mwambelablog

Saturday, 11 March 2023

TASAC YATOLEA UFAFANUZI JUU YA UZUSHI WA VIJANA 209 WALIOFUTIWA MKATABA WA MAFUNZO KWA VITENDO KAZINI.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bwana Kaimu Mkeyenge akitolea ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Kwenye ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma Machi 10,2023.


Na Deborah Lemmubi - Dodoma.



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bwana Kaimu Mkeyenge ametolea ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii hususan Twitter na Instagram kuhusu malalamiko dhidi ya Shirika hilo yanayosema kuwa Mikataba ya mafunzo kwa vitendo kwa vijana zaidi ya 400 waliokuwa TASAC ilivunjwa bila kufuata utaratibu na ikiwa imebaki muda wa mwaka mmoja kuisha kwa mikataba hiyo.



Mkeyenge ametoa ufafanuzi huo Jijini Dodoma Machi 10/2023 wakati akitoa taarifa kwa Umma kupitia waandishi wa habari kuhusu Vijana hao waliokuwa wanafanya shughuli za Mafunzo ya kazi ndani ya shirika hilo.



Bwn Mkeyenge amesema kuwa tuhuma walizotoa Vijana hao ni kuwa wanafanya kazi bila bima ya afya na kwamba TASAC ilitoa rushwa kwa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) katika mashauri ya kazi yaliyofunguliwa na vijana hao ili haki isitendeke.


''Hakuna sheria inayomtaka muajiri yeyote yule kumkatia bima ya afya kijana anayefanya shughuli za Mafunzo kazini suala hilo halipo na hakuna taasisi yeyote inayoweza kufanya hivyo kwani stahiki zao zimeainishwa kwenye Muongozo wa Kitaifa wa Mafunzo Kazi uliotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu na tuhuma kuhusu TASAC kutoa rushwa kwa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ili mashauri ya kazi yaliyofunguliwa na vijana hao haki isitendeke hakuna ukweli wowote''.


Pia Bwn Mkeyenge ameongeza kuwa kati ya vijana 209 waliofutiwa mikataba yao, ni vijana 41 tu ambao hawakuridhika na maamuzi hayo ambapo vijana 32 kati ya vijana 41, shauri lao lilifutwa na CMA kwa kuwa liliwasilishwa nje ya muda, hivyo ni vijana 9 tu ambao shauri lao dhidi ya TASAC lilipokelewa na lipo katika Tume ya Usuluhisi na Uamuzi.


Ambapo vijana 168 waliobaki hawakupinga uamuzi wa TASAC wa kuvunja mikataba yao kutokana na mabadiliko ya Sheria ambayo yalikuwa ni nje ya uwezo wa Shirika.


Mkurugenzi huyo amesema suala hilo lipo kwenye chombo cha maamuzi kisheria, TASAC haipaswi kuzungumzia shauri hilo ila waliona ni busara kulitolea ufafanuzi wa kilichofanyika kwa upande wa TASAC na kuacha hatua za maamuzi zinazoendelea kuchukua mkondo wake.


TASAC ni Shirika la Umma linalotekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo inayotolewa na Serikali, hivyo linatoa wito kwa Umma kuwa na subira wakati Tume inapoyafanyia kazi mashauri hayo.



Katika hatua nyingine amesema TASAC ni taasisi ya Serikali inayosimamiwa na Sheria, Kanuni na Miongozo ya Serikali, hivyo basi mashauri yake kisheria yanasimamiwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ikiwa ni pamoja na shauri hili hivyo kwa mantiki hiyo, Shirika hilo halijatoa na haiwezi kutoa rushwa yoyote kwa CMA ili kuzuia haki isitendeke kama ilivyoripotiwa katika mitandao ya kijamii.


''Kwa mantiki hiyo, niwahakikishie kuwa TASAC haijatoa na haiwezi kutoa rushwa yoyote kwa CMA ili kuzuia haki isitendeke kama ilivyoripotiwa katika mitandao ya kijamii'' amesema Bwana Mkeyenge



Hata hivyo Mkeyenge amehitimisha kwa kusema kati ya vijana 209 waliofutiwa mikataba yao, ni vijana 41 tu ambao hawakuridhika na maamuzi hayo Vijana 32 kati ya vijana 41, shauri lao lilifutwa na CMA kwa kuwa liliwasilishwa nje ya muda, hivyo ni vijana 9 tu ambao shauri lao dhidi ya TASAC lilipokelewa na lipo katika Tume ya Usuluhisi na Uamuzi.

Thursday, 9 March 2023

NAFASI KUJIUNGA JWTZ ZATANGAZWA NA TAHADHALI KUTOLEWA KWA WANANCHI JUU YA MAPATELI KATIKA KIPINDI HIKI

 

kaimu mkurugenzi wa Habari na uhusiao wa JWTZ, Luteni Kanali GAUDENTIUS ILONDA akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma Leo Machi, 9,2023



Na Deborah Lemmubi - Dodoma.


Jeshi la Wananchi la Tanzania kupitia Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano JWTZ Luteni Kanali Gaudentius Ilonda limetangaza nafasi za kujiunga na Jeshi kwa vijana wa kitanzania wenye elimu ya kuanzia kidato cha nne mpaka kidato cha sita na wale wa shahada ya uzamili ambao wamemaliza mkataba wa miaka miwili wa mafunzo ya kujitolea katika Jeshi la kujenga Taifa (JKT) na kurudishwa majumbani.


Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa Habari leo Machi 9,2023 Jijini Dodoma  Luteni Kanali Gaudentius Ilonda , amesema nafasi hizo zinawahusu vijana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 26 kwa wenye elimu ya kidato cha 4 na cha sita na umri usiozidi miaka 27 kwa wenye elimu ya juu.


"Nafasi hizi haziwahusu vijana ambao bado wapo katika kambi mbalimbali za JKT kwa sasa bali zinawahusu wale ambao tayari wamemaliza mikataba yao ya mafunzo ya miaka miwili na kurudishwa majumbani na wenye vigezo vilivyotajwa vya kuomba nafasi hii".


Sambamba na hilo pia Luteni Kanali Ilonda, ameeleza vigezo vitakavyozingatiwa wakati wa kutuma maombi hayo kuwa ni pamoja na  mwombaji kuwa raia wa Tanzania wa kuzaliwa mwenye kitambulisho cha Taifa,awe na afya nzuri na akili timamu,awe na cheti halisi cha kuzaliwa,vyeti vya shule na vyeti vya taaluma yake.


Vigezo vingine ni pamojana na mwombaji awe hajatumikia Jeshi la Polisi,magereza,Chuo cha Mafunzo au Kikosi maalumu cha kuzuia magendo na asiwe ameoa au kuolewa.


Kwa upande wa utaratibu wa jinsi ya kutuma maombi Luteni Kanali Ilonda ,amebainisha kuwa maombi yote yaandikwe kwa mkono na yawasilishwe makao makuu ya jeshi hilo Dodoma kwanzia leo tarehe 9,Machi hadi tarehe 20 ,Machi 2023 yakiwa na viambatanisho kama vile nakala ya kitambulisho cha taifa au namba ya nida,nakala ya cheti cha kuzaliwa,vyeti vya shule na chuo,nakala cheti cha JKT na namba ya simu ya mkononi ya muombaji na maombi yanaweza kutumwa Kupitia njia ya barua pepe ulinzimagazine@tpdf.mil.tz


Katika yote Luteni Kanali Ilonda amewakumbusha  wananchi kuwa makini na matapeli kwani kumekuwa na tabia ya kuibuka matapeli pindi matangazo hayo ya nafasi ya kujiunga na jeshi hili zinapotangazwa


"Natambua katika matangazo haya ya kujiunga na nafasi hizi kuna matapeli watajitokeza na kuanza kupenyeza utapeli wao ,hivyo watanzania wasidanganyike wala kurubuniwa na hakuna njia ya mkato katika kupata nafasi hizi zaidi ya kuzingatia vigezo vilicyowekwa wazi kabisa,


"Matapeli ni Binadamu hivyo kutokana na kukua kwa teknolojia kila siku wanabuni mbinu mpya hivyo inabidi kuchukua tahadhari kwa pamoja ili kuepukana na mitego ya utapeli wao".

KANISA LA EAGT LAMKABITHI GARI ASKOFU MKUU MWAKIPESILE

 Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dkt. Brown Abel Mwakipesile wakati wa Hafla ya kukabidhiwa gari ya Utumishi na kanisa hilo Jijini Dodoma


Kutoka Dodoma.

Katika kuazimisha siku ya Wanawake Duniani Kanisa la (EAGT) Dodoma limewataka wakina mama kutambua ratiba ,hasa katika majukumu ya kulea na kutunza watoto pamoja na waume zao kwa sababu mwanamke ndio wenye uchungu zaidi hivyo wanapaswa kuwa na wajibu wenye utaratibu wa kifamilia.


Hayo yamesemwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dkt. Brown Abel Mwakipesile wakati wa Hafla ya kukabidhiwa gari ya Utumishi na kanisa hilo Jijini Dodoma huku akiwaasa wanadamu kutopumbazika na utandawazi kwa sababu Misingi ya Mungu ipo wazi na inaelekeza namna Mwanadamu anapaswa kuishi kwa kufuata mienendo ya Biblia.

''Mimi nasema wanadamu wasizuzuke kwa sababu Misingi ya Mungu ipo wazi Kibiblia Mungu aliweka utaratibu wa mwanadamu anapaswa kuishije kwa sababu kinachokuwa chema kina mipaka yake na mtu kama umeumbwa na utashi wa busara unapaswa kupambanua kipi kinafaa na kipi kisichofaa kwa ajili ya manufaa yake''amesema Dkt.Mwakipesile

Aidha Dkt. Mwakipesile amesema Kanisa la EAGT wanapambana kuubiri injili watu kuacha Uovu wabaki na mawazo waliyopewa na Mungu ili wapate kumuheshimu Mungu anapowapa afya na uzima.

''mambo ya ushonga,ulawiti ni kinyume na mapenzi ya Mungu na yataleta hukumu kubwa kwa wanadamu na hii italeta laana kubwa hata katika familia na jamii watanzania waepuke kuigiza sana vitu visivyofaa''amesema Dkt.Mwakipesile.


Kwa upande wake Makamu Askofu Mkuu (EAGT) Askofu. Joshua Wawa amesema Dkt. Mwakipesile amekuwa akijitaabisha kwa kazi ya Mungu kwanzia ngazi ya chini hadi majimbo hivyo kutokana na jitihada zake na kuzitambua kwa kazi anazozifanya ikawapasa wao kama kanisa kumnunulia chombo cha usafiri.

