mwambelablog

Tuesday, 13 December 2022

MRADI WA UVIKO 19 KAGERA WAONGEZA UTAYARI WA WANANCHI KUCHANJA.

 

Na Lydia Lugakila, 

Kutoka Kagera.

Pichani:Afisa mradi shirika la kwa wazee Abdon Daud akizungumza katika mdahalo na wazee pamoja na makundi mbalimbali katika utoaji elimu ya UVIKO19 katika kata ya Mikoni halmashauri ya wilaya ya Bukoba.


Mradi wa UVIKO 19 unaotekelezwa na shirika la KWA WAZEE wilayani Muleba mkoani Kagera kwa ufadhili wa Help Age ya Germany kupitia Help Age international hapa nchini umeendelea kuongeza utayari kwa wananchi kupata chanjo dhidi ya UVIKO 19 katika kata ya mikoni halmashauri ya wilaya ya Bukoba.


Akiongoza mdahalo uliolenga kuwapatia elimu na mafunzo dhidi ya UVIKO 19 na uondoaji wa dhana potofu dhidi ya chanjo ya UVIKO 19, afisa mradi kutoka shirika la kwa wazee Abdon Daud amesema kuwa mradi huo umelenga  kuwapatia elimu ya UVIKO 19 wazee, vijana, na wanawake kutokana na makundi hayo kutopata taarifa sahihi kwa wakati  jambo linaloonyesha kupunguza utayari wa kupata chanjo hiyo kwa baadhi ya makundi hayo.


"Utayari huu utaongezeka endapo wananchi watakuwa na uelewa mkubwa kuhusiana na chanjo hiyo ukizingatia kundi la wazee watu, wenye ulemavu na wanawake wanapata changamoto kufika katika vituo vya afya wakati mwingine taarifa huwafikia kwa  shida", alisema Daud.


Mwezeshaji  huyo ameishukuru serikali kwa jitihada za kupambana na janga la UVIKO 19 kwa kuweka mikakati ya kuwawakinga wananchi wake katika kipindi chote licha ya uwepo wa dhana potofu juu ya kinga hiyo ambapo kupitia elimu hiyo makundi hayo yameweka utayari wa kuhitaji huduma hiyo papo hapo.


Naye afisa miradi kutoka shirika kutoka shirika la kwa wazee Edmund Revelian amesema wanafanya shughuli za utekelezaji wa mradi wa UVIKO 19 katika wilaya 2 za mkoa huo ambazo ni Muleba na Halmashauri ya wilaya ya Bukoba huku matarajio yao yakiwa ni kuifikia jamii nzima.


"Lilipokuja suala la chanjo kila mmoja alitafsiri yake sisi kama wadau tunaofanya kazi kwa wazee kwa kushirikiana na halmashauri mbili tunatumia wataalam,maafisa chanjo wa maeneo husika ili kuwawezesha kupeleke elimu sahihi katika jamii"alisema Revelian.


Amewapongeza wazee kwa namna walivyoweza kushiriki katika kuchanja kwa baadhi ya awamu zilizopita na kipindi hiki cha awamu ya mwisho walivyoonesha utayari  baada ya kupata elimu hiyo.


Kwa upande wake muhudumu wa afya ngazi ya jamii katika kata ya Mikoni Eugenius Laulian amesema ni muda sasa kwa wazee kupitia mabaraza yao kuchanja huku akiahidi kuendelea kutoa elimu kwa wale ambao hawajapata chanjo hiyo huku akiwaomba viongozi wa serikali ya kijiji kutoa ushirikiano ili kila mwananchi afikiwe huduma hiyo bila usumbufu.

Pichani:Sehemu ya wazee waliopata mafunzo hayo kutoka kata ya mikoni mkoani Kagera wakimsikiliza mwezesha wa mafunzo hayo.


Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo  baadhi ya mzee hao wakiwemo Alfred Rubagumya, Robert Kambibi, Agnes Christopher na Maria Fabian mwenye umri wa miaka 75 wameishuku  Help Age international Tanzania kwa uwezeshaji uliosaidia kuwafikishia elimu hiyo kupitia maafisa hao.


 Aidha kundi hilo baada ya kupata elimu hiyo wameahidi kuwa balozi wazuri huku wakieleza kuwa tangu wapate chanjo hiyo hakuna aliyepata madhara yoyote kiafya.


Mradi huo unatarajia kuzitembelea kata za Bujugo, Mugajwale, Nyakato, Kaibanja Buendangabo ambapo unatarajiwa  kumalizika mnamo mwezi April mwaka 2023.

No comments:

Post a Comment

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...