Pichani: Mkurugenzi wa shirika la (FAHODE) Shakira Omary Akizungumza katika Hafla ya miaka mitano tokea Imeanzishwa Taasisi hiyo.
Na Lydia Lugakila, Kagera
Shirika lisilo la kiserikali la Faraja for hope and Development Organization (FAHODE) linaloihudumia jamii kupitia miradi ya maendeleo katika manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera limeadhimisha miaka mitano huku likijivunia namna lilivyofanikiwa kuijengea uwezo jamii.
Akizungumza katika Hafla ya miaka mitano mkurugenzi wa shirika hilo Shakira Omary amesema kuwa wanapoadhimisha miaka mitano wanajivunia kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa thamani ya ujana uliosaidia kutoa elimu ya kujitambua na kuepuka mimba za utotoni kwa vijana walioko mashuleni kwa shule za sekondari Kashai, Bilele, Hamgembe Nshambya na Mugeza
Ameitaja baadhi ya imiradi mingine waliyoitekeleza kuwa ni Nishike mkono, uliwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapatia vifaa vya shule, ufuatiliaji wa uwajibikaji wa jamii, pamoja na miradi mingine.
Shakira amesema kuwa dira ya shirika hilo kuona jamii iliyoelimika na iliyojikomboa dhidi ya umaskini na kuimalisha ustawi wa maendeleo.
Aidha amezitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na ukosefu wa raslimali fedha kwa ajili ya kuendesha miradi isiyo na wafadhili, ukosefu wa watumishi huku mikakati yao ikiwa ni kufungua SACCOS ambayo lengo lake ni kuwaelimisha wanawake na vijana kujua umuhimu wa kuweka akiba na kukopa ili faida itakayopatikana isaidie katika shughuli za shirika.
Kwa upande mgeni rasmi katika sherehe hizo Erasto Medard afisa tarafa Katerero amelishukuru shirika hilo kwa namna lilivyopambana katika kutekeleza miradi hiyo na kuziomba taasisi na mashirika kutoa ushirikiano ili kulifanya shirika hilo linatimiza vyema malengo yake.
Hata hivyo Mwenyekiti wa shirika hilo Antidius Augustine amesema hadi sasa shirika hilo limeacha alama katika jamii kwani wameguswa maisha ya watu.
No comments:
Post a Comment