Na Deborah Lemmubi - Dodoma.
Imeelezwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt.Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuwa fedha zote kiasi cha Milioni 960 zilizokuwa zimetengwa na Wizara na Taasisi kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe za Uhuru mwaka huu 2022 zipelekwe Ofisi ya Raisi Tamisemi na zitatumika kujenga mabweni katika shule nane (8) za Msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum hapa Nchini.
Hayo yamesemwa leo hii na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe George Simbachawene wakati akizungumza na wanahabari kuhusu Maadhimisho ya miaka 61 Uhuru ambapo amesema kuwa Maadhimisho ya Sherehe hizi kwa Tanzania Bara mwaka huu 2022 zitafanyika kwa njia ya Midahalo na Makongamano mbalimbali yatakayofanyika katika Wilaya zote hapa Nchini kujadili, kutafakari kwa pamoja na kukumbuka tulikotoka, tulipo na tunakoelekea kuhusu Maendeleo Endelevu ambayo Nchi yetu adhimu Tanzania imeyafikia.
"Midahalo na Makongamano hayo itatanguliwa na ratiba mbalimbali kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya kufanya shughuli za Kijamii kama vile kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali, shule, nyumba za Wazee na makundi yenye mahitaji maalum. Hivyo, sherehe za mwaka huu hakutokuwa na Gwaride na shughuli nyingine za Kitaifa,"
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dodoma.
Na kuongeza kuwa "Midahalo na Makongamano hayo itatanguliwa na ratiba mbalimbali kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya kufanya shughuli za Kijamii kama vile kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali, shule, nyumba za Wazee na makundi yenye mahitaji maalum. Hivyo, sherehe za mwaka huu hakutokuwa na Gwaride na shughuli nyingine za Kitaifa"
Aidha Waziri Simbachawene amezitaja shule hizo kuwa ni shule ya msingi Buhangija (Shinyanga), Goweko (Tabora),Darajani (Singida), Mtanga (Lindi), Songambele (Manyara), Msanzi (Rukwa), Idofi (Njombe), na shule ya msingi Longido (Arusha).
Mhe.Simbachawene amesema kuwa Maadhimisho ya Sherehe za miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara mwaka huu 2022 yataadhimishwa kwa Kauli mbiu inayosema:- MIAKA 61 YA UHURU: AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU.
Waziri huyo ameongeza kuwa Kauli mbiu hiyo inaonyesha nia ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha uchumi unaojikita katika Maendeleo ya watu kwa kufanya mabadiliko katika sekta zote za kiuchumi na kijamii ili kufikisha neema na Maendeleo.
No comments:
Post a Comment