Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira {NEMC} Dkt. Samwel Gwamaka akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma.
Na Deborah Lemmubi - Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira {NEMC} Dkt. Samwel Gwamaka ameeleza kuwa katika kipindi cha Julai 2021 hadi Februari 2022, Baraza limepokea na kushughulikia malalamiko takribani 369 ya Uchafuzi na Uharibifu wa Mazingira kutoka kwa wananchi ikiwemo kuvuja kwa mafuta kutoka kwenye mabomba ya mafuta ,kuchoma taka hatarishi chini ya kiwango kinachotakiwa kisheria.
Dkt. Gwamaka ameeleza hayo leo Machi 3,2023Jijini Dodoma wakati akielezea kuhusu mafanikio ya Baraza hilo katika kipindi cha miaka miwili ya Utawala wa serikali ya Awamu ya Sita chini ya Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ambapo Dkt.Gwamaka amesema malalamiko hayo yalihusisha uchafuzi wa vyanzo vya maji, utiririshaji wa maji taka ,uchafuzi wa hewa kutokana na shughuli za viwandani,kelele za muziki,kushamiri kwa gereji bubu maeneo ya makazi,kushamiri vituo vya mafuta katikati ya makazi ya watu,matumizi ya mifuko ya plastiki iliyokatwa na kutapaka maeneo ya makazi na kuhakikisha inatoa elimu elimu sahihi na suluhisho juu ya jambo husika.
Aidha Dkt Gwamaka amesema Baraza limefanikiwa kusajili miradi 1702 ambapo kati yake 967 ni ya {TAM} na 735 ni ya ukaguzi wa Mazingira.
"Kwa kupitia taarifa ya Tathimini ya Athari kwa Mazingira katika kipindi cha Julai 2021 hadi Februari 2022 Baraza limefanikiwa kusajili miradi 1702 ambapo kati yake 967 ni ya {TAM} na 735 ni ya ukaguzi wa Mazingira".
Katika hatua nyingine Dkt.Gwamaka amebainisha kuwa Baraza hilo limetoa Jumla ya Vibali 174 vya kushughulika na taka hatarishi ndani ya Nchi ambapo vibali 10 vya kuingiza na kusafirisha nje ya Nchi na kupelekea kiasi cha Tani 516,041 za taka mbalimbali kukusanywa na makampuni yenye vibali.
"kukusanywa huku kwa tani 516,041 za taka inaonesha jinsi Braza linavyowajibika katika kuhakikisha Sheria ya Mazingira inayozingatia uhifadhi na utunzaji wake unazingatiwa na ndio maana pia tumetoa jumla ya vibali 174 vya kushughulika na taka hatarishi ndani ya Nchi yetu .
Hata hivyo amebainisha usimamizi wa tafiti za Mazingira huku ikifanikiwa kuratibu uteuzi wa Eneo la Rufiji-Mafia-Kibiti-Kilwa {RUMAKI} ikiwa na lengo la kujumuishwa katika mtandao wa kidunia wa Hifadhi za Binadamu na Hifadhi hai.
No comments:
Post a Comment