mwambelablog

Tuesday, 28 February 2023

KATIBU MKUU DKT. YONAZI APOKELEWA RASMI OFISI YA WAZIRI MKUU AOMBA USHIRIKIANO.



Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akipokea ua kutoka kwa Mwandishi Mwendesha Ofisi  kutoka Ofisi hiyo Bi. Tusekile Mwakangata mara baada ya kuwasili rasmi katika Ofisi hiyo,  Februari 28, 2023 Jijini Dodoma.


Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi hiyo, Dkt. Jim Yonazi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya mapokezi mara baada ya kuwasili rasmi Ofisini hapo Jijini Dodoma tarehe 28 Februari, 2023. 



NA. MWANDISHI WETU- Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi  amepokelewa rasmi  katika Ofisi ya Waziri Mkuu  hii leo Februari 28, 2023 Jijini Dodoma na kutoa wito kwa Menejimenti na watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu kwa lengo la kuleta ufanisi.

Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Stella Mwaiswaga akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo wakati wa haflaya kumpokea kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi.

 

Dkt. Yonazi amewasihi watumishi hao kufanya kazi kwa juhudi, upendo na Amani ili kuwatumikia wananchi na kuifaya Ofisi ya Waziri Mkuu kuendelea na jukumu lake kubwa la kuratibu shughuli za Serikali kwa matokeo chanya.

Baadhi ya Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi hiyo, Dkt. Jim Yonazi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya mapokezi.

 

Katika hafla hiyo ya mapokezi amewasihi watumishi kuwa wamoja na kufanya kazi kwa weledi zaidi huku akiwashukuru kwa mapokezi mazuri.

Nimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Sulluhu Hassan kwa kuniteua kuitumikia nafasi hii, ikumbukwe  kuwa tuna jukumu kubwa la kuwatumikia wananchi hivyo tufanye  kazi kwa juhudi huku tukidumisha ushirikiano, Alieleza Dkt. Yonazi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo Februari 28, 2023Jijini Dodoma.

 

DKT.NDUMBARO AMEWATAKA VIONGOZI WA TAASISI ZA UTOAJI HAKI KUSHIRIKIANA KATIKA KUONDOA VIKWAZO VINAVYOKWAMISHA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA WATOA TAARIFA

 


Na.Mwandishi Wetu,

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Dkt.Damas Ndumbaro ,amewataka viongozi wa taasisi za utoaji haki kushirikiana katika kuondoa vikwazo vinavyokwamisha utekelezaji thabiti wa Sheria ya watoa Taarifa na Ulinzi wa Mashahidi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.


Dkt.Ndumbaro ameyasema hayo leo Februari 28,2023 Jijini Dodoma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kanuni za watoa taarifa na Ulinzi wa Mashahidi ,ambapo amesema kuwa taarifa zinaonesha kuwa utayari wa wananchi kutoa taarifa umeongezeka na walio wengi wako tayari kushiriki katika mapambano dhidi ya uhalifu kwa kufika katika vyombo vya sheria.

Amesema kuwa watanzania wakishiriki kwa pamoja katika kufichua maovu yakiwemo yanayosababisha hasara kwa taifa utasaidia kukuza uchumi na kuweka mazingira wezeshi kwa uwekezaji.

4I6A6210.JPG


"Ili tufikie malengo yaliyokusudiwa ya kuhakikisha tunafichua kila aina ya maovu yanayotokea ikiwemo ufisadi,ukiukwaji wa haki za binadamu na matumizi mabaya ya madaraka na mengine mengi yaweze kuripotiwa bila woga kwa maslahi mapana ya nchi yetu,"

Na kuongeza kuwa "Niwaombe tuendelee kutoa elimu ya kisheria kwa umma wa watanzania kuhusiana na sheria na kanuni tajwa ili wawe na uelewa na wajue umuhimu wa kuwafichua wahalifu wa makosa mbalimbali yanayotendeka katika jamii yetu ili mwisho wa siku matukio ya kiuhalifu yapungue na na hatimaye kuisha kabisa,"amesema Dkt.Ndumbaro

4I6A6242.JPG

Pia Dkt.Ndumbaro amewataka wananchi kutohofia kujitokeza kutoa taarifa za uhalifu na matendo ya aina zote yanayofanywa kinyume cha sheria, kwani taarifa hizo zitakuwa siri na zitafanyiwa kazi bila ya kuwataja watoa taarifa , pia mashahidi wanapotakiwa kufika mahakamani wasiogope kwani Kanuni hizo zinaweka mfumo wa kuwalinda ambao unaeleza masharti na namna za ulinzi huo.

"Kanuni hizi zinalenga kurahisisha utekelezaji wa Sheria na kuongeza ufanisi katika utekelezaji na kufikiwa kwa madhumuni ya Sheria. Sambamba na hilo, Kanuni hizi zitasaidia kuwapatia ulinzi wa kisheria wale wote wanaotoa taarifa za uhalifu wa makosa ya aina mbalimbali na hivyo kuwaongezea imani na usalama wao na hivyo kurahisha uendeshaji wa mashtaka,"amesisitiza Dkt.Ndumbaro

4I6A6230.JPG

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na ufuatiliaji Haki Kharist Luanda amesema kuwa kuzinduliwa kwa kanuni hizo inafungua milango kwa wananchi kuanza kutoa taarifa mbalimbali kwa kujiamini kwani kanuni hizo zimebainisha namna watoa taarifa na mashahidi watakavyopatiwa ulinzi.

"Kanuni hizi ni muhimu sana kwani zinamuhakikishia ulinzi mtoa taarifa na shahidi na kumtengenezea uhuru hata wakati wa kutoa ushahidi mahakamani kwa sababu kanuni hizi zimeshamuhakikishia usalama,"amesema Luanda


Kanuni hizo za Watoa Taarifa na Ulinzi wa Mashahidi zimekuja baada ya Serikali, mwaka 2016 kuanza kutekeleza Sheria ya Watoa Taarifa na Ulinzi wa Mashahidi ya mwaka, 2016 (The Whistleblower and Witness Protection Act. 2016 ,sheria hiyo ikiwa na lengo la kuimarisha misingi ya utoaji haki jinai na kukuza utawala bora na mapambano dhidi ya uhalifu nchini.

