Na Lydia Lugakila
Bukoba
Jumla ya unit 25 za damu zimepatikana kupitia kongamano la Kibeta women Galla lililolenga kuwajengea uwezo wanawake kujitegemea kiuchumi.
Akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika katika kata ya Kibeta Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, mratibu wa damu salama mkoa Boniphace Meza amesema kuwa kongamano hilo limesaidia kwa kiasi kikubwa kuwakutanisha wanawake walioamua kuchangia unit 25 za damu.
"Ninamshukuru diwani wa kata ya Kibeta kupitia kongamano hili lilowezesha upatikanaji wa damu, uchangiaji huu ni muhimu sana kwa wenye uhitaji niwapongeze wananchi wa Kagera kutokana na kuwa na muitikio mzuri katika uchangiaji wa damu kwa sasa sina upungufu wa damu katika katika kapu langu alisema Meza."
Aidha amewapongeze pia wanafunzi wa shule ya sekondari Ihungo ambayo imekuwa ikichangia pakubwa kupatikana kwa wastani wa chupa za damu 150 hadi 200.
Nao baadhi ya wachangiaji wa damu hiyo akiwemo bi Oliva Godwin na Judika Kalumna wamesema kuwa wameamua kuchangia damu hiyo kutokana na wanawake kupata matatizo ya upungufu wa damu wakati wa kujifungua.
Aidha kwa upande wake diwani wa kata ya Kibeta Anastella Alphonce ambaye ni muandaaji wa kongamano hilo amesema kuwa wamelenga kuwajengea uwezo wanawake hao kuondokana na utegemezi kiuchumi huku akiwahimiza kujenga utamaduni wa kuchangia damu salama ili kuokoa maisha ya watu wenye huhitaji
Bi Anastella amesema kuwa kongamano hilo litakuwa endelevu kila mwaka ili kuwakumbusha wanawake kuwajibika vyema katika nafasi zao sambamba na uchangiaji wa damu salama.
Naye katibu wa wamachinga manispaa ya Bukoba Eliana Elias mmoja kati ya waandaaji wa kongamano la Kibeta Women Galla amesema kuwa wanawake wamenufaika na elimu ya ujasiriamali na kuwa lengo lao ni kumuunga mkono Rais Dokta Samia mbapo KAULI MBIU NI "MWANAMKE INUKA SONGA MBELE MWINUE NA MWENZAKO.
No comments:
Post a Comment