mwambelablog

Saturday, 3 December 2022

PROF. SHEMDOE AWATAKA WAHITIMU KUTUMIA FURSA ZA KIUCHUMI

 

Pichani: Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe akizungumza na wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha.
Pichani: Wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha.


Na Mwandishi wetu Kibaha


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe amewataka wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (KFDC) kutumia fursa zilizopo kujiajiri ili kuongeza kipato na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja, jamii na Taifa kwa ujumla.


Hayo ameyasema tarehe 02/12/2022 kwenye sherehe za mahafali ya 50 ya KFDC zilizofanyika katika Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, Mkoani Pwani.


“Ndugu wahitimu, leo hii mnahitimu mafunzo yenu ya miaka miwili hapa chuoni pia wapo wale wanaohitimu mafunzo ya miezi mitatu yaliyotolewa kwa njia ya masafa ambayo yamewanufaisha wananchi wengi, nilipopita kwenye maonesho ya fani nimeshuhudia jinsi vijana mlivyoiva kiufundi katika fani mbalimbali. 


Nawapongeza sana kwa kupata ujuzi katika fani hizo natarajia kuwa ujuzi mliopata chuoni hapa mtautumia popote mtakapo pata ajira au mtakapokuwa mmejiajiri.


Prof. Shemdoe amewaeleza wahitimu kuwa ujuzi walioupata ukawasaidie kupiga hatua zaidi kimaisha na kuwataka  kujiunga kwenye vikundi ili kuweza kupata fedha za mitaji kupitia mikopo ya asilimia kumi ya mapato kwenye kila Halmashauri ambazo hazina riba yoyote. 


"waliopata ujuzi wa ufundi uwashi muende kuomba kazi za miradi katika Halmashauri zetu kwa kuwa mna ujuzi na vyeti huko kuna miradi mingi ya ujenzi” amesema Prof. Shemdoe.


Awali akitoa taarifa ya KFDC  Mkuu wa Chuo hicho Bw. Joseph Nchimbi ameeleza kuwa chuo hicho kinatoa mafunzo ya fani za ujuzi wa aina mbalimbali pia alieleza jumla ya wanachuo 383 wa kozi ndefu wakiwemo 235 mwaka wa kwanza na 170 mwaka wa pili.


“Chuo kimefanikiwa kuanzisha kozi fupi zaidi ya kumi ambazo zinatolewa kwa njia ya kiswahili na kuwafikia idadi kubwa ya wanufaika kwa wakati mmoja,” alisema Bw. Nchimbi.


Bw. Nchimbi amefafanua mafanikio ya chuo kwa  kutoa mafunzo ya nadharia na vitendo kwa wanafunzi wa muda mrefu na muda mfupi na kufanya vizuri katika mitihani yao ya VETA na wahitimu  kupata ajira katika taasisi mbalimbali na kujiajiri pia.


“Fani zinazotolewa na KFDC ni ufundi bomba, ufundi wa umeme majumbani, ufundi wa magari, ufundi wa uungaji na uundaji vyuma,  ufundi wa uwashi, ufundi wa useremala, ufundi wa ushonaji nguo na ubunifu wa mavazi, kilimo cha bustani na mazao mbalimbali, ufugaji, hotelia na udereva,” alisema Bw. Nchimbi.

No comments:

Post a Comment

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...