Monday, 27 February 2023

NDANI YA AZMA YA KUMTUA MAMA NDOO KICHWANI, IRUWASA YAONGOZA KUFUNGA MITA NYINGI ZA MALIPO YA KABLA KWA WATEJA 6,752.

Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Iringa (IRUWASA)  Mhandisi David Pallanjo akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma.




Na.Deborah Lemmubi - Dodoma.


Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Iringa (IRUWASA)  Mhandisi David Pallangyo amesema kuwa Mamlaka hiyo inajivunia mafanikio katika eneo la TEHAMA kwa kufunga mita za malipo  ya kabla (prepaid water meters) kwa wateja 6,752 na kuwa Mamlaka ya kuongoza nchini kwa kufunga mita nyingi za malipo kabla.

Mhandisi Pallangyo amesema hayo Jijini hapa, leo Februari 27 ,2023 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu mafanikio na utekelezaji wa shughuli na majukumu ya mamlaka hiyo.

Mhand.Pallangyo amesema kuwa ufungaji wa mita hizo za maji zimesababisha kwa kiwango kikubwa cha vyombo vya habari na malalamiko ambayo yalikuwa yakilalamikiwa hapo awali.

“Mamlaka imejitahidi kusaidia inafunga mita za malipo kabla kwa wanachi pamoja na baadhi ya taasisi ambayo kwa kiasi kikubwa zimesaidia malalamiko, na kuwafanya kuwaamini kuwa wanachotumia ni sahihi na wala hawaibiwi,

“Mamlaka inaendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa maji ya kutosha sambamba na wadau mbalimbali katika vyanzo vya maji ili kutuma ujumbe na mazingira jambo ambalo umuhimu wake ni kuwa shida”.

Aidha Pallangyo ameeleza kuwa kiasi cha sh. bilioni 2 zimetumika kwa ajili ya miradi ya maji ya IRUWASA ambapo fedha hizo zitengwa kusaidia miradi ya maji inaendelea kuimarika na kuwafanya wakazi wa mkoa na tatizo la maji.

Amesema kuwa katika miradi hiyo pia kufungua fursa ya ajira zaidi ya 6400 za mikataba na kuzungumza pato la mtu mmoja na taifa huku kila mmoja na akiwa shahuku ya kufanya kazi kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.

Vilevile Mha.Pallangyo ameeleza kuwa IRUWASA imeweza kuvuka lengo la sera ya Maji na Ilani ya Chama tawala ya kutoa huduma ya elimu kwa mji wa Iringa na maeneo ya pembezoni inayowafikia wakazi hao asilimia 97.

Pia IRUWASA imefanikiwa kupata huduma ya maji Mjini Iringa amesema maeneo ya pembezoni kwa wastani wa saa 23 kwa siku.

“IRUWASA imefanikiwa kuongeza maduhuli (revenue collection) kwa huduma zilizotolewa kutoka wastani wa Tshs 770M/= (2020) kwa mwezi hadi 860M/= (2023) hivyo hali hii inaiwezesha IRUWASA kuweza kugharamia kwa kiasi kikubwa kikubwa cha taasisi".

Pamoja na hayo amesema IRUWASA imefanikiwa kiasi cha maji yasiyolipiwa (NRW) kwa upande wa Iringa Mjini kutoka wastani wa 24.6 (2020) hadi wastani wa 22.52% ,mwezi wa Desemba, 2022 

huku idadi ya wateja/maunganisho ya Majisafi imeongezeka kutoka 28,133 (2020) hadi 40,549 (Desemba, 2022)
 

Thursday, 23 February 2023

TANZANIA YASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO YA KUANZISHWA KITUO CHA HUDUMA ZA KIBINADAMU NA OPERESHENI ZA DHARURA.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Mh. Geogre Simbachawene akitia Saini Mkataba wa Makubaliano ya Kuanzishwa kwa Kituo cha Huduma za Kibinadamu na Operesheni za Dharura cha Jumuiya ya Maendleo Kusini mwa Africa (SADC) jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Mh. Geogre Simbachawene akitia Saini Mkataba wa Makubaliano ya Kuanzishwa kwa Kituo cha Huduma za Kibinadamu na Operesheni za Dharura cha Jumuiya ya Maendleo Kusini mwa Africa (SADC) jijini Dodoma.


Na,Winner Marawiti ,Dodoma.

Serikali ya Tanzania imesema itahimarisha na kuendeleza ushirikiano  baina ya nchi Wanachama katika  kukabiliana na maafa, Kuimarisha usalama wa watu na kujenga mazingira rafiki ya shughuli za maendeleo  ili kukuza uchumi.


Kauli hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Mh. Geogre Simbachawene katika Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Makubaliano ya Kuanzishwa Kituo cha Huduma za Kibinadamu na Operesheni za Dharura cha Jumuiya ya Maendleo Kusini mwa Africa (SADC) na kusema Jumuiya hiyo imeendelea kushirikiana katika masuala ya usimamizi wa maafa kupitia Kamati ya Mawaziri wenye Dhamana ya Usimamizi wa Maafa. 


Aidha Mkataba huo umepitishwa na kamati zote zinazohusika ikiwemo Kamati ya Mawaziri wanaohusika na usimamizi wa maafa Aprili, 2022 Lilongwe, Malawi; Kamati ya Mawaziri wanaohusika na usimamizi wa sheria na Wanasheria Wakuu Julai, 2022 Lilongwe Malawi; na Baraza la Mawaziri katika mkutano wa kawaida uliofanyika Agosti, 2022 Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huku Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika tarehe 17 na 18 Agosti, 2022 Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo uliidhinisha Mkataba huu na kuelekeza kuwa usainiwe na Mawaziri wanaohusika katika usimamizi wa maafa.

