Pichani: Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi mhe, Godfrey Kasekenya akiwa ziarani mkoani kagera kukagua mradi wa Ujenzi wa nyumba ya Jaji unaosimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania
Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi mhe, Godfrey Kasekenya ameagiza wakala wa majengo Tanzania (TBA) Mkoa wa Kagera kukamilisha nyumba ya jaji wa mahakama mkoani Kagera kwa wakati ndani ya miezi 6 ikiwa ni pamoja na kuzingatia ubora kwa kuwasimamia wanaojenga nyumba hiyo.
Agizo la naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi limekuja baada ya kufanya ziara ya kukagua mradi wa Ujenzi wa nyumba hiyo unaosimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na kujionea shughuli mbalimbali zinavyoendelea.
Mh, Kasekenya amesema kua hivi karibuni wizara ya ujenzi na uchukuzi ilitoa kiasi cha shilingi milioni 360 katika mradi huo na kuwa mradi umefikia asilimia 13 hivyo anategemea kuona ndani ya miezi 6 unakamilika.
"Naomba muisimamie ahadi hiyo muitekeleze na naomba hilo lifanyike zingatieni ubora,wasimamie wanaojenga kamilisha kazi hiyo kwa wakati sababu nyumba hii inahitajika sana ili ianze kutumika alisema Kasekenya."
Aidha amewapongeza Wakala wa Majengo Tanzania kwa hatua waliyofikia katika ujenzi huo na kuongeza kuwa mradi huo utakuwa mkombozi kwa watumishi.
Kwa upande wake kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania TBA mkoa wa Kagera Adam Malimi amesema nyumba hiyo itakuwa ya ghorofa moja lenye vyumba vinne vya kulala, sebule, chumba cha kusomea, sehemu ya kulia chakula, maliwato na vibaraza na vyumba na vyumba vya vya wasaidizi.
Malimi Ameongeza kuwa hadi sasa wanaenda awamu ya pili ya mradi huo ambapo awamu ya kwanza ilianza tarehe 1 mwezi machi, 2022 hadi June 30,2022 buku awamu ya pili ikianza desemba 10 mwaka huu na utakamilika juni 12, 2023.
Hata hivyo amesema kuwa licha ya mradi huo kukabiliwa na changamoto ya upandaji bei wa vifaa vya ujenzi pamoja na mvua watahakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili ikamilike kwa muda uliopangwa.
miradi aliyoitembelea ni pamoja na daraja la kitengule wilayani Misenyi, mradi wa barabara wa Bugene - Burigi wilaya Karagwe Nyakasimbi
No comments:
Post a Comment