''Amekuwa akijitaabisha kwa kazi ya Mungu kwanzia ngazi ya chini hadi majimbo na kutokana na jitihada na kuzitambua kazi anazozifanya ikatupasa sisi kumnunulia chombo cha usafiri''amesema Askofu Wawa.

Hata hivyo amehitimisha kwa kusema kanisa imefanya hayo kwa ujulisho kwa kuwa ukitenda vyema kazi ya Mungu utaenziwa kuanzia Duniani

.

Tuesday, 7 March 2023

WADAU WA MASUALA YA MAAFA WAJA NA MIKAKATI MADHUBITI YA KUDHIBITI MAAFA

 

Washiriki kikao kazi cha Jukwaa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa kujadili rasimu ya taarifa ya tathmini na mapendekezo ya mahitaji ya mfumo wa mawasiliano ya usimamizi wa maafa na kuimarisha uelewa wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi.

KUTOKA DODOMA.

SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Menejimenti ya Maafa imedhamiria kuwa na mikakati madhubuti katika kukabiliana na maafa nchini.


Akizungumza wakati wa kikao kazi cha Jukwaa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa kujadili rasimu ya taarifa ya tathmini na mapendekezo ya mahitaji ya mfumo wa mawasiliano ya usimamizi wa maafa na kuimarisha uelewa wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022 Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw. Charles Msangi alisema Idara imeendelea kuchukua hatua za kupunguza madhara kwa kuhakikisha usimamizi na uratibu wa maafa na huduma za dharura zinatolewa kwa wakati.

Afisa Sheria Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Nelson Hutty akiwasilisha mada kuhusu Sheria yaUsimamizi wa Maafa Na. 6 ya Mwaka 2022 wakati wa kikao hicho Jijini Dodoma


Kikao kazi hicho kilichoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) ilifanya Tathmini ya Mahitaji ya Mfumo wa Usimamizi wa Maafa (Disaster Management Information System Requirement mapping) ambapo rasimu ya taarifa ya tathmini ya mahitaji (Needs assessment and proposed system) ambayo inahitaji maoni ya wadau ili kuboresha Mfumo utakaopendekezwa ili kusaidia kuimarisha mawasiliano baina ya wadau wa usimamizi wa maafa.


“Mfumo huo utaboresha utaratibu wa kutoa tahadhari ya mapema kwa wadau na umma ili kuchukua hatua za haraka kwa ajili ya kuokoa maisha na mali,”alisisitiza Msangi.


Aidha, Sheria ya Usimamizi wa Maafa kifungu cha 4 imeelekeza kuweka mfumo wa teknolojia ya habari na mawasiliano utakaowaunganisha wadau wa masuala ya maafa ili kufuatilia mwenendo wa majanga na hali ya maafa kwa ajili ya kuchukua hatua za kuzuia na kukabiliana na maafa kwa wakati.

Idara ya Menejimenti ya Maafa itaendelea kuratibu na kusimamia masuala ya maafa nchini kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa ya Mwaka 2004 na Sheria ya Usimamizi wa Maafa, Na. 6 ya mwaka 2022.


Kwa upande wake Mratibu Maafa UNICEF Bi.Judith ameeleza kuwa wataendelea kuboresha mashirikiano na wadau ili kuhakikisha wanajenga uwezo kwa wadau wa maafa katika ngazi zote kuanzia Taifa hadi vijiji.

“UNICEF tupo pamoja na tunaunga mkono jitihada zote zinazofanya na Seikali hivyo tutaendelea kuwajengea uwezo wadau wote na kuwafikia waathirika wa madhara yatokana ya maafa kwa lengo la kupunguza madhara hayo, na kuendelea kuboresha mifumo ya kupashanaji wa habari wakati wa maafa,”alisema Judith


Monday, 6 March 2023

TASAC YATEKELEZA MIONGOZO INAYOTOLEWA NA MAMLAKA YA SERIKALI MTANDAO(e-GA)

 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Kaimu Mkeyenge akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma.




Na Deborah Lemmubi - Dodoma.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Kaimu Mkeyenge amebainisha kuwa Shirika linatekeleza miongozo inayotolewa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) katika kuhakikisha manunuzi, matumizi bora, sahihi na salama ya vifaa na mifumo yote ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Serikalini yanazingatiwa.


Bwana Mkeyenge amebainisha hayo leo Machi 7,2023 Jijini Dodoma, wakati akitoa taarifa kwa Umma juu ya utekelezaji wa majukumu ya TASAC, pamoja na kubainisha Mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.



Aidha Mkeyenge amesema kuwa TASAC imeunganisha ofisi zake zote zikiwemo zile za Mikoa, Wilaya na mipakani kwenye Mkongo wa Taifa ambao umerahisisha na kuharakisha mawasiliano ya ndani (Intranet), barua pepe, na mawasiliano na wadau wa nje .