''Kamati ya Mawaziri wanaohusika na usimamizi wa sheria na Wanasheria Wakuu Julai, 2022 Lilongwe Malawi; na Baraza la Mawaziri katika mkutano wa kawaida uliofanyika Agosti, 2022 Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huku Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika tarehe 17 na 18 Agosti, 2022 Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo uliidhinisha Mkataba huu na kuelekeza kuwa usainiwe na Mawaziri wanaohusika katika usimamizi wa maafa''Mh Simbachawene.


Kwa upande wake Mwakilishi kutoka SADC Phineas Matto (Legal Cancel Office SADC in Tanzania) amesema Tanzania ndio Nchi ya kwanza kusaini Mkataba huo, na umekuja wakati ambapo unahitajika kutokana na matukio mbalibali ya majanga yanayoendleea kutokea duniani.

SERIKALI MTANDAO (e-EGA) KUTEKELEZA MIKAKATI KUIMARISHA JITIHADA ZAKE KWA MIAKA 10 IJAYO.

 

Mhandisi Ndomba ameyasema hayo mapema leo hii Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo.


Na. Deborah Lemmubi - Dodoma.


MKURUGENZI Mkuu Mamlaka ya Serikali Mtandao(e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba amesema kuwa

katika kuhakikisha wanaijenga Serikali ya Kidijiti, Katika kipindi cha miaka 10 ijayo,itaandaa na kutekeleza mikakati madhubuti ili kuimarisha zaidi utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao.


Mhandisi Ndomba ameyasema hayo mapema leo hii Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo.


Na kueleza kuwa mikakati hiyo ni pamoja na kuwa na Sehemu moja ambayo huduma mtandao zote zitakuwa zinapatikana,Uwezo wa kutumia teknolojia mpya zinazoibuka, hasa zile za akili bandia, sarafu za kidijiti na teknolojia za kifedha, ili kuwezesha maboresho ya kiutendaji katika Taasisi za Umma na utoaji wa huduma kwa Umma.


“Pia Uzalishaji wa vifaa na miundombinu ya TEHAMA (Hardware) ndani ya Tanzania pamoja na Mifumo na miundombinu ya Serikali mtandao iliyobora na imara zaidi".


Pia Mha.Ndomba amefafanua kuwa ili kufikia yote hayo katika kipindi kijacho, Mamlaka imepanga kushughulikia maeneo ya kipaumbele kama kuendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Serikali Mtandao kwa Taasisi zote za umma, ikiwa ni pamoja na kupitia na kukagua miradi na Mifumo ya TEHAMA ya kimkakati, kisekta na kitaasisi ili kuhakikisha kuwa imetengenezwa na inatumika kwa kufuata Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo iliyopo na kushauri maeneo ya kuboresha na kufuatilia utekelezaji wake.


Pia Kupitia na kutathmini hali ya usalama wa Mifumo na Miundombinu ya Serikali Mtandao na kuzishauri Taasisi za Umma katika maeneo ya kuboresha, pamoja na kufuatilia utekelezaji wake ili kuhakikisha kuwa Mifumo na Miundombinu ya TEHAMA inafanya kazi wakati wote kwa ufanisi na usalama.


Pamoja na hayo Mha.Ndomba amesema kuwa  Mamlaka inashirikiana na Wakala ya Serikali Mtandao Zanzibar (eGAZ) kwa lengo la kuhakikisha Serikali Mtandao inaimarika kote Bara na Visiwani.


“Kupitia ushirikiano huu, Mifumo kadhaa imeboreshwa na inatumiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mifumo hii ni pamoja na Mfumo wa Barua Pepe Serikalini, Mfumo wa Masjala, Mfumo wa Malipo Zanzibar (ZanMalipo), Mfumo wa Ajira (ZanAjira), e-Wawakilishi na Mfumo wa Ankara za Maji (MAJIIS) kwa ajili ya Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA). Pia, Mamlaka inashirikiana na eGAZ katika utoaji wa huduma ya miundombinu ya Serikali mtandao".


Aidha ameeleza kuwa Serikali Mtandao ni matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika utendaji kazi wa Taasisi za Umma na utoaji wa huduma kwa wananchi. 


Ambapo amesema Lengo la Serikali Mtandao ni kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika Taasisi za Umma pamoja na kuboresha utoaji wa huduma kwa Umma ili huduma hizo zipatikane kwa urahisi, haraka na kwa gharama nafuu kupitia tehama.

Wednesday, 22 February 2023

TANESCO YAJIWEKEA MALENGO YA KUZALISHA UMEME MEGAWATI 5000 HADI 6000 IFIKAPO 2025 NA KUUZA NJE YA NCHI.


Bw.Martin Mwambene Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa Wateja kutoka TANESCO, Wakati akizungumza na wanahabari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo jijini Dodoma.



Na Deborah Lemmubi.

Kutoka Dodoma.

Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO)limesema kuwa linatekeleza miradi kadhaa ya umeme ambalo linatumia kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa kila kukiwa na lengo la kuzalisha Megawati 5000 hadi 6000 ifikapo 2025 na kuuza nje ya nchi.


Hayo yameelezwa Jijini Dodoma Februari 22,2023 na Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa Wateja kutoka TANESCO, Bwn Martin Mwambene. Wakati akizungumza na wanahabari kuhusu utekelezaji wa majukumu  ya Taasisi hiyo.

Mwambene amesema kuwa uwezo wa kutumia umeme nchini katika Megawati 1,820, ambapo sasa mitambo iliyopo inauwezo wa Megawati 1,300.


