mwambelablog

Wednesday, 1 March 2023

TPHPA YABAINISHA KUWA UDANGANYIFU WA WAUZAJI NA MATUMIZI YASIYO SAHIHI YA VIUATILIFU NI KIKWAZO KUKABILIANA NA WADUDU WAHARIBIFU WA MIMEA NCHINI.

 


Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.



Na Deborah Lemmubi - Dodoma.


KAIMU Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru amebainisha kuwa  Matumizi yasiyosahihi ya viuatilifu na udaganyifu wa baadhii ya wauzaji wa viuatilifu na mazao ya mimea imekuwa kikwazo katika kukabiliana na wadudu waharibifu wa mimea hapa Nchini.

Prof. Ndunguru amebainisha haya Jijini hapa leo Machi 1,2023  wakati akizungumza na wanahabari akielezea kuhusu majukumu na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo kwa mwaka 2022/2023.
Prof. Ndunguru amesema kuwa Uelewa mdogo wa wakulima na wadau wengine juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu, na uwepo wa wauuzaji wa Viuatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu imesababisha kuendelea kuwepo kwa wadudu wasumbufu wa mimea.

“Matumizi yasiyosahihi ya viuatilifu na udaganyifu wa baadhii ya wauzaji wa viuatilifu changanya na Uelewa mdogo wa wakulima na wadau wengine juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu, na uwepo wa wauuzaji wa Viuatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu imesababisha kuendelea kuwepo kwa wadudu visumbufu wa mimea".

Aidha ameeleza madhara ya kutumia viuatilifu visivyo sahihi kwa wakulima kuwa inawaongezea gharama kwa sababu mkulima analazimika kutumia viuatilifu vingi  na inaathiri afya yake na mazingira kwa ujumla.

“Madhara ni mengi ndio maana tulitilia mkazo kwa kuwajengea uelewe wakulima juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu sababu wanapopulizia viuatilifu visivyosahihi vinawajengea usugu wadudu waharibifu na kuuwa wadudu rafiki wa mimea".

Akitoa takwimu za Uchambuzi wa sampuli mbalimbali zilizofanywa na  Mamlaka hiyo ,Prof. Ndunguru ameeleza kuwa sampuli 1025 za viuatilifu (analysis of pesticide samples) ambazo zimeshafanyika ikiwa sampuli 1005 sawa na asilimia (98.04%) zilikidhi viwango huku sampuli 20 (1.96%) zimeonesha kutokidhi viwango.

Na kusema kuwa Jumla ya viuatilifu vipya 409 na kampuni za ufukizaji
198 vilisajiiliwa huku Vibali vya shehena za viuatilifu 1324 vyenye ujazo wa lita 58,379,97.98 na kilogram 3,880,772.77 ambapo Jumla ya vibali vya maduka 802 vilitolewa kwa wafanyabiashara wa Viuatilifu.

''Jumla ya viuatilifu vipya 409 na kampuni za ufukizaji 198 vilisajiiliwa Vibali vya shehena za viuatilifu 1324; ujazo wa lita 58,379,97.98 na kilogram 3,880,772.77 Mapato kiasi cha TZS Bilioni 3.06 Jumla ya vibali vya maduka 802 vilitolewa kwa wafanyabiashara wa Viuatilifu''.

Aidha amesema Mamlaka kwa kushirikiana na Wizara ya kilimo imefanya uchambuzi wa sampuli za udongo takribani 1300 kutoka kwenye mashamba ya “Block farming”na kutumia Matokeo ya uchambuzi yatawezesha kutoa ushauri kulingana na eneo husika.

Majukumu ya mamlaka hii ya afya ya mimea na viuatilifu ni Kuwezesha biashara ya mimea na mazao ya mimea hapa nchini na kimataifa Pamoja na Kudhibiti uagizaji, usafirishaji, utengenezaji, usambazaji, uuzaji, matumizi ya viuatilifu na vifaa vya unyunyiziaji wa viuatilifu.

No comments:

Post a Comment

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...