Tuesday, 6 December 2022

CHETI CHA KUZALIWA NI HAKI YA KILA MTANZANIA

 

Pichani: Afisa wa usajili na wakala wa usajili,ufanisi na udhamini(RITA) Eminyanda Madunga akizungumza na waandishi wa Habari.

Na.Hamson Mniha. Dodoma

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Wamesema kuwa Jukumu la kuchukuwa Cheti cha kuzaliwa siyo la Mtu Fulani au Serikali ila ni haki ya kila mwananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa wa usajili na wakala wa usajili,ufanisi na udhamini(RITA)Eminyanda Madunga Kwenye uzinduzi wa siku ya Maadili Na haki za Binadamu Kwenye viwanja vya nyerere Square Leo Disemba 6,2022.

Aidha Afisa usajili na wakala wa usajili,ufanisi na udhamini(RITA) Eminyanda Madunga amesema mtu kupata cheti ni haki yake na kuwataka wananchi wajitokeze kupata cheti kwakua ni muhimu kutokana na mahitaji mengi yanategemea cheti Cha kuzaliwa.

"tunachukuwa fulsa hii kuwakaribisha wananchi wote wa jiji la Dodoma kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hili litakalodumu kwa siku 6 kwani nafasi hii inatokea Mara chache Sana wahudumu kusogea maeneo Kama haya". Alisema Eminyanda.



Vilevile serikali imesema Kutokana na Takwimu za Shirika la Amnesty International kuhusu hali ya rushwa nchini zimeonesha kuwa katika mwaka 2021 Tanzania ilipata alama 39 na kupanda kutoka nafasi ya 97 mwaka 2020 hadi nafasi ya 94 kati ya nchi 180.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damasi Ndumbaro wakati wa Uzinduzi wa Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Jijini Dodoma na kusema  serikali ina wajibu wa kusimamia vyema matumizi ya rasilimali za nchi kwa maslahi mapana ya wananchi. 

DPP SYLVESTER MWAKITALU ATAKA HAKI JINAI ISIMAMIWE IPASAVYO KWA MAHABUSU NA WAFUNGWA NCHINI

 

Pichani: Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini DPP Sylvester Mwakitalu Akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi Mbalimbali waliotembelea Gereza kuu la Isanga Dodoma.

DODOMA.

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Mwakitalu ametembelea Gereza Kuu la Isanga jijini Dodoma kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili Maafisa wa Magereza katika kuwatunza wafungwa pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili mahabusu.

Akizungumza  baada ya kutembelea Gereza Kuu la Isanga Mkurugenzi  wa Mashtaka amesema kuwa lengo la  kutembelea wafungwa na mahabusu ni kuona Haki Jinai inasimamiwa ipasavyo kwa misingi ya sheria na kanuni zake.

'’kufanya haya yote ni kuona haki jinai inasimamiwa ipasavyo lakini tukipata hizi changamoto na kuzisikiliza tunaenda kuzifanyia kazi na kuzishughulikia. Changamoto tulizozipokea ambazo hazipo chini ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka tunazichukua na kuzipeleka ofisi ambazo zinahusika lengo ikiwa ni kuona Haki Jinai inasimamiwa ipasavyo.Amesema DPP Mwakitalu



Hata hivyo,Mwakitalu amezitaja changamoto ambazo  amezipokea katika ziara yake ambapo mahabusu wamezieleza ikiwa ni sula zima la ucheleweshwaji wa kesi na kuchelewa kwa upelelezi ambapo ameeleza kuwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeendelea kuzishughulikia changamoto hizo kwa kuhakikisha kuwa wameshasajili Hati za Mashtaka Mahakama Kuu ambazo hivi sasa zipo katika mchakato wa kusikilizwa.

'’Mahabusu wengi ambao nimewasikiliza  wamesema kesi zao zimechelewa upelelezi ,lakini hali halisi ni kwamba kesi zao hazijachelewa upelelezi kwa kuwa tayari zimekamilika na kinachosubiriwa ni  utaratibu wa kisheria ambao utawezesha kesi hizo kusikilizwa na Mahakama Kuu Amesema DPP Mwakitalu.



Ofisi ya Taifa ya Mashtaka nchini imeanza mwendelezo wa ziara zake katika Magereza mbalimbali nchini kwa lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili Maafisa wa Magereza, wafungwa pamoja na mahabusu ili kuhakikisha Haki Jinai inasimamiwa ipasavyo kwa mujibu wa Ibara ya 59B ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.