“TANESCO miradi miradi ambayo inaweza kuongeza kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa kila kuweka malengo ni mawazo Megawati 5,000 hadi 6000 ifikapo mwaka 2025,


“Kwasasa Mradi wa Umeme wa bwawa la Julius Nyerere upo asilimia 88 ambapo sasa hivi tumeanza mabadiliko maji ambayo yamefikia mita za ujazo 133 kutoka usawa wa bahari,


“Najua Wateja wamekua wakijiuliza TANESCO hawafikirii kutafuta njia mbadala lakini kama TANESCO tumefikiria kuwa na mbinu za miradi mbadala ambayo itaongeza uwezo wa kuweka umeme wa jua, pia kuna vyanzo vya ziada uwezo wa kuwa na viwanda viwanda".


Aidha amesema kuwa Miradi ya uwezo inaenda sambamba na miradi ya kusafirisha umeme, katika mradi wa JNHPP ambapo kuna njia ya kusafirisha umeme itakayoanzia Rufiji mpaka Chalinze na tayari transfoma kubwa takriban sita zimepelekwa zinasubiri kufungwa.


“Kuna baadhi ya mikoa inayohusisha Rukwa na Katavi haipo katika Gridi ya Taifa, hivyo kuna laini ambazo zitajengwa ambazo zitakuwa zinaunganisha nchi nyingine karibu nchi nzima itakuwa ipo katika mfumo wa Gridi ya Taifa"


Mwambene ameeleza kuwa utatekeleza mradi wa Gridi Imara utajumuisha ununuzi wa mashine umba 6,000, mita laki 7 za umeme, nguzo 380,000, ununuzi na ufungaji wa urefu wa KM 40,000, ujenzi wa vituo 14 vya kupoza umeme na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme mkubwa. takriban KM 948.


“Mradi huu wa Gridi Imara ni ushahidi kwamba matatizo ya umeme yaliyopo nchini tunayatarajia na tunatarajia mradi huu utayatatua"


Pamoja na hayo Mwambene amefafanua swali lililoulizwa na Mwandishi wa habari kuwa kumekuwepo na changamoto kwa wateja wapya wanaotaka kuwekewa umeme kutoa gharama za hadi tatu huku wengine wakipata urahisi wa kuunganisha umeme bila gharama za nguzo kupitia nguzo zilizonunuliwa na wateja wengine,


Ambapo Mwambene alijibu kuwa TANESCO haiuzi nguzo bali inauza huduma ya umeme hivyo kama mteja atatakiwa kuunganishiwa huduma ya umeme kwa kulipia nguzo basi atakuwa amelipia huduma ya umeme.

SERIKALI YATENGA BILIONI 6.4 MRADI WA ELIMU YA JUU KWA MAGEUZI YA KIUCHUMI.

 



 
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU), Prof.Charles Kihampa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo.

 

Na Deborah Lemmubi.

Kutoka Dodoma.


Serikali yatenga kiasi cha Shilingi Bilioni 6.4 kwa mwaka wa fedha 2022/23 kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (Higher Education for Economic Transformation-HEET) kwa ajili ya kuimarisha uthibiti ubora na uhuishaji wa mitaala ya vyuo vikuu Nchini.


Hayo yamesemwa Jijini Dodoma Februari 22,2023 na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU), Prof.Charles Kihampa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo.

Prof.Kihampa amesema kuwa kupitia mradi huo zaidi ya mitaala 300 ya vyuo vikuu iko katika hatua mbalimbali za kufanyiwa mapitio ili kuhuishwa kwa kuzingatia maoni ya wadau mbalimbali ili kukidhi matarajio yao na mahitaji ya soko.


“Katika kufanikisha hili, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, imeendelea kuandaa na kuratibu mafunzo ya kubadilishana uzoefu kwa viongozi na wanataaluma wa vyuo vikuu kuhusiana na uendeshaji wa vyuo vikuu, utengenezaji mitaala inayozingatia ujuzi na inayoendana na soko, mbinu za ufundishaji kwa wahadhiri ambao hawakusoma fani za ualimu, ulinganifu wa programu za masomo (programme benchmarks), uthibiti ubora, na utengenezaji na utumiaji wa mifumo ya kompyuta,


“Kwa mfano, katika kipindi cha  Julai hadi Desemba, 2022 jumla ya viongozi na wanataaluma 575 wameshanufaika na mafunzo hayo na Mafunzo hayo yamelipiwa na serikali kwa asilimia 100"


Prof.Kihampa amesema kutokana na hatua hizi zinazochukuliwa na Serikali, vyuo vikuu vimeweza kuimarisha mifumo yake ya uthibithi ubora na uendeshaji wa mafunzo pamoja na kuongezeka kwa fursa za masomo ya elimu ya juu na idadi ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya elimu ya juu nchini.


Akizungumzia mafanikio ya Tume hiyo Prof.Kihampa amesema kuwa mifumo ya uthibiti ubora, ushauri na usimamizi wa elimu inayotolewa na Vyuo Vikuu hapa nchini imeimarika.

“Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania imeendelea kuimarisha mifumo yake ya uthibiti ubora na mifumo ya ndani ya vyuo vikuu ili kuhakikisha vyuo vikuu vinaendana na mwelekeo wa nchi, ambapo Tanzania imelenga kuwa Taifa la watu wenye maarifa, ujuzi, weledi na uwezo wa kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wake ifikapo mwaka 2025 pamoja na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati unaochochewa na uwepo wa viwanda"


Pia amesema katika kuhakiki ubora, TCU imeimarisha mifumo yake ya ushauri na ukaguzi wa mara kwa mara, wa kawaida na wa kushtukiza kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo kwa lengo la kuhakikisha kuwa elimu itolewayo na vyuo vikuu hapa nchini inakidhi viwango vya ubora kitaifa, kikanda, na kimataifa. Kwa mfano, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Februari, 2023 vyuo vikuu vyote 47 vilivyopo vimekaguliwa na kupewa ushauri wa maeneo yanayohitaji kuboreshwa.


