mwambelablog

Tuesday, 6 December 2022

DPP SYLVESTER MWAKITALU ATAKA HAKI JINAI ISIMAMIWE IPASAVYO KWA MAHABUSU NA WAFUNGWA NCHINI

 

Pichani: Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini DPP Sylvester Mwakitalu Akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi Mbalimbali waliotembelea Gereza kuu la Isanga Dodoma.

DODOMA.

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Mwakitalu ametembelea Gereza Kuu la Isanga jijini Dodoma kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili Maafisa wa Magereza katika kuwatunza wafungwa pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili mahabusu.

Akizungumza  baada ya kutembelea Gereza Kuu la Isanga Mkurugenzi  wa Mashtaka amesema kuwa lengo la  kutembelea wafungwa na mahabusu ni kuona Haki Jinai inasimamiwa ipasavyo kwa misingi ya sheria na kanuni zake.

'’kufanya haya yote ni kuona haki jinai inasimamiwa ipasavyo lakini tukipata hizi changamoto na kuzisikiliza tunaenda kuzifanyia kazi na kuzishughulikia. Changamoto tulizozipokea ambazo hazipo chini ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka tunazichukua na kuzipeleka ofisi ambazo zinahusika lengo ikiwa ni kuona Haki Jinai inasimamiwa ipasavyo.Amesema DPP Mwakitalu



Hata hivyo,Mwakitalu amezitaja changamoto ambazo  amezipokea katika ziara yake ambapo mahabusu wamezieleza ikiwa ni sula zima la ucheleweshwaji wa kesi na kuchelewa kwa upelelezi ambapo ameeleza kuwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeendelea kuzishughulikia changamoto hizo kwa kuhakikisha kuwa wameshasajili Hati za Mashtaka Mahakama Kuu ambazo hivi sasa zipo katika mchakato wa kusikilizwa.

'’Mahabusu wengi ambao nimewasikiliza  wamesema kesi zao zimechelewa upelelezi ,lakini hali halisi ni kwamba kesi zao hazijachelewa upelelezi kwa kuwa tayari zimekamilika na kinachosubiriwa ni  utaratibu wa kisheria ambao utawezesha kesi hizo kusikilizwa na Mahakama Kuu Amesema DPP Mwakitalu.



Ofisi ya Taifa ya Mashtaka nchini imeanza mwendelezo wa ziara zake katika Magereza mbalimbali nchini kwa lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili Maafisa wa Magereza, wafungwa pamoja na mahabusu ili kuhakikisha Haki Jinai inasimamiwa ipasavyo kwa mujibu wa Ibara ya 59B ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.



No comments:

Post a Comment

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...