Na kuongeza  kuwa uendelezaji wa miundombinu na mifumo ya TEHAMA ulianza mwaka wa fedha 2018/19 na utakamilika mwaka wa fedha 2025/26 huku mifumo ambayo inayoboreshwa ndani ya Shirika ni pamoja na mfumo wa ukaguzi, usajili wa vyombo vya usafiri kwa njia ya maji na utoaji wa vyeti vya Mabaharia (Maritime Administration Management System), mfumo wa utoaji leseni, ukusanyaji wa mapato ya udhibiti, uhakiki kadhia na kutoa ankara za malipo ya watoa huduma wa meli (Manifest Billing System), pamoja na mfumo wa kutoa huduma za biashara ya Meli.


"Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) imetusaidia sana katika kuhakikisha manunuzi, matumizi bora, sahihi na salama ya vifaa na mifumo yote ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Serikalini tunaitumia kwa mafanikio makubwa na tunaami mpaka mwaka wa fedha wa 2025/26 mifumo yote ndani ya Shirika itakuwa tayari,"

Na kuongeza  "mifumo ya TEHAMA ulianza mwaka wa fedha 2018/19 na utakamilika mwaka wa fedha 2025/26 huku mifumo ambayo inayoboreshwa ndani ya Shirika ni pamoja na mfumo wa ukaguzi, usajili wa vyombo vya usafiri kwa njia ya maji na utoaji wa vyeti vya Mabaharia (Maritime Administration Management System), mfumo wa utoaji leseni, ukusanyaji wa mapato ya udhibiti, uhakiki kadhia na kutoa ankara za malipo ya watoa huduma wa meli (Manifest Billing System), pamoja na mfumo wa kutoa huduma za biashara ya Meli".



Pia Mkeyenge amesema katika kuimarisha usimamizi wa usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira dhidi ya shughuli za meli na kupunguza matukio ya ajali za vyombo vya majini TASAC imefanya sensa na kaguzi za vyombo vya usafiri majini ambapo kaguzi 6,208 katika mwaka wa fedha 2021/22 zilifanyika na kaguzi 4,490 zilfanyika katika kipindi cha Julai 2022 mpaka Januari 2023 inayotarajiwa kufikia vyombo takriban 8,000 ifikapo mwezi Juni 2023.


"Tumefanya kaguzi za vyombo vya usafiri majini ambapo kaguzi 6,208 katika mwaka wa fedha 2021/22 na kaguzi 4,490 katika kipindi cha Julai 2022 mpaka Januari 2023 inayotarajiwa kufikia vyombo takriban 8,000 ifikapo mwezi Juni 2023".


Katika hatua nyingine amesema shirika hilo limefanikiwa Kuboresha ufanisi wa bandari kwa kupunguza uwezo wa shehena inayoruhusiwa kukaa bandarini kwa wakati mmoja (yard density) kutoka asilimia 65 hadi asilimia 50 kwa kuweka Amri ya Tozo ya Bandari Kavu ambapo wamefungua ofisi 11 za Shirika katika maeneo mbalimbali ili kusogeza huduma karibu na wananchi Shirika lina ofisi katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara, Tanga, Mwanza, Kagera, Mara, Kigoma, Rukwa, Ukerewe pamoja na Geita.


"Kuboresha ufanisi wa bandari kwa kupunguza uwezo wa shehena inayoruhusiwa kukaa bandarini kwa wakati mmoja (yard density) kutoka asilimia 65 hadi asilimia 50 kwa kuweka Amri ya Tozo ya Bandari Kavu ambapo wamefungua ofisi 11 za Shirika katika maeneo mbalimbali ili kusogeza huduma karibu na wananchi Shirika lina ofisi katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara, Tanga, Mwanza, Kagera, Mara, Kigoma, Rukwa, Ukerewe pamoja na Geita".


Hata hivyo TASAC imefanikiwa kukagua meli za kigeni 36 kwa kipindi kuanzia Julai 2022 hadi Disemba 2022, na kuanzia Januari 2023 tumekagua meli za kigeni 37 ambapo shirika linategemea kukagua meli 61 hadi kufikia juni 2023.


TASAC ilianzishwa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415 na kuanza rasmi kutekeleza majukumu yake tarehe 23 Februari, 2018. Kuundwa kwa TASAC ni hatua ya kisera ya Serikali, kwa upande wa Tanzania Bara, inayokusudia kukuza sekta za usafiri majini, kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma hususan kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa kuinua mchango wa usafiri kwa njia ya maji. Hii ni kwa sababu Tanzania ina ukanda mkubwa wa Bahari ya Hindi wenye urefu takriban Kilomita 1,424, Maziwa makubwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa

MAJADILIANO MRADI WA KUCHAKATA NA KUSINDIKA GESI ASILIA (LNG) YAKAMILIKA

 


Na Teresia Mhagama


Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba, amesema kuwa, majadiliano yanayohusu Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia  baina ya Serikali ya Tanzania na wawekezaji Kampuni ya Shell ya Uholanzi na Equinor ya Norway na washirika wao yamekamilika na kwamba sasa wataalam wapo katika kazi ya kuandika mikataba ya mradi huo.


Waziri wa Nishati ameyasema hayo tarehe 06 Machi, 2023 jijini Arusha wakati akitoa vipaumbele vya Wizara katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati ambapo pamoja na masuala mengine ya kiutumishi, Baraza hilo limepitia Mpango wa Bajeti wa Wizara ya Nishati kwa mwaka 2023/2024.