“Zoezi hili la ukaguzi wa vyuo ni endelevu kila mwaka. Vilevile TCU imeweka utaratibu wa kuanzishwa na kuimarishwa mifumo ya uthibiti ubora ndani ya vyuo vikuu ambapo vyuo vyenyewe vimekua na utaratibu wa kujikagua, kujitathmini na kufanya marekebisho mbalimbali kwa kuzingatia miongozo ya uendeshaji wa vyuo vikuu".


Ameeleza kuwa mifumo ya ushauri, ukaguzi, na ufuatiliaji wa mara kwa mara imefanya vyuo kufanya maboresho makubwa katika miundombinu ya kufundishia na kujifunzia ikiwa ni pamoja na ujenzi wa maabara za kisasa, mifumo ya mawasiliano ya kielektroniki, madarasa na kuongeza idadi ya viongozi na wahadhiri wenye sifa stahiki kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo iliyopo.

Thursday, 16 February 2023

MEJA JENERALI MBUGE: TUTAENDELEA KUJIPANGA KATIKA KUKABILANA NA MAAFA NCHINI

                    

Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Charles Mbuge akihutubia wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wadau cha kupitia na kujadili Rasimu ya Mpango wa Taifa wa Mawasiliano ya Dharura kilichofanyika tarehe 16 Februari, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya African Dream Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Charles Mbuge (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikao kazi cha kupitia na kujadili Rasimu ya Mpango wa Taifa wa Mawasiliano ya Dharura kilichofanyika tarehe 16 Februari, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya African Dream Jijini Dodoma mara baada ya ufunguzi wa kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa kikao kazi cha kujadili Rasimu ya Mapango wa Taifa wa Mawasiliano ya Dharura wakiwa katika kazi za vikundi wakiujadili mpango huo.

 

Kamishna Msaidizi wa Polisi Makao Makuu Dodoma ACP Simon Haule akichangia jambo wakati wa kikao hicho.

 

Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Charles Mbuge (katikati), Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa (Kituo cha Operesheni na Mawasilino ya Dharura) Bw. Prudence Constantino (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Mawasiliano ya Simu Wizara ya Habari, Mawasilino na Teknolojia ya Habari Mhandisi Edith Turuka wakifuatilia kikao hicho.

 


Mjumbe wa kikao cha wadau wa kupitia rasimu ya Mpango wa Taifa ya Mawasiliano ya Dharura Meja Lusajo Basyagile akichangia jambo wakati wa kikao hicho. 

 Mratibu wa Maafa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Yona Benjamin akiongoza kikao hicho.


Meneja Usimamizi wa Rasilimali za Mawasiliano na Tekinolojia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Felician Mwesigwa akiwasilisha rasimu ya Mpango wa Taifa ya Mawasiliano ya Dharura wakati wa kikao cha kuupitia mpango huo Jijini Dodoma.

 


NA. MWANDISHI WETU.

Kutoka Dodoma.


Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kuweka mikakati madhubuti katika masuala ya menejimenti ya maafa nchini ili kuhakikisha inapunguza madhara yatokanayo na maafa.


Kauli hiyo imetolea na Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Charles Mbuge wakati akifungua kikao kazi cha wadau cha kupitia na kujadili Rasimu ya Mpango wa Taifa wa Mawasiliano ya Dharura kilichofanyika tarehe 16 Februari, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya African Dream Jijini Dodoma.


Kikao kazi hicho kililenga kupitia na kujadili rasimu ya mpango huo wenye malengo ya  kusimamia mawasiliano na kuweka utaratibu wa matumizi ya huduma za mawasiliano ndani ya Serikali, Umma, Wadau wa Mawasiliano na Mashirika Binafsi.

 

Meja Jenerali Mbuge alisema, upo umuhimu wa kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na wadau wote wa masuala ya maafa nchini kwa lengo la kuhakikisha wanaendelea kuwa na mikakati madhubuti ya mawasilino wakati wa dharura.


“Hakikisheni kuwa mpango unazingatia Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022, Kanuni za Usimamizi wa Maafa za mwaka 2022 na Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano wakati wa Maafa 2022 ili kurahisisha utekelezaji wake,”alisisitiza Meja Jenerali Mbuge.


Akieleza kuhusu Mpango huo, alisema utarahisisha mawasilino ya haraka, sahihi na kwa wakati unaohitajika kwa kuzingatia mfumo huo uliojikita kidijiti na unahusisha vyombo vya habari ikiwemo matumizi ya radio, televisheni na mitandao ya kijamii.


Katika hatua nyingine Idara imeendelea kuchukua hatua za kupunguza madhara kwa kuhakikisha usimamizi na uratibu wa maafa na huduma za dharura zinatolewa kwa wakati kwa kuzingatia mipango, miongozo na mikakati ya kitaifa na kisekta. Juhudi hizi zimekuwa zikifanyika kwa kushirikiana na Wizara, Taasisi, Mashirika ya kimataifa na Asasi zisizo za kiserikali. 


“Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa ya Mwaka 2004 na Sheria ya Usimamizi wa Maafa, Na. 6 ya mwaka 2022 inajukumu la kuratibu na kusimamia masuala ya maafa nchini,”alisema. 


Idara ya maafa ilizindua nyaraka za usmamizi wa maafa nchini ikiwemo; Mkakati wa Taifa wa  Mawasiliano ya Dharura 2022 ambao umelenga kuhakikisha utendaji kazi, ushirikiano, na mwendelezo wa mawasiliano vinaimarika wakati wa maafa ili kuruhusu watoa huduma za dharura kufanya mawasiliano baina yao na ngazi nyingine za serikali wakati wote, hata pindi miundombinu ya mawasiliano itakapoharibiwa.  



Wednesday, 15 February 2023

WRRB YATOA WITO KWA MADALALI WA MAZAO KUACHA KUWARUBUNI WAKULIMA KATIKA UUZAJI WA MAZAO YAO.