Monday, 5 December 2022

RAIS SAMIA ASITISHA MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU


pichani:Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt.Samia Suluhu Hassan.


Na Deborah  Lemmubi - Dodoma.


Imeelezwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt.Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuwa fedha zote kiasi cha Milioni 960 zilizokuwa zimetengwa na Wizara na Taasisi kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe za Uhuru mwaka huu 2022 zipelekwe Ofisi ya Raisi Tamisemi na zitatumika kujenga mabweni katika shule nane (8) za Msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum hapa Nchini.

Hayo yamesemwa leo hii na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe George Simbachawene wakati akizungumza na wanahabari kuhusu Maadhimisho ya miaka 61 Uhuru ambapo amesema kuwa Maadhimisho ya Sherehe hizi kwa Tanzania Bara mwaka huu 2022 zitafanyika kwa njia ya Midahalo na Makongamano mbalimbali yatakayofanyika katika Wilaya zote hapa Nchini kujadili, kutafakari kwa pamoja na kukumbuka tulikotoka, tulipo na tunakoelekea kuhusu Maendeleo Endelevu ambayo Nchi yetu adhimu Tanzania imeyafikia.

"Midahalo na Makongamano hayo itatanguliwa na ratiba mbalimbali kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya kufanya shughuli za Kijamii kama vile kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali, shule, nyumba za Wazee na makundi yenye mahitaji maalum. Hivyo, sherehe za mwaka huu hakutokuwa na Gwaride na shughuli nyingine za Kitaifa,"


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dodoma.

Na kuongeza kuwa "Midahalo na Makongamano hayo itatanguliwa na ratiba mbalimbali kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya kufanya shughuli za Kijamii kama vile kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali, shule, nyumba za Wazee na makundi yenye mahitaji maalum. Hivyo, sherehe za mwaka huu hakutokuwa na Gwaride na shughuli nyingine za Kitaifa"

Aidha Waziri Simbachawene amezitaja shule hizo kuwa ni shule ya msingi Buhangija (Shinyanga), Goweko (Tabora),Darajani (Singida), Mtanga (Lindi), Songambele (Manyara), Msanzi (Rukwa), Idofi (Njombe), na shule ya msingi Longido (Arusha).

Mhe.Simbachawene amesema kuwa Maadhimisho ya Sherehe za miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara mwaka huu 2022 yataadhimishwa kwa Kauli mbiu inayosema:- MIAKA 61 YA UHURU: AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU.

Waziri huyo ameongeza kuwa Kauli mbiu hiyo inaonyesha nia ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha uchumi unaojikita katika Maendeleo ya watu kwa kufanya mabadiliko katika sekta zote za kiuchumi na kijamii ili kufikisha neema na Maendeleo.


Sunday, 4 December 2022

FAHODE YAACHA ALAMA KAGERA.

 

Pichani:  Mkurugenzi wa shirika la (FAHODE) Shakira Omary Akizungumza katika Hafla ya miaka mitano tokea Imeanzishwa Taasisi hiyo.

Na Lydia Lugakila, Kagera


Shirika lisilo la kiserikali la Faraja for hope and Development Organization (FAHODE) linaloihudumia jamii kupitia miradi ya maendeleo katika manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera limeadhimisha miaka mitano huku likijivunia namna lilivyofanikiwa kuijengea uwezo jamii.


Akizungumza katika Hafla ya miaka mitano  mkurugenzi wa shirika hilo Shakira Omary amesema kuwa wanapoadhimisha miaka mitano wanajivunia kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa thamani ya ujana uliosaidia kutoa elimu ya kujitambua na kuepuka mimba za utotoni kwa vijana walioko mashuleni kwa shule za sekondari Kashai, Bilele, Hamgembe Nshambya na  Mugeza


Ameitaja baadhi ya imiradi mingine waliyoitekeleza kuwa ni Nishike mkono,  uliwasaidia watoto  wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapatia vifaa vya shule, ufuatiliaji wa uwajibikaji wa jamii, pamoja na miradi mingine.


Shakira amesema kuwa dira ya shirika hilo kuona jamii iliyoelimika na iliyojikomboa dhidi ya umaskini na kuimalisha ustawi wa maendeleo.


Aidha amezitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na ukosefu wa raslimali fedha kwa ajili ya kuendesha miradi isiyo na wafadhili, ukosefu wa watumishi huku mikakati yao ikiwa ni kufungua SACCOS ambayo lengo lake ni kuwaelimisha wanawake na vijana kujua umuhimu wa kuweka akiba na kukopa ili faida itakayopatikana isaidie katika shughuli za shirika.