“Mazungumzo ya mradi huu wa LNG yamekamilika na wataalam kwa sasa wanaandika mikataba mikubwa miwili yenye masuala mengi ikiwemo ya kiufundi, Mkataba mmoja ni wa Nchi Hodhi (HGA) na mwingine ni mkataba uliounganishwa wa vitalu vya Gesi Asilia NambaI,II na IV ambavyo gesi yake itatumika kwenye mradi wa LNG, kila mkataba una takriban kurasa zaidi ya 600, hii si kazi ndogo ila nimewasisitiza wamalize kazi mwezi huu ili kuweza kuendelea na hatua nyingine za utekelezaji.” Amesema Makamba


 Amesema kuwa mradi huo ambao uwekezaji wake ni zaidi ya Shilingi Trilioni 70 utaleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi nchini na utaifanya Tanzania kuwa moja ya nchi zinazochangia katika usalama wa nishati duniani hivyo amewataka Watendaji wa Wizara ya Nishati kuendelea kusimamia utekelezaji wa mradi huo.



Makamba ametaja mradi mwingine unaoendelea kutekelezwa ni wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania ambapo kwa sasa shughuli mbalimbali za maandalizi ya ujenzi zinaendelea na mwezi uliopita Serikali imetoa kibali cha ujenzi wa bomba hilo kwa kampuni ya EACOP na kwa sasa inaendelea kukamilisha taratibu za kupata pesa za kutekeleza mradi huo ambazo zimefikia mwishoni.


Ameongeza kuwa, zoezi la ulipaji fidia kwa watu 9800 katika mkuza wa Bomba la mafuta zinaendelea ambapo mpaka sasa shilingi Bilioni 29.2 zimelipwa kati ya shilingi Bilioni 30 zilizokuwa zinahitajika kwenye ulipaji fidia na matarajio ni kwamba ujenzi unatarajiwa kuanza kabla ya mwisho wa mwaka huu.


Ametaja baadhi ya faida zitakazotokana na mradi huo kuwa ni pamoja na ajira 10,000, Serikali kupata mapato kupitia tozo ya kupitisha mafuta, ada mbalimbali kupitia matumizi ya Bandari ya Tanga na kampuni mbalimbali za kitanzania zitatoa huduma katika mradi huo. Pia ujenzi wa bomba unahamasisha shughuli za utafiti na uchimbaji wa mafuta kwani linapita kwenye maeneo yenye viashiria vya upatikanaji wa mafuta hivyo Tanzania ikipata mafuta tayari miundombinu ya usafirishaji mafuta hayo ipo.


Kuhusu hali ya upatikanaji umeme amesema kuwa, kazi ya kurekebisha miundiombinu na kuongeza uzalishaji umeme inaendelea kupitia miradi mbalimbali kama ya gridi imara na hivi karibuni Serikali imesaini mikataba ya takriban ya shilingi Trilioni 1.9 ya kurekebisha miundombinu ya umeme. Amesema kuwa, kazi hiyo inachukua muda hivyo amewaomba watanzania wawe na subira ili matunda ya uwekezaji kama huo yaonekane.


Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia, amesema kuwa hiyo ni ajenda ya Wizara ya Nishati kwani ni suala linalowagusa watanzania wote kuanzia mtu maskini hadi tajiri hivyo  Serikali ambayo ina jukumu la kuboresha maisha ya watanzania inalisimamia suala hilo ili nchi iingie kwenye nishati safi ya kupikia huku akitolea mfano nchi ya India ambayo asilimia 98 ya wananchi wake hawatumii kuni na mkaa .


“Kamati inayohusika na mradi huu wa  Nishati Safi ya Kupikia inafanya kazi na kabla ya Bajeti ya Mwaka 2023/2024, Serikali itatoa Dira, Mkakati na Mwelekeo wa kuondokana na matumizi ya nishati chafu  na isiyo salama kwa takriban asilimia 80 ndani ya miaka 10, na haya ni maelekezo ya Mhe,Rais hivyo  lazima tuyatekeleze.” Ameeleza Makamba


Katika hatua nyingine, Makamba amewataka watendaji wa Wizara kubuni vyanzo vya mapato vya kutekeleza miradi ya Nishati na kutoitegemea Serikali pekee hivyo amewaelekeza watendaji hao kushirikisha sekta binafsi ili kutekeleza miradi ya nishati.


Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato alimshukuru Waziri wa Nishati kwa ubunifu wa miradi mbalimbali itakayoboresha Sekta ya Nishati nchini na kwamba chini ya uongozi wake tayari kuna mafanikio yanaonekana  na kuahidi kuwa watendaji wa Wizara wataendelea kufanya kazi kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba alimshukuru Waziri kwa jitihada mbalimbali na msukumo anaoutoa katika  Sekta ya Nishati nchini ikiwemo suala la uwepo wa  Nishati Safi ya Kupikia na kusema kuwa Watumishi na viongozi wa Wizara watafanya kila jitihadi ili kutekeleza miongozo anayoitoa.


Akifunga Mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Athuman Mbuttuka amesema kuwa masuala yote yaliyoelekezwa na Viongozi Wakuu wa Wizara yatafanyiwa kazi na kwamba kuna kazi kubwa ya kutekeleza masuala hayo, pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuhudumu katika Sekta ya Nishati na pia amesisitiza uwepo wa ushirikiano katika kutekeleza masuala mbalimbali ya Wizara.

