Ndg.Eric Hamissi wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma.
Na Deborah Lemmubi-Dodoma.
Imeelezwa kuwa katika mwaka fedha 2022/2023 Serikali imeitengea Shilingi Bilioni 111.8 Kampuni ya huduma za Meli Tanzania MSCL kwa ajili ya ujenzi wa miradi 12.
Katika miradi hiyo 12 kuna miradi 4 ambayo ni mipya,miradi 5 ni ya ukarabati na miradi 3 inayoendelea kutekelezwa tangu mwaka wa fedha uliopita.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Ndg.Eric Hamissi wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha wa 2022-2023.
Ambapo Eric amesema kuwa kati ya hizo Bilioni 111.8 Ziwa Tanganyika imetengewa kiasi cha Shilingi bilioni 53.9 itakayotumika kwa ajili ya kutekeleza miradi Mipya na kukarabati meli zinginine ikiwemo Meli Kongwe yenye miaka 105 ya MV Liemba.
"Katika ziwa Tanganyika kuna mradi mpya wa ujenzi wa Meli Mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo ambapo kwa mwaka huu wa fedha imetengewa jumla ya Bilioni 12,na mradi mwingine mpya kwa upande wa ziwa Tanganyika ni ujenzi wa Cherezo ambao nao umetengewa bilioni 12,
Na kuongeza kuwa " Mradi mwingine mpya ni ujenzi wa Meli Mpya ya Mizigo tu ambapo itakuwa na uwezo wa kubeba tani 3000 nayo imetengewa bilioni 12 kwa mwaka huu wa fedha"
Aidha amesema kuwa katika ziwa Tanganyika wapo katika ukarabati wa Meli ya MT Sangara,MV Liemba ,MV Mwongozo ambayo inabeba idadi ya watu 800 na tani 80 ya mzigo pamoja na kukarabati Boti ya Kitalii ya Sea Warriors.
Kwa Upande wa Ziwa Victoria imetengewa kiasi cha Bilioni 59 ambapo kati ya hizo bilioni 24 zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa MV Mwanza Hapa kazi Tu ambapo mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 73.
Pia Mtendaji huyo amesema wataendelea na ukarabati wa Mv Umoja ambapo imetengewa Bilioni 1.7,Mv Ukerewe ambapo imetengewa bilioni 3.5 na ukarabati wa Meli ya Mafuta ya MT Nyangumi yenye uwezo wa kubeba lita 350 nayo imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 6.8.
"Tutajenga pia Meli nyingine Mpya kabisa ya Mizigo ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba tani 3000 ambapo katika mwaka huu imetengewa bilioni 12 na hii itasaidia sana kuunganisha na Uganda yenye soko kubwa sana la bidhaa ambayo inahitaji zaidi ya tani elfu sita hivyo kukamilika kwa meli hii itasaidia sana nchi kuingiza mapato makubwa"
Pia amesema kuwa huduma ya usafiri kwa njia ya maji ni moja ya njia rahisi sana ndio maana serikali imeona umuhimu wa kuwekeza fedha nyingi ili kuimarishwa kwa miundombinu hiyo.
Pia Kampuni hiyo kabla ya kutetereka ilikuwa inaajiri zaidi ya vijana 300 ila baada ya kufa ila baada ya kufufuliwa tena kwa sasa ina wafanyakazi 120 ila miradi yote hii ikikamilika itaongeza idadi ya ajira na mapato pia yataongezeka kwa taifa.
Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa amesema kuwa serikali ya awamu ya sita mbali nakufanya juhudi za miradi ya ujenzi wa meli serikali pia inafanya uboreshaji wa bandari zote za maziwa makuu.
Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania inamilikiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Tanzania imejikita katika kusafirisha mizigo na abiria kwa njia ya maji ikiwa na meli 17 na boti 1 ya kitalii na makao makuu yake yakiwa ni jijini Mwanza.
#mwambelaUpdates
No comments:
Post a Comment