Kwa upande mgeni rasmi katika sherehe hizo Erasto Medard afisa tarafa Katerero amelishukuru shirika hilo kwa namna lilivyopambana katika kutekeleza miradi hiyo na kuziomba taasisi na mashirika kutoa ushirikiano ili kulifanya shirika hilo linatimiza vyema malengo yake.


Hata hivyo Mwenyekiti wa shirika hilo Antidius Augustine amesema hadi sasa shirika hilo limeacha alama katika jamii kwani wameguswa maisha ya watu.

Saturday, 3 December 2022

PROF.MDOE ATOA SIRI YA KISWAHILI KUPAA KIMATAIFA

Pichani: Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu  Prof.James Mdoe akikabidhiwa kitabu na Bi.Menna Yasser Jana Disemba 3,2022 kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari bikini Dodoma.

 Kutoka Dodoma 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia,ipo katika hatua za kuimarisha nguvu ya kueneza matumizi ya Lugha ya Kiswahili kupitia mafunzo yatakayo ongeza hamasa kwa lugha ya Kiswahili zaidi ya inavyotumika kwa sasa.


Hayo yameelezwa  na  Prof.James Mdoe wakati wa hafla fupi ya kuzindua Sherehe za maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru yanayokwenda sambamba na Matumizi ya Kiswahili ,Disemba 3,2022,Jijini Dodoma.

Aidha Prof.Mdoe amesema kuwa ,Kuelekea maadhimisho hayo yanayofanyika Disemba 9 2022 ,Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatarajia kupandisha Bango la Kiswahili katika Mlima Kilimanjaro lengo likiwa ni kueneza lugha hiyo Kwa mataifa mengi zaidi Duniani.

"Lengo la kufanya hivyo ni kusherehekea Uhuru wa Nchi yetu kwa kutangaza Lugha yetu Kwa mataifa mengine ndio maana bango hili litapandishwa na kusimikwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kama ambavyo ulisimikwa Mwenge wa uhuru,"


Prof.Mdoe ameongeza kuwa kwa sasa watumiaji wa Lugha ya Kiswahili Duniani wanakadiriwa kuwa takribani milioni 250 na lengo ni kuhakikisha ifikapo mwakani wakati wa maadhimisho hayo idadi ya watu wanaotumia Lugha ya kiswahili iwe imeongezeka

Ameongeza kuwa "Wameandaliwa vijana wawili shupavu ambao watakwenda kusimika Bango lenye kauli mbiu "Kiswahili Kileleni" kwenye kilele Cha mlima Kilimanjaro siku ya maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania,"Amesema Prof.Mdoe




Vilevile Prof.Mdoe amesema kuwa mpaka sasa kuna vyuo zaidi ya 150 duniani zinazofundisha Lugha ya kiswahili na vituo 300 vya Radio na Runinga Duniani vyenye vipindi vya Lugha ya Kiswahili.

Prof.Mdoe ametumia muda huo kutoa wito kwa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika Mataifa mbalimbali kuendelea kuchochoe matumizi ya Lugha ya kiswahili katika mataifa hayo ikiwemo kufungua madarasa ya awali ya kufundisha Lugha ya kiswahili.

"Nchini Malawi tumefungua tayari Darasa la kufundisha Lugha ya kiswahili na imewezekana kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini humo ndio maana natoa wito kwa Mabalozi wengine kufany hivyo ili kuendelea kukuza lugha yetu kimataifa,"Ameeleza Prof.Mdoe

Kwa Muktadha huo Bi.Menna Yasser ambaye ni Raia ya Misri na Mwandishi wa kitabu cha kwanza kilichoandikwa kwa lugha ya kiswahili nchini humo amesema kuwa matumizi ya lugha ya kiswahili inazidi kukuwa kwani kuna baadhi ya Nchi kwa sasa zimeendelea kukitambua kiswahili kama lugha ya kutumiwa katika mataifa yao.

Amesema kuwa Lugha ya Kiswahi inazidi kukuwa kwa kasi kwani kwa sasa kuna baadhi ya vyuo nchini Misri zinafundisha Kiswahili na mataifa kama Uganda,Sudan Kusini na mataifa mengine ya Ukanda wa mashariki na kusini Mwa Afrika zinatumia kiswahili kama lugha mojawapo ya mawasiliano.

