mwambelablog

Tuesday, 13 December 2022

JITIHADA ZA SERIKALI KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA KWA WAZEE MULEBA ZALETA TIJA CHANJO YA COVID 19.

Pichani:Mratibu wa chanjo halmashauri ya wilaya ya Bukoba Yohana Buluba.


Na Lydia Lugakila, 

Kagera.


Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera imepongeza jitihada za serikali na mashirika mbali mbali kwa juhudi za kutoa elimu ya chanjo ya Covid 19 kwa makundi ya wazee, vijana na wanawake katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba na Muleba.


Alielezea hatua iliyofikiwa na halmashauri ya wilaya ya Bukoba mratibu wa chanjo wa wilaya hiyo  Yohana Buluba amesema wamefanikiwa kuwachanja watu  laki1, 92, 384 sawa na asilimia 92 ya watu ambao wamelengwa kupatiwa huduma hiyo kwa mwaka 2022.


Akizungumza na vyombo vya habari Buluba amesema kuwa halmashauri hiyo ililenga kutoa chanjo ya UVIKO 19 kwa watu laki 207,656


 amesema hadi sasa wamefanikiwa pakubwa kutokana na mikakati ya serikali juu ya uhamasishaji wa chanjo hiyo  kwa kushirikiana na wadau mbali mbali likiwemo shirika la kwa wazee wilayani Muleba chini ya ufadhili wa help Age Germany kupitia Help Age international hapa nchini.


Amesema kuwa hadi sasa wanaume ambao tayari wamejitokeza kuchanja ni elfu 84, 649 wanawake 107, 735 ambapo malengo yao  kufikia Desemba 31 mwaka huu wawe wamechanja watu 207,656.


Ameongeza kuwa kupitia njia mbali mbali ya kuelimisha kuhusu umuhimu wa chanjo ya ZUVIKO 19 kwa kushirikiana na viongozi  wa dini serikali za vijiji na mitaa, vitongoji pamoja na viongozi wengine wa serikali, na mashirika ndo jambo lililopelekea mafanikio makubwa.


Aidha amesema kuwa katika halmashauri ya wilaya Bukoba kwa sasa muitikio kwa wanaopata chanjo hiyo ni mkubwa tofauti na ilivyokuwa awali kwani wananchi walikuwa hawajapa uelewa wa kutosha ambapo kulingana na elimu iliyotolewa wananchi wamepata uelewa kuhusiana na chanjo hiyo.


Kufuatia hali hiyo mratibu huyo ameipongeza mradi wa UVIKO 19 unaotekelezwa na shirika la KWA WAZEE wilayani Muleba mkoani hapa ambao umeendelea kuongeza utayari kwa wananchi kupata chanjo dhidi ya UVIKO 19 katika kata mbali mbali za halmashauri ya wilaya ya Bukoba.


 Akitoa mafunzo dhidi ya UVIKO 19 afisa mradi kutoka shirika la kwa wazee Jovinary Frances  amesema kuwa wanafanya shughuli ya kutoa elimu ya UVIKO 19 kwa kusaidiana na serikali bado huku akitaja kuwa wanakumbana na changamoto kutokana na baadhi ya wananchi ambao bado hawajachanja kuhitaji elimu zaidi kwa kushirikiana na Halmashauri.


Kwa upande wa wazee walioshiriki katika mafunzo hayo kutoka kata ya Bujugo wakiwemo Merrynes Revelian, Adelitus Bitegeko wameishuku  Help Age international Tanzania kwa utoaji elimu uliosaidia kuwaondolea hofu  huku wakiitaka jamii kuondoa dhana potofu pale serikali na wadau wanapoonyesha jitihada kuleta mabadiliko katika jamii.


 Hata hivyo Naye Diwani wa kata ya Bujugo Anatory Mwoleka ameishukuru serikali kwa hatua zilizochukuliwa za kuwaelimisha wananchi kwani awali hawakuwa na elimu sahihi hivyo kupitia mashirika  mbali mbali amewashauri wananchi kuendelea kupata chanjo huku akiiomba serikali kuendelea na mwendo huo huo ili kuelimisha wananchi kuchanja zaidi ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na kutopata chanjo dhidi ya UVIKO 19.

No comments:

Post a Comment

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...