mwambelablog

Friday, 9 December 2022

MAVUNDE AWATAKA WAJASIRIAMALI WADOGO KUWA WANYENYEKEVU KWENYE SHUGHULI ZAO.

 

      Na ELIZABERTH PAULO DODOMA

Naibu waziri kilimo ambaye ni mbunge wa jimbo la Dodoma mjini amewaasa wajasirimali wadogo wadogo kujifunza Unyenyekevu pindi wanapokua katika shughuli zao. 

Mavunde amesema Hayo leo katika ziara aliyoifanya pamoja na wajasirimali (Mama Lishe ) mkoani Dodoma walipotembelea katika mashamba ya Waziri Mkuu Mstaafu Peter Pinda na kuishukuru familia hiyo kwa Ukarimu wao wa Kutenga muda na kuwapokea.

Ziara hiyo ni katika Kuisherehekea siku maalumu ya kuadhimisha Miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika na sherehe hizo zinafanyika bila kuwepo Kwa shamrashamra zozote kama ilivyo zoeleka na badala yake Mavunde ameitumia siku hii kwa kusaidia kuongezea mama lishe ujuzi katika ujasiria Mali wao.

"Lipo jambo la kujifunza kwa sisi viongozi na kwenu nyie mliofika hapa leo hii tujifunze Unyenyekevu jamani Ukiagalia mzee Pinda kwanafasi alizozishika Ameshawahi kuwa kiongozi mkubwa lakini leo Amekubali nimekuja na mama lishe


na akakubali kututembeza shamba lote kwahiyo hapa ndipo tunajifunza Unyenyekevu.


"Ukiwa kiongozi ukiona watu hawaji kwako hata kuuliza maji ujue unashida kwani kiongozi maana yake ni kupokea watu hivyo mzee Pinda na familia yake wana mioyo ya kipekee na ukarimu mkubwa sana ni wazi kuwa katika hali ya kawaida sisi Wenyewe tu ambaye unaweza kuwa na Ukarimu mkubwa wa kiasi cha familia ya Mzee Pinda ni ukarimu mkubwa sana na ni upendo mkubwa sana". Alisema Mavunde

Aidha Mavunde ametumia ziara Hiyo kutangaza January kufanyika kongamano kubwa la siku ya MWANAMKE DODOMA JIJI ili kutathimi makubaliano ya mwaka mzima Yalipofikia.

" Mimi nimejiitolea kulilea hili kundi ili nione mafanikio Yao kila mmoja kwa nafasi yake nataka nione wanapiga hatua kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine, Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Rais Samia imefanya kazi kubwa ya Kuendeza Dodoma inakua makao makuu Fursa zipo nyingi nataka nione akina mama wa Dodoma wakichangamkia hizi fursa" 

 "Siyafanyi haya ili mnichague kuwa mbunge wenu,Sifanyi siasa nafanya haya kwasababu niliomba dhamana ya kuwa kiongozi Nina wajibu wa kuwasaidia watu wangu".Alisema 

Akizungumza na umati huo Waziri mkuu Mstaafu Kayanza Peter Pinda Amewasihi kushirikiana kuifanya Dodoma kuwa ya Kijani kwani kila mtu mmoja akipanda mti Dodoma itakua na mwonekano mzuri hiyo hudhihirishwa baada ya mvua kunyesha Dodoma inakua na muonekano mzuri hivyo kila mtu alichukue Hilo.

" Niseme tu Tushirikiane katika kupanda miti ili tuifanye Dodoma yetu ipendeze kwani mji ukiwa na kijani kingi ni mji unaovutia sana na kitu kingine mimi huwa napenda kusema mjasiri wa mali na siyo mjasiriamali kwani ukishakua mjasiri wa mali utakua mbali kimaendeleo".

"Anthony naomba niwepo kwenye Hilo kongamano lako unalotaka lifanyike January ili niweze kuhamasisha washiri Hao kupanda miti ." Alisema Pinda

Nao baadhi ya wajasirimali waliozungumza kwa nyakati tofauti wametoa shukrani zao kwa Mavunde kwani hakuna mbunge aliyeifanya tukio kama alichofanya yeye kwa kuwakutanisha na kuwapeleka katika mashamba ya mzee Pinda kwani wamejifunza vitu vingi na kuahidi kwenda kufanyia kazi.

No comments:

Post a Comment

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...