"Kiswahili lazima kifike Kileleni kwa sababu nia ipo na naona Wizara imejidhatiti kuhakikisha kiswahili kinaendelea kuvuka mipaka zaidi,"Amesema Bi.Menna

PROF. SHEMDOE AWATAKA WAHITIMU KUTUMIA FURSA ZA KIUCHUMI

 

Pichani: Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe akizungumza na wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha.
Pichani: Wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha.


Na Mwandishi wetu Kibaha


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe amewataka wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (KFDC) kutumia fursa zilizopo kujiajiri ili kuongeza kipato na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja, jamii na Taifa kwa ujumla.


Hayo ameyasema tarehe 02/12/2022 kwenye sherehe za mahafali ya 50 ya KFDC zilizofanyika katika Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, Mkoani Pwani.


“Ndugu wahitimu, leo hii mnahitimu mafunzo yenu ya miaka miwili hapa chuoni pia wapo wale wanaohitimu mafunzo ya miezi mitatu yaliyotolewa kwa njia ya masafa ambayo yamewanufaisha wananchi wengi, nilipopita kwenye maonesho ya fani nimeshuhudia jinsi vijana mlivyoiva kiufundi katika fani mbalimbali. 


Nawapongeza sana kwa kupata ujuzi katika fani hizo natarajia kuwa ujuzi mliopata chuoni hapa mtautumia popote mtakapo pata ajira au mtakapokuwa mmejiajiri.


Prof. Shemdoe amewaeleza wahitimu kuwa ujuzi walioupata ukawasaidie kupiga hatua zaidi kimaisha na kuwataka  kujiunga kwenye vikundi ili kuweza kupata fedha za mitaji kupitia mikopo ya asilimia kumi ya mapato kwenye kila Halmashauri ambazo hazina riba yoyote. 


"waliopata ujuzi wa ufundi uwashi muende kuomba kazi za miradi katika Halmashauri zetu kwa kuwa mna ujuzi na vyeti huko kuna miradi mingi ya ujenzi” amesema Prof. Shemdoe.


Awali akitoa taarifa ya KFDC  Mkuu wa Chuo hicho Bw. Joseph Nchimbi ameeleza kuwa chuo hicho kinatoa mafunzo ya fani za ujuzi wa aina mbalimbali pia alieleza jumla ya wanachuo 383 wa kozi ndefu wakiwemo 235 mwaka wa kwanza na 170 mwaka wa pili.


“Chuo kimefanikiwa kuanzisha kozi fupi zaidi ya kumi ambazo zinatolewa kwa njia ya kiswahili na kuwafikia idadi kubwa ya wanufaika kwa wakati mmoja,” alisema Bw. Nchimbi.


Bw. Nchimbi amefafanua mafanikio ya chuo kwa  kutoa mafunzo ya nadharia na vitendo kwa wanafunzi wa muda mrefu na muda mfupi na kufanya vizuri katika mitihani yao ya VETA na wahitimu  kupata ajira katika taasisi mbalimbali na kujiajiri pia.


“Fani zinazotolewa na KFDC ni ufundi bomba, ufundi wa umeme majumbani, ufundi wa magari, ufundi wa uungaji na uundaji vyuma,  ufundi wa uwashi, ufundi wa useremala, ufundi wa ushonaji nguo na ubunifu wa mavazi, kilimo cha bustani na mazao mbalimbali, ufugaji, hotelia na udereva,” alisema Bw. Nchimbi.

Friday, 2 December 2022

WAHITIMU ELIMU YA JUU WAASWA KUJIFUNZA KWA WALIOFANIKIWA.

Pichani:Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi Jenifa Omolo na mgeni kwenye Mahafali ya 36 chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Kilichopo Jijini Dodoma.

PichaniWahitimu wa Kozi mbalimbali waliohudhulia kwenye Mahafali ya 36 chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Kilichopo Jijini Dodoma.

Pichani: Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi Jenifa Omolo akimpongeza Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Prof. Hozen Mayaya kwenye Mahafali ya 36 Jijini Dodoma.


Na Deborah kutoka Dodoma

Wahitimu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kilichopo Jijini Dodoma wameaswa kujikita katika malengo yao na kuacha kuangalia walioshindwa na kuanguka badala yake wajifunze kwa waliofanikiwa ili na wao waweze kuwa wenye mafanikio.


Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi Jenifa Omolo akiwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Lameck Nchemba katika mahafali ya 36 ya chuo hiki cha Mipango ya Maendeleo Vijijini yaliyofanyika Jijini Dodoma.


