mwambelablog

Tuesday, 1 November 2022

BINADAMU ANATAKIWA KULA NYAMA WA

 



KUTOKA DODOMA

IMEELEZWA KUWA ILI MWILI WA BINADAMU UPATE VIRUTUBISHO VYOTE MUHIMU MTU MMOJA ANATAKIWA KWA WIKI WALAU ALE KILO MOJA YA NYAMA KWANI VIRUTUBISHO VINAVYOPATIKANA KWENYE NYAMA NYEKUNDU HAVIPATIKANI KWENYE MIMEA NA KITAALAMU MTU ANAPASWA KULA NYAMA ANGALAU KILO HAMSINI KWA MAWAKA.

AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA BODI YA NYAMA TANZANIA KWA MWAKA WA FEDHA 2022-2023 MSAJILI WA BODI HIYO DKT. DANIEL MUSHI AMESEMA KUNA WATU WAMEKUWA WAKISEMA NYAMA NI MBAYA LAKINI UZURI AU UBAYA WA KULA NYAMA UNATOKANA NA KIASI CHA NYAMA MTU ANACHOKULA NA AINA YA NYAMA ANAYOKULA.


AIDHA AMESEMA KUWA ENDAPO MTU ATAKULA NYAMA KWA KIWANGO KINACHOTAKIWA MTU HUYO ATAKUA NA AFYA KWANI ITASAIDIA KUIMARISHA KINGA YA MWILI YAKUPAMBANA NA MAGONJWA NYEMELEZI NA NGUVU YAKUFANYA KAZI HIVYO ITASAIDIA KUONGEZA UZALISHAJI.


KATIKA HATUA NYINGINE AMESEMA KUWA BODI ITAHAKIKISHA INALINDA AFYA YA MLAJI KUPITIA UDHIBITI NA UKAGUZI SAMBAMBA NA KUHAMASISHA UZAJISHAJI BORA WA NYAMA ILI KUPATA MASOKO NJE YA NCHI.


MWAKA 2006 SERIKALI ILITUNGA SHERIA YA TASNIA YA NYAMA SURA YA 421 YENYE LENGO LA KUWEZESHA MABADILIKO KATIKA TASNIA YA NYAMA, KUANZISHA MISINGI THABITI YA USIMAMIZI, KUHAKIKISHA UPATIKANAJI WA BIDHAA BORA ZA NYAMA, KUENDELEZA UKUAJI WA TASNIA YA NYAMA NA BODI YA NYAMA TANZANIA ILIANZISHWA KATIKA SHERIA HII ILI KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA SHERIA HUSIKA.

No comments:

Post a Comment

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...