 Mkrugenzi Mtendaji wa Bodi ya usimamizi wa Stakabadhi za ghalani  (WRRB) Asangye Bangu akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jijini Dodoma.


Na.Deborah Lemmubi.

Kutoka Dodoma


MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya usimamizi wa Stakabadhi za ghala (WRRB) Asangye Bangu ametoa wito kwa madalali kuacha tabia ya kuwarubuni wakulima na badala yake kuwaacha waingie kwenye mfumo wa Stakabadhi ghalani ili kuuza mazao yao kulingana na bei iliyopo sokoni.


Bangu ametoa Kauli hiyo ,wakati akielezea utekelezaji wa majukumu na shughuli mbalimbali za bodi hiyo mbele ya waandishi wa habari Februari 15,2023,Jijini Dodoma.


Ambapo amesema kuwa kumekuwa na wimbi la watu wanakwenda mashambani kwa wakulima na kuwadalalia mazao na kununua kwa bei ya chini kitu ambacho kinaendelea kudidimiza maendeleo ya wakulima.


"Natoa wito kwa madalali waache kuwarubuni wakulima wawaache wajiunge katika Mfumo wa Stakabadhi ghalani ili waweze kuuza mazao yao kwa bei ya ushindani iliyopo sokoni kwa kuendelea kuuza mazao shambani inaendelea kuwadidimiza wakulima kwa sababu madalali wengi wananunua mazao kwa bei ya chini tofauti kabisa na bei iliyopo kwenye mfumo"


Bangu amesema mafanikio yaliyopatikana baada ya kuanzishwa kwa Mfumo wa Stakabadhi za Ghalamni pamoja na ongezeko la bei za mazao, mapato ya mkulima na mapato ya Serikali kwa wastani wa asilimia 200% kutokana na urasimishaji, ongezeko la uzalishaji wa mazao kwa wastani wa asilimia 12% kwa mwaka,kichecheo cha ubora wa mazao yanayofikishwa sokoni,


Ametaja mafanikio mengine ni upatikanaji wa takwimu sahihi za mazao yanayopita kwenye Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, ongezeko la mapato ya uhakika kwa Serikali Kuu na Serikali Mitaa na kukuza huduma za fedha vijijini,kufanikisha uanzishaji wa Soko la Bidhaa Tanzania.


Aidha, Mkurugenzi huyo amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Mfumo 2007/08 hadi 2020/21 ukuaji wa uzalishaji umekuwa ukiongezeka kwa wastani wa 12% kwa mwaka ikilinganishwa na ukuaji wa 2% kwa mwaka kabla ya kuanzishwa kwa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala.


"Kwa mfano katika zao la Korosho mara baada ya kuanzishwa kwa Mfumo palikuwa na ongezeko la asilimia 164% la bei kutoka Ths 350.00 msimu wa 2006/07 hadi kufikia Tsh 925.00 msimu wa 2007/08 mwaka wa kuanza wa Mfumo; katika miaka minane tokea kuanzishwa kwa Mfumo 2007/08 hadi 2014/15 wastani wa ongezeko la bei kwa mwaka ulikuwa 25% kulinganisha na ongezeko la bei miaka minane kabla ya kuanzishwa kwa Mfumo la 12% kwa mwaka kaunzia mwaka 1998/99 hadi 2006/07"


Mkurugenzi huyo amesema kuwa ili kuendana na kasi ya ukuaji wa teknojia Bodi imekuwa ikishirikiana kwa karibu na kuhamasisha bodi ya TEHAMA kukamilisha mifumo mipya na kuhamishia huduma za Bodi hiyo kwenda kidijitali.


Aidha, Bodi imeendalea juhudi za kuboresha Mfumo uliokuwepo wa kizamani wa Usimamizi wa ghala, ambapo kushirikiana na Bodi ya TEHAMA inakuja na Mfumo mpya wenye kuweza kurahisisha kazi za

maandalizi ya taarifa, utoaji stakabadhi na udhibiti wa matukio ghalani hivyo kupunguza muda wa michakato na kuongeza ufanisi na usalama wa mzigo.


"Majaribio ya Mfumo wa Maombi ya Leseni Mtandaoni yamefanyika na mapendekezo ya maboresho yamepelekwa kwa programmers kwa ajili ya kufanyiwa kazi"


Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) ni taasisi chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara iliyoundwa kwa Sheria Namba 10 ya 2005 na Marekebisho Kifungu 4 Sura 339 R.E. 2016 iliyopewa majukumu chini ya Kifungu 5 (a-j) ikiwemo kutoa leseni kwa waendesha ghala, meneja dhamana na wagakuzi wa ghala; kuchapa and kuidhinisha vitabu vya Stakabadhi za Ghala, kusajili na kuingiza taarifa za wadau muhimu wa mfumo, kuwakilisha nchi katika masuala ya taifa na kimataifa yahusuyo Mfumo wa Stakabadhi za Ghala pamoja na majukumu mengine kama taasisi itakavyoelekezwa na Mhe. Waziri wa Viwanda na Biashara.

Tuesday, 14 February 2023

WATANZANIA WENGI HAWANA ELIMU YA KUTOSHA,YA FEDHA HASA YA MIKOPO.



 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Beng'i Issa akizungumza na Wanahabari Jijini Dodoma Februari 13,2023.


Na.Deborah Lemmubi.

Kutoka Dodoma

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Beng'i Issa amesema kuwa Watanzania wengi bado hawana elimu ya kutosha juu ya matumizi ya fedha itokanayo na mikopo na badala yake wanakopa na kutumia nje ya mipango waliyokusudia.

Ameyasema haya Jijini Dodoma, leo Februari 14,2023 wakati akizungumz na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Baraza hilo.