Saturday, 4 March 2023

OSHA YAFANIKIWA KUONGEZA MAENEO YA KAZI YALIYOSAJILIWA KWA ASILIMIA 276.

 

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya mahala Pa kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda Akizungumza na Waandishibwa Habari Jijini Dodoma.



Na. Deborah Lemmubi -Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya mahala Pa kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda amesema kuwa  kutokana na kuimarika kwa shughuli za usimamizi wa usalama na afya mahali pa Kazi, Wakala umefanikiwa kuongeza idadi ya maeneo ya kazi yaliyosajiliwa kutoka 4,336 hadi 11,953 ikiwa ongezeko hilo ni sawa asimilia 276 na idadi ya kaguzi zilizofanyika zimeongezeka kutoka kaguzi 104,203 hadi kufikia Kaguzi 322,241 sawa na asilimia 132.



Bi. Mwenda ameyasema hayo  Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa Umma kupitia vyombo vya habari juu ya  utekelezaji wa shughuli mbalimbali wa  Wakala hiyo,ambapo ni mwendelezo wa Taasisi za Serikali kutoa taarifa za utekelezaji wa Majukumu yao.




"Katika kipindi hiki cha miaka miwili kumekuwa na umarishaji mkubwa sana wa shughuli za usimamizi wa usalama na afya mahali pa Kazi ndio maana usajili wa maeneo ya kazi umeongezeka kwa asilimia 276 ambapo kuna ongezeko kutoka 4,336 hadi 11,953 na hata idadi ya kaguzi tulizoganya nazo zimeongezeka kutoka 104,203 hadi 322,241 sawa na asilimia 132 ni mafanikio makubwa haya"



Bi.Mwenda amesema kumekuwa na ongezeko la asilimia 175 ya Wafanyakazi waliopata mafunzo ya Usalama na afya mahali pa kazi kutoka wafanyakazi 32,670 hadi kufikia Wafanyakazi 43,318.



"Mafunzo haya yanajumuisha mafunzo ya usimamizi wa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi na uundwaji wa kamati za Usalama na Afya (Health and Safety Managemnet System), mafunzo ya kufanya kazi za mazingira ya juu (working at height), mafunzo ya huduma ya kwanza, mafunzo ya usimamizi na udhibiti wa kemikali katika maeneo ya kazi, mafunzo ya usalama na afya katika sekta ya mafuta na gesi na katika sekta ya ujenzi na majenzi, mafunzo ya usalama wa mitambo". 


Aidha, Bi.Mwenda ameongeza kuwa kumekuwa na ongezeko la upimaji afya za wafanyakazi kwa asilimia 320. Upimaji afya kutoka Wafanyakazi 363,820 hadi kufikia Wafanyakazi 1,112,237 waliopimwa katika kipindi hicho cha miaka miwili ,kutotokana na kupunguzwa kwa ada mbalimbali na kuboresha mifumo ya usimamizi ambayo imewezesha maeneo mengi ya kazi kukaguliwa, wafanyakazi wengi kupimwa afya na mafunzo mbalimbali kufanyika, ongezeko hili ni tafsiri kwamba hali ya usalama na afya  katika maeneo ya kazi inazidi kuimarika.



Katika kusimamia Sheria ya Usalama na Afya kwa lengo la kuzuia ajali Bi.Mwenda amesema magonjwa na vifo vitokanavyo na kazi, maeneo ya kazi ambayo hayakuzingatia Sheria na Kanuni za Usalama na Afya yalichukuliwa hatua mbali mbali za kisheria zikiwemo kupewa hati ya maboresho (Improvement Notice) ambapo maeneo ya kazi 1,588 yalipewa hati hizo na maeneo ya kazi mengine 105 yalitozwa faini. 



Mtendaji Mkuu huyo  amebainisha kuwa ,miongoni mwa majukumu ya OSHA ni kuchunguza ajali mbali mbali zinazotokea katika sehemu za kazi kwa lengo la kubaini vyanzo vya ajali hizo ili kushauri namna bora ya kuzuia ajali kutokea tena.



" Katika kipindi cha miaka miwili, ajali zilizoripotiwa zilipungua kwa asilia 13.2 kutoka ajali 2,138 kupungua hadi kufika 1,855.  Magonjwa yanayotokana na kazi yalipungua kwa asilimia 22.1 kutoka wagonjwa 140 kufikia wagonjwa 109".



Katika hatua nyingine Bi.Mwenda asema kuwa katika kipindi hicho cha miaka miwili ya Utawala wa serikali ya Awamu ya Sita,OSHA wamefanikiwa Kupunguza Urasimu na kuboresha   Mifumo ya TEHEMA,ambapo mifumo ya TEHAMA kama TANEPS, GePG, GAMIS, MUSE, E-office imesimikwa na inatumika na imekuwa ni nyenzo muhimu katika kutoa huduma.



"Kwa kutumia mifumo hiyo imetusaidia kupunguza muda wa kupata Cheti cha Usajili wa sehemu za kazi kutoka siku 14 hadi siku 1 kwa kuwa usajili unafanyika kwa njia ya kielektroniki na ambapo mteja ana uwezo kuprinti cheti chake cha usajili popote alipo (Online registration),Kutoa Leseni ya Kukidhi Matakwa ya Sheria ya Usalama na Afya mahali pa kazi (Compliance License) kutoka siku 28 hadi siku 7 kwa sasa".



