mwambelablog

Saturday, 3 December 2022

PROF.MDOE ATOA SIRI YA KISWAHILI KUPAA KIMATAIFA

Pichani: Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu  Prof.James Mdoe akikabidhiwa kitabu na Bi.Menna Yasser Jana Disemba 3,2022 kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari bikini Dodoma.

 Kutoka Dodoma 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia,ipo katika hatua za kuimarisha nguvu ya kueneza matumizi ya Lugha ya Kiswahili kupitia mafunzo yatakayo ongeza hamasa kwa lugha ya Kiswahili zaidi ya inavyotumika kwa sasa.


Hayo yameelezwa  na  Prof.James Mdoe wakati wa hafla fupi ya kuzindua Sherehe za maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru yanayokwenda sambamba na Matumizi ya Kiswahili ,Disemba 3,2022,Jijini Dodoma.

Aidha Prof.Mdoe amesema kuwa ,Kuelekea maadhimisho hayo yanayofanyika Disemba 9 2022 ,Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatarajia kupandisha Bango la Kiswahili katika Mlima Kilimanjaro lengo likiwa ni kueneza lugha hiyo Kwa mataifa mengi zaidi Duniani.

"Lengo la kufanya hivyo ni kusherehekea Uhuru wa Nchi yetu kwa kutangaza Lugha yetu Kwa mataifa mengine ndio maana bango hili litapandishwa na kusimikwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kama ambavyo ulisimikwa Mwenge wa uhuru,"


Prof.Mdoe ameongeza kuwa kwa sasa watumiaji wa Lugha ya Kiswahili Duniani wanakadiriwa kuwa takribani milioni 250 na lengo ni kuhakikisha ifikapo mwakani wakati wa maadhimisho hayo idadi ya watu wanaotumia Lugha ya kiswahili iwe imeongezeka

Ameongeza kuwa "Wameandaliwa vijana wawili shupavu ambao watakwenda kusimika Bango lenye kauli mbiu "Kiswahili Kileleni" kwenye kilele Cha mlima Kilimanjaro siku ya maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania,"Amesema Prof.Mdoe




Vilevile Prof.Mdoe amesema kuwa mpaka sasa kuna vyuo zaidi ya 150 duniani zinazofundisha Lugha ya kiswahili na vituo 300 vya Radio na Runinga Duniani vyenye vipindi vya Lugha ya Kiswahili.

Prof.Mdoe ametumia muda huo kutoa wito kwa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika Mataifa mbalimbali kuendelea kuchochoe matumizi ya Lugha ya kiswahili katika mataifa hayo ikiwemo kufungua madarasa ya awali ya kufundisha Lugha ya kiswahili.

"Nchini Malawi tumefungua tayari Darasa la kufundisha Lugha ya kiswahili na imewezekana kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini humo ndio maana natoa wito kwa Mabalozi wengine kufany hivyo ili kuendelea kukuza lugha yetu kimataifa,"Ameeleza Prof.Mdoe

Kwa Muktadha huo Bi.Menna Yasser ambaye ni Raia ya Misri na Mwandishi wa kitabu cha kwanza kilichoandikwa kwa lugha ya kiswahili nchini humo amesema kuwa matumizi ya lugha ya kiswahili inazidi kukuwa kwani kuna baadhi ya Nchi kwa sasa zimeendelea kukitambua kiswahili kama lugha ya kutumiwa katika mataifa yao.

Amesema kuwa Lugha ya Kiswahi inazidi kukuwa kwa kasi kwani kwa sasa kuna baadhi ya vyuo nchini Misri zinafundisha Kiswahili na mataifa kama Uganda,Sudan Kusini na mataifa mengine ya Ukanda wa mashariki na kusini Mwa Afrika zinatumia kiswahili kama lugha mojawapo ya mawasiliano.

"Kiswahili lazima kifike Kileleni kwa sababu nia ipo na naona Wizara imejidhatiti kuhakikisha kiswahili kinaendelea kuvuka mipaka zaidi,"Amesema Bi.Menna

No comments:

Post a Comment

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...