Aidha Beng’i ameeleza kuwa pamoja na Serikali kutoa fedha za mikopo kiasi cha shilingi Trilioni 5.6 kwa ajili ya kuwawezesha watanzania milioni 8 bado watanzania wengi wanakabiliwa nakutokua na elimu juu ya matumizi ya fedha na kumiliki fedha.

“Nataka kuwaeleza kuwa katika kipindi cha mwaka jana baraza kwa kushirikiana na serikali kwa ujumla wake wametoa kiasi cha sh.tirion 5 .6 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali wapatao milioni 8 jambo ambalo ni hatua kubwa katika kuwawezesha watanzania kujiinua kiuchumi”.

Kutokana na kutokuwepo kwa elimu ya kutosha juu ya matumizi ya fedha na kumiliki fedha amesema kuwa serikali kwa kushirikiana taasisi mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu juu ya matumizi ya fedha na kumiliki fedha.

“Tunaendelea kutoa elimu kwa watanzania ili kuhakikisha watanzania wanajikwamua katika maisha na kuishi maisha ambayo yatakuwa bora kila mmoja jambo ambalo litawafanya watanzania kuwa na amani na furaha”.

Pamoja na hayo Beng’i amewashauri watanzania kutopenda kujitumbukiza kwenye masuala ya mikopo kama hawajajipanga kwa kujua wanachotakiwa kukifanya.Aidha amewataka watanzania kuwa na nidhamu ya fedha sambamba na kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba benki.

Vilevile amezungumzia ufanisi wa baraza hilo ambapo amesema kuwa kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanawawezesha wananchi kupata fursa mbalimbali za kujikwamua kihuchumi .

Katika kutilia mkazo juu ya kuwawezesha wananchi ameeleza kuwa kwa sasa kuna mifuko mbalimbali ya kuwawezesha akina mama na vijana huku akieleza kuwa akina mama wamekuwa wakipewa kipaumbele zaidi kwa kuwa ni waaminifu katika kurejesha.

MARUFUKU KUTUMIKISHA WATOTO KWENYE MACHIMBO-MAJALIWA

Waziri mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Songwe Februari 13,2023.
 


Na.Mwandishi Wetu.

Kutoka songwe.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza Wakuu wa wilaya kwenye maeneo yenye shughuli za uchimbaji wa madini wahakikisha wanakemea vitendo vya ukatili dhidi ya watoto badala na yake watoto hao wapelekwe shule kwa ajili ya kupatiwa elimu.

 Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kuwatumikisha watoto katika maeneo ya machimbo ya madini na kuwanyima fursa watoto hao wa Kitanzania kupata haki yao ya msingi ya elimu.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Februari 13, 2023) wakati akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Songwe inayojengwa katika kata ya Mkwajuni akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Songwe.

Waziri Mkuu amesema viongozi wa machimbo ya madini katika maeneo mbalimbali nchini wafanye uhakiki wa watu wote wanaofanya kazi katika maeneo hayo na wahakikishe watoto wote walio kwenye umri wa kwenda shule wanapelekwa.


“Kumeibuka tatizo la ukatili wa kuwatumikisha na vitendo vya hovyo wanavyofanyiwa watoto wetu kwenye maeneo hayo fanyeni uchungu na kubaini wanaohusika na vitendo hivyo. Mkuu wa wilaya hakikisha unatokomeza ukatili kwa watoto na wanawake.”

“Viongozi katika mikoa yote nchini wachukulieni hatua wazazi wanaoshindwa kuwasimamia watoto wao kwenda shule. Wananchi shirikianeni kuhakikisha watoto wenye umri wa kwenda shule wanakwena shule, mtoto wa mwenzio ni wako.”

Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, Cecilia Kavishe ahakikishe ujenzi wa mradi wa hospitali hiyo ukamilika katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu na ifikapo Aprili ianze kutoa huduma.

“Katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hakuna mahali ambapo hapajaguswa na miradi ya maendeleo, kamilisheni ujenzi wa majengo haya ili wananchi wapate huduma karibu na makazi yao.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, Cecilia amesema mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo hiyo ambao umefikia asilimia 95 umegharimu shilingi bilioni 3.5 na unatarajiwa kukamilika Machi 31, 2023.

Amesema ujenzi wa hospitali hiyo unahusisha majengo ya huduma za wagonjwa wa nje, mionzi, maabara, wodi tatu za magonjwa mchanganyiko, famasia, utawala, mama na mtoto, huduma ya dharura, upasuaji, uchunguzi, jengo la kuhifadhia maiti na wodi mbili za upasuaji.

Naye, Mbunge wa jimbo la Songwe, Philipo Mulugo ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuridhia utoaji wa fedha ambazo zinatumika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo ikiwemo ya afya, maji na elimu.

Hata hivyo mbunge huyo ameiomba Serikali iwajengee kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Mbalizi-Changombe-Mkwajuni-Saza-Patamela-Makongorosi yenye urefu wa kilomita 118 ili kurahisisha usafiri wa watu na mizigo.

IFAD NA MAWAZIRI WA TANZANIA WAKUTANA ITALIA KUJADILI MAENDELEO YA UVUVI


Rais wa Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo duniani Mhe. Alvaro Lario wa IFAD akiwa na Viongozi waandamizi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Waziri wa mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki, Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe Mahmoud Thabiti Kombo na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia

 






Na.Mwandishi Wetu,

Kutoka Rome,Italia.


Mkutano wa Mfuko wa Maendeleo wa Kilimo na Uvuvi Duniani (IFAD) umeanza mapema jana Februari 13, 2023 ukihudhuriwa na Rais wa Mfuko huo, Alvaro Lario pamoja na Mawaziri wa Uvuvi kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ambapo wamejadili mambo mbalimbali juu ya sekta ya uvuvi.