Dhima kuu ya  Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi(OSHA), ni kuelimisha na Kuhamasisha masuala ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi kwa kuweka mifumo thabiti itakayo zuia ajali, magonjwa na vifo pamoja na uharibifu wa mali ili kupunguza gharama za uendeshaji na kukuza uchumi wa Taifa.

NEMC YASHUGHULIKIA MALALAMIKO TAKRIBANI 369 YA UCHAFUZI NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA NCHINI.


Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira {NEMC} Dkt. Samwel Gwamaka akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma.


Na Deborah Lemmubi - Dodoma.



Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira {NEMC} Dkt. Samwel Gwamaka ameeleza kuwa katika kipindi cha Julai 2021 hadi Februari 2022, Baraza limepokea na kushughulikia malalamiko takribani 369 ya Uchafuzi na Uharibifu wa Mazingira kutoka kwa wananchi ikiwemo kuvuja kwa mafuta kutoka kwenye mabomba ya mafuta ,kuchoma taka hatarishi chini ya kiwango kinachotakiwa kisheria.


Dkt. Gwamaka ameeleza hayo leo Machi 3,2023Jijini Dodoma wakati akielezea kuhusu  mafanikio ya Baraza hilo katika kipindi cha miaka miwili ya Utawala wa serikali ya Awamu ya Sita chini ya Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Ambapo Dkt.Gwamaka amesema malalamiko hayo yalihusisha uchafuzi wa vyanzo vya maji, utiririshaji wa maji taka ,uchafuzi wa hewa kutokana na shughuli za viwandani,kelele za muziki,kushamiri kwa gereji bubu maeneo ya makazi,kushamiri vituo vya mafuta katikati ya makazi ya watu,matumizi ya mifuko ya plastiki iliyokatwa na kutapaka maeneo ya makazi na kuhakikisha inatoa elimu elimu sahihi na suluhisho juu ya jambo husika.

Aidha Dkt Gwamaka amesema Baraza limefanikiwa kusajili miradi 1702 ambapo kati yake 967 ni ya {TAM} na 735 ni ya ukaguzi wa Mazingira.


"Kwa kupitia taarifa ya Tathimini ya Athari kwa Mazingira katika kipindi cha Julai 2021 hadi Februari 2022 Baraza limefanikiwa kusajili miradi 1702 ambapo kati yake 967 ni ya {TAM} na 735 ni ya ukaguzi wa Mazingira".


Katika hatua nyingine Dkt.Gwamaka amebainisha kuwa Baraza hilo limetoa Jumla ya Vibali 174 vya kushughulika na taka hatarishi ndani ya Nchi ambapo vibali 10 vya kuingiza na kusafirisha nje ya Nchi na kupelekea kiasi cha Tani 516,041 za taka mbalimbali kukusanywa na makampuni yenye vibali.

"kukusanywa huku kwa tani 516,041 za taka inaonesha jinsi Braza linavyowajibika katika kuhakikisha Sheria ya Mazingira inayozingatia uhifadhi na utunzaji wake unazingatiwa na ndio maana pia tumetoa jumla ya vibali 174 vya kushughulika na taka hatarishi ndani ya Nchi yetu .


Hata hivyo amebainisha usimamizi wa tafiti za Mazingira huku ikifanikiwa kuratibu uteuzi wa Eneo la Rufiji-Mafia-Kibiti-Kilwa {RUMAKI} ikiwa na lengo la kujumuishwa katika mtandao wa kidunia wa Hifadhi za Binadamu na Hifadhi hai.

Thursday, 2 March 2023

WCF KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA MUHIMU KWA WADAU NCHINI KWA NJIA YA MTANDAO.

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi {WCF} Dkt. John Mduma akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma Leo March 2,2023.


Na Deborah Lemmubi - Dodoma.



MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi {WCF} Dkt. John Mduma amesema kuwa mfuko umeendelea kuboresha huduma muhimu kwa wadau nchi nzima kwa njia ya mtandao ili kufikia malengo ya Mfuko huo.


Huduma hizo za kimtandao ni pamoja na Usajili wa wanachama ambapo wanachama wa Mfuko huo ni Waajiri, kupata cheti cha Usajili,kuwasilisha michango kila mwezi na Mfuko unapokea mchango kupitia nambari ya Udhibiti ambayo hupatikana kwa njia ya Mtandao.



Dkt. Mduma amebanisha haya wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Mfuko huo leo Machi 2,2023, Jijini Dodoma na kusema hadi kufikia Juni 30 2022 Mfuko umekusanya kiasi cha Shillingi Bilioni 241.48 ikiwa ni kutokana na mapato ya uwekezaji.


"Hadi kufikia tarehe 30 June 2022,Mfuko umekusanya jumla ya Shillingi Billioni 241.48 toka kwenye mapato yanayotokana na uwekezaji"


Aidha amesema kuwa kabla ya kuanzishwa kwa WCF malipo ya fidia nchini kwa mwaka mzima yalikuwa chini ya Shillingi millioni 200 lakini baada ya kuanzishwa kwa Mfuko huo malipo yanaongezeka kila mwaka.

"Mfuko huu umekuwa na faida kubwa kwani lengo,lake kubwa ni kuwakomboa wafnykazi waliopata madhili ama majanga wakiwa kazini kutoka katika dimbwi la umasikini ambapo takwimu za hivi karibuni zikionesha tangu kuanzishwa, idadi ya wanufaika wa Mfuko imefikia 10,454 ambao wamelipwa jumla ya shilingi Billioni 49.44".


