Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Kaimu Mkeyenge akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma.
Na Deborah Lemmubi - Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Kaimu Mkeyenge amebainisha kuwa Shirika linatekeleza miongozo inayotolewa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) katika kuhakikisha manunuzi, matumizi bora, sahihi na salama ya vifaa na mifumo yote ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Serikalini yanazingatiwa.
Bwana Mkeyenge amebainisha hayo leo Machi 7,2023 Jijini Dodoma, wakati akitoa taarifa kwa Umma juu ya utekelezaji wa majukumu ya TASAC, pamoja na kubainisha Mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha Mkeyenge amesema kuwa TASAC imeunganisha ofisi zake zote zikiwemo zile za Mikoa, Wilaya na mipakani kwenye Mkongo wa Taifa ambao umerahisisha na kuharakisha mawasiliano ya ndani (Intranet), barua pepe, na mawasiliano na wadau wa nje .
Na kuongeza kuwa uendelezaji wa miundombinu na mifumo ya TEHAMA ulianza mwaka wa fedha 2018/19 na utakamilika mwaka wa fedha 2025/26 huku mifumo ambayo inayoboreshwa ndani ya Shirika ni pamoja na mfumo wa ukaguzi, usajili wa vyombo vya usafiri kwa njia ya maji na utoaji wa vyeti vya Mabaharia (Maritime Administration Management System), mfumo wa utoaji leseni, ukusanyaji wa mapato ya udhibiti, uhakiki kadhia na kutoa ankara za malipo ya watoa huduma wa meli (Manifest Billing System), pamoja na mfumo wa kutoa huduma za biashara ya Meli.
"Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) imetusaidia sana katika kuhakikisha manunuzi, matumizi bora, sahihi na salama ya vifaa na mifumo yote ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Serikalini tunaitumia kwa mafanikio makubwa na tunaami mpaka mwaka wa fedha wa 2025/26 mifumo yote ndani ya Shirika itakuwa tayari,"
Na kuongeza "mifumo ya TEHAMA ulianza mwaka wa fedha 2018/19 na utakamilika mwaka wa fedha 2025/26 huku mifumo ambayo inayoboreshwa ndani ya Shirika ni pamoja na mfumo wa ukaguzi, usajili wa vyombo vya usafiri kwa njia ya maji na utoaji wa vyeti vya Mabaharia (Maritime Administration Management System), mfumo wa utoaji leseni, ukusanyaji wa mapato ya udhibiti, uhakiki kadhia na kutoa ankara za malipo ya watoa huduma wa meli (Manifest Billing System), pamoja na mfumo wa kutoa huduma za biashara ya Meli".
Pia Mkeyenge amesema katika kuimarisha usimamizi wa usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira dhidi ya shughuli za meli na kupunguza matukio ya ajali za vyombo vya majini TASAC imefanya sensa na kaguzi za vyombo vya usafiri majini ambapo kaguzi 6,208 katika mwaka wa fedha 2021/22 zilifanyika na kaguzi 4,490 zilfanyika katika kipindi cha Julai 2022 mpaka Januari 2023 inayotarajiwa kufikia vyombo takriban 8,000 ifikapo mwezi Juni 2023.
"Tumefanya kaguzi za vyombo vya usafiri majini ambapo kaguzi 6,208 katika mwaka wa fedha 2021/22 na kaguzi 4,490 katika kipindi cha Julai 2022 mpaka Januari 2023 inayotarajiwa kufikia vyombo takriban 8,000 ifikapo mwezi Juni 2023".
Katika hatua nyingine amesema shirika hilo limefanikiwa Kuboresha ufanisi wa bandari kwa kupunguza uwezo wa shehena inayoruhusiwa kukaa bandarini kwa wakati mmoja (yard density) kutoka asilimia 65 hadi asilimia 50 kwa kuweka Amri ya Tozo ya Bandari Kavu ambapo wamefungua ofisi 11 za Shirika katika maeneo mbalimbali ili kusogeza huduma karibu na wananchi Shirika lina ofisi katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara, Tanga, Mwanza, Kagera, Mara, Kigoma, Rukwa, Ukerewe pamoja na Geita.
"Kuboresha ufanisi wa bandari kwa kupunguza uwezo wa shehena inayoruhusiwa kukaa bandarini kwa wakati mmoja (yard density) kutoka asilimia 65 hadi asilimia 50 kwa kuweka Amri ya Tozo ya Bandari Kavu ambapo wamefungua ofisi 11 za Shirika katika maeneo mbalimbali ili kusogeza huduma karibu na wananchi Shirika lina ofisi katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara, Tanga, Mwanza, Kagera, Mara, Kigoma, Rukwa, Ukerewe pamoja na Geita".
Hata hivyo TASAC imefanikiwa kukagua meli za kigeni 36 kwa kipindi kuanzia Julai 2022 hadi Disemba 2022, na kuanzia Januari 2023 tumekagua meli za kigeni 37 ambapo shirika linategemea kukagua meli 61 hadi kufikia juni 2023.
TASAC ilianzishwa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415 na kuanza rasmi kutekeleza majukumu yake tarehe 23 Februari, 2018. Kuundwa kwa TASAC ni hatua ya kisera ya Serikali, kwa upande wa Tanzania Bara, inayokusudia kukuza sekta za usafiri majini, kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma hususan kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa kuinua mchango wa usafiri kwa njia ya maji. Hii ni kwa sababu Tanzania ina ukanda mkubwa wa Bahari ya Hindi wenye urefu takriban Kilomita 1,424, Maziwa makubwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa
No comments:
Post a Comment