Katika mkutano huo, viongozi hao waandamizi ni pamoja na Mawaziri wawili wa Uvuvi na Makatibu Wakuu wawili, wakiongozwa na Waziri wa Uvuvi Mashimba Ndaki sambamba na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Balozi Mahmmoud Thabiti Kombo ambaye pia ni Mwakilishi wa kudumu wa mfuko huo wa IFAD akiwakilisha Tanzania,

Miradi inayojadiliwa ni pamoja na miradi ya ujenzi wa meli za uvuvi, ujenzi wa masoko, majokofu ya baridi ya kuhifadhi samaki na mazao ya baharini ikiwemo mwani.

Wengine waliohudhuria mkutano huo ambao unatarajiwa kufikia mwisho Februati 16,2023, ni  moja na timu ya maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Italia wakiongozwa na Mwambata wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Misitu, Jaquiline Mhando.


SERIKALI YAFUNGUA MIPAKA KWA KAMPUNI CHANGA ZA TEHAMA.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Jimmy Yonazi akitia saini hati ya makubaliano baina ya Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia na kampuni ya Tanzania startups Association (TSA).

Na.Mwandishi Wetu

 Kutoka Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Jimmy Yonazi amesema Wizara itaendelea kushirikiana na kampuni changa za TEHAMA, kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya ufanyaji kazi pamoja na kuwafungulia masoko.


Dkt.Yonazi amesema kuwa kwa Kuwezesha  kampuni changa za TEHAMA kuwataftia Masoko Itasaidia kuongeza uchumi wa Taifa na kuongeza ajira kwa vijana ambao watapata fursa ya kuonesha bunifu zao katika sekta ya Teknolojia.



Hayo yameelezwa leo Februari 14,2023 jijini Dodoma  wakati wa hafla ya utiaji saini kati ya Wizara ya habari , mawasliano na Taknologia ya habari na Tanzania Startup's Association (TSA) , kwa ajili ya uanzishwaji na uimarishaji wa Miongozo mbalimbali inayosimamia bunifu na kampuni changa Nchini.


Aidha Dkt.Yonazi ametanabainisha kuwa Wizara hiyo ina Sera na sheria rafiki zinazowezesha makapuni machanga kufanya kazi zao kwa uhuru hivyo ujio wa (TSA) utasaidia kupeleka uchumi wa makampuni machanga mbele ndani na nje ya nchi.



"Serikali ipo tayari kushirikiana na kampuni hizi changa na lengo letu sio tu kwamba tunaongeza uchumi kwa makampuni na taifa ila lengo letu ni kulikomboa bara la Afrika kwa upande wa TEHAMA kwani kwa sasa soko la dunia limehamia upande wa digitali,"amesema Dkt.Yonazi



Vilevile Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Startups Association (TSA) Zahoro Muhaji amesema kuwa bara la Afrika linakabiliwa na changamoto kubwa ya ajira hivyo TSA imeona hilo na kwa sasa inaendelea kufungua fursa za ajira kupitia TEHAMA.


"Tumeanza safari nzuri ya kufanya kazi na Serikali kupitia Wizara hii Mama ya mawasiliano na ahadi yetu kubwa ni ushirikiano wa kutosha wenye tija kwa taifa letu na jamii kwa ujumla,"amesema Zahoro

SERIKALI KUTOA SHILINGI BILIONI 199 KUJENGA MINARA YA MAWASILIANO 1,087.

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko huo katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita leo Februari 13, 2023, jijini Dodoma.



Na.Deborah Lemmubi,

kutoka Dodoma.


 Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) kupitia Mtendaji wake Mkuu  Bi Justina Mashiba amesema Serikali imetoa ruzuku ya sh.bilioni 199 kwa ajili ya kuwezesha kampuni za mawasiliano kujenga minara ya mawasiliano 1,087 katika kata 1242 zenye vijiji 3654 wakazi 15,130,750.

Bi Justina ameeleza hayo Jijini hapa,leo Februari 13,2023 wakati akizungumza na  wanahabari kuhusu utekelezaji wa mradi huo ambapo amesema utaekeleza katika Minara 155 yenye vijiji 276 na wakazi 1,809,500 ili kurahisisha matumizi ya Mtandao.

Aidha Mashiba ameeleza kuwa kwa mfuko huo unafikisha mawasiliano kwa watanzania waishio vijijini wameona vyema kujenga minara hiyo na kukamilika kwa watanzania waishio vijijini watapata zaidi ya milioni 15 wataweza kupata mawasiliano ya mawasiliano kwa uhakika.

“UCSAF imeingia kufikisha huduma katika kata 1242 zenye vijiji 3,654,wakazi 15,130,250 minara 1087 yenye vijiji 3378 na wakazi 13320750 utekelezaji unaendelea katika minara 155 yenye jiji 276 na wakazi 1,809,500 na tayari Ruduru.


“Pia tayari ruzuku ya sh.bilioni 6.9 imeshatolewa katika mradi wa kimkakati wa Zanzibari ,ambapo minara 42 katika shehia 38.

Pia amesema kuwa mfuko huo umetekeleza mradi wa kupeleka vifaa vya tehama katika shule 811 na wastani wa shule upewa mwanzo 5,printa 1 na projekta 1.

Aidha amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 shule 150 zitafikishiwa vifaa vya tehama huku bajeti kwa mwaka ikiwa ni sh 1,950,000,000.

Pia amezungumzia utoaji wa elimu kwa walimu juu ya kuboreshaji wa matumizi ya TEHAMA ambapo mwaka 2016 mafunzo yalianza ambapo walimu 3,465 wamepatiwa mafunzo na walimu wapatao 3,139 wanatoka Tanzania bara na walimu 326 wanatoka Tanzania Zanzibar.

Hata hivyo UCSAF imeeleza kuwa katika mkakati wa kutafuta kila mtanzania anatumia huduma ya tehama wameanzisha mpango wa kufungua mitandao ya WiFi katika sehemu za wazi kama vyuo vikuu,mahosipitali pamoja na kwenye masoko ili kila mtanzania aweze kutumia mtandao nakupata huduma kwa wepesi.

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...