Katika hatua nyingine,Dkt.Mduma amesema kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Machi 2021 hadi Februari 2023 Waajiri wapya 5,250 wamejisajili WCF huku kati ya waajiri hao asilimia 99.27% ni waajiri wakubwa ,huku asilimia 98.71% ni waajiri wa kati na waajiri wa chini ni asilimia 88.56%.


"Waajiri wengi kwa sasa wanavutiwa kujisajili na WCF kutokana na Serikali sikivu ya awamu ya sita kupunguza kiwango cha mchango kwa sekta binafsi kutoka asilimia 1 ya hapo awali kabla ya maboresho ya kisera hadi asilimia 0.5 ya sasa hivyo kuleta mlingano wa michango kuwa sawa na sekta za umma,"


Na kuongeza kuwa "Lakini serikali pia imeendelea kuleta unafuu kwa waajiri kwa kupunguza kiwango cha kodi ya malimbikizo ya madeni ya michango ya nyuma kutoka asilimia kumi (10%) hadi asilimia mbili (2%)


Hata hivyo kumekuwa na ongezeko kubwa la waajiri kujisajili kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi {WCF} katika kipindi cha Awamu ya Sita.


Wednesday, 1 March 2023

TPHPA YABAINISHA KUWA UDANGANYIFU WA WAUZAJI NA MATUMIZI YASIYO SAHIHI YA VIUATILIFU NI KIKWAZO KUKABILIANA NA WADUDU WAHARIBIFU WA MIMEA NCHINI.

 


Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.



Na Deborah Lemmubi - Dodoma.


KAIMU Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru amebainisha kuwa  Matumizi yasiyosahihi ya viuatilifu na udaganyifu wa baadhii ya wauzaji wa viuatilifu na mazao ya mimea imekuwa kikwazo katika kukabiliana na wadudu waharibifu wa mimea hapa Nchini.

Prof. Ndunguru amebainisha haya Jijini hapa leo Machi 1,2023  wakati akizungumza na wanahabari akielezea kuhusu majukumu na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo kwa mwaka 2022/2023.
Prof. Ndunguru amesema kuwa Uelewa mdogo wa wakulima na wadau wengine juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu, na uwepo wa wauuzaji wa Viuatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu imesababisha kuendelea kuwepo kwa wadudu wasumbufu wa mimea.

“Matumizi yasiyosahihi ya viuatilifu na udaganyifu wa baadhii ya wauzaji wa viuatilifu changanya na Uelewa mdogo wa wakulima na wadau wengine juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu, na uwepo wa wauuzaji wa Viuatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu imesababisha kuendelea kuwepo kwa wadudu visumbufu wa mimea".

Aidha ameeleza madhara ya kutumia viuatilifu visivyo sahihi kwa wakulima kuwa inawaongezea gharama kwa sababu mkulima analazimika kutumia viuatilifu vingi  na inaathiri afya yake na mazingira kwa ujumla.

“Madhara ni mengi ndio maana tulitilia mkazo kwa kuwajengea uelewe wakulima juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu sababu wanapopulizia viuatilifu visivyosahihi vinawajengea usugu wadudu waharibifu na kuuwa wadudu rafiki wa mimea".

Akitoa takwimu za Uchambuzi wa sampuli mbalimbali zilizofanywa na  Mamlaka hiyo ,Prof. Ndunguru ameeleza kuwa sampuli 1025 za viuatilifu (analysis of pesticide samples) ambazo zimeshafanyika ikiwa sampuli 1005 sawa na asilimia (98.04%) zilikidhi viwango huku sampuli 20 (1.96%) zimeonesha kutokidhi viwango.

Na kusema kuwa Jumla ya viuatilifu vipya 409 na kampuni za ufukizaji
198 vilisajiiliwa huku Vibali vya shehena za viuatilifu 1324 vyenye ujazo wa lita 58,379,97.98 na kilogram 3,880,772.77 ambapo Jumla ya vibali vya maduka 802 vilitolewa kwa wafanyabiashara wa Viuatilifu.

''Jumla ya viuatilifu vipya 409 na kampuni za ufukizaji 198 vilisajiiliwa Vibali vya shehena za viuatilifu 1324; ujazo wa lita 58,379,97.98 na kilogram 3,880,772.77 Mapato kiasi cha TZS Bilioni 3.06 Jumla ya vibali vya maduka 802 vilitolewa kwa wafanyabiashara wa Viuatilifu''.

Aidha amesema Mamlaka kwa kushirikiana na Wizara ya kilimo imefanya uchambuzi wa sampuli za udongo takribani 1300 kutoka kwenye mashamba ya “Block farming”na kutumia Matokeo ya uchambuzi yatawezesha kutoa ushauri kulingana na eneo husika.

Majukumu ya mamlaka hii ya afya ya mimea na viuatilifu ni Kuwezesha biashara ya mimea na mazao ya mimea hapa nchini na kimataifa Pamoja na Kudhibiti uagizaji, usafirishaji, utengenezaji, usambazaji, uuzaji, matumizi ya viuatilifu na vifaa vya unyunyiziaji wa viuatilifu.

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...