"Msiwe na mawazo tofauti kwamba kuna mwingine alihitimu mwaka jana na hajapata kazi, wewe jikite kwenye malengo yako usiangalie mtu kaanguka, kila mtu ana malengo yake. Mwingine alianza biashara kaanguka wewe hiyo sio kazi yako hujui kilichomfanya aanguke,watu wameanza makampuni wameshindwa kuendelea . Usiangalie kufeli angalia mafanikio hapo utafanikiwa,usiangalie jirani yako ameanzisha sijui kitu gani kimeanguka ,usiende kujifunza huko, jifunze kwa waliofanikiwa"


Aidha Bi Jenifa amewataka Wahitimu na wale wanafunzi watakaoendelea na mafunzo kwa ngazi ya juu kuwa na chachu ya kuendelea kujifunza ili kuongeza maarifa,ujuzi na ubunifu unaohitajika katika kuboresha utendaji wao wa kazi.


"Ni matumaini yangu kuwa mtathibitisha vema maarifa ya ujuzi mliyopa hapa Chuo cha Mipango Kwenye ulimwengu wa kazi, niwakumbushe kuwa mafanikio katika ulimwengu wa leo wa kazi yanahitaji moyo wa kupenda kuendelea kuwa na chachu ya kujifunza ili kuongeza Maarifa,Ujuzi na Ubunifu unaohitajika katika kuboresha utendaji wenu wa kazi"


"Na kuongeza kuwa, na wale mtakaoendelea na ngazi ya juu katika masomo Nawaasa mkaendelee kujifunza kwa bidii ili kupata maarifa na ujuzi utakaowezesha kuhimili Mazingira ya ulimwengu wa kisasa kwa kazi ya Maendeleo ya kiuchumi ya Familia zetu na Taifa kwa ujumla".


 Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Mipango Vijijini Prof. Hozen Mayaya ameeleza mafanikio waliyoyapata kwa mwaka 2021/2022 katika miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Mabweni na Kumbi za mihadhara kwa kutumia fedha za vyanzo vya ndani ya chuo na Ruzuku kutoka Serikalini na kueleza matarajio yao ya 2022/2023 ya kujenga Maktaba kubwa na ya kisasa pamoja na bweni la wanafunzi katika eneo la Kisesa Jijini Mwanza.


"Matarajio yetu kwa mwaka 2022/2023 ni kuanza ujenzi eneo la Miyuji Bweni na Kantini, aidha tunategemea kuanza ujenzi wa maktaba kubwa ya kisasa kule Mjini Mwanza pamoja na bweni la wanafunzi "


"Ameongeza kuwa,chuo kimetekeleza jumla ya miradi 8 ya ujenzi kwa fedha za ruzuku kutika Serikalini, Mabweni 2 na Kumbi za mihadhara 3 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 9.7. Miradi inayotekelezwa na mapato ya ndani ya chuo ni miradi 3 ikiwemo jengo la Mgahaw, jengi la Utawala na Maktaba kwenye kituo cha mafunzo cha kanda ya Ziwa Mwanza yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.2"


"Katika mafanikio ya 2021/2022 pia tumefanya upanuzi maeneo ya chuo katika kituo cha mafunzo Mwanza ikiwemo kulipa fidia kwa wananchi waliopisha maeneo, hii inaendana na ongezeko la wanafunzi watakaofanya udahili nayo thamani ni Bilioni 1.7 kutoka katika vyanzo vya ndani vya chuo"


Akisoma hotuba kwa niaba ya wanafunzi wenzake muhitimu Gift Kyando wa kozi ya Bachelor Degree In Environmental Planning and Management, kwanza ameishukuru Serikali na Wizara ya Fedha na Mipango ambayo ni Wizara Mama ya chuo chao na kuomba Chuo kuendelea kuwasaidia ili waweze kusonga mbele zaidi hasa wanapohitaji kupata Barua za uthibitisho kutoka Chuoni hapo.


"Kwanza kabisa kwa niaba ya wanafunzi wenzangu tunaohitimu leo tunaishukuru Serikali yetu na Wizara ya fedha ambayo ndio Wizara Mama ya Chuo chetu cha Mipango lakini pia thnaomba Chuo kiendelee kutusaidia katika mambo mbalimbali tutakayohitaji ili kuendelea kusonga mbele hasa pale tutakapohitaji kupata Barua za uthibitisho kutoka chuoni hapa"


Haya ni mahafali ya 36 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini ya mwaka 2022 ambapo wanafunzi 6225 wamehitimu wakiwemo wanaume 2722 na wanawake 3502 katika fani mbalimbali za Maendeleo vijijini.

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...