mwambelablog

Tuesday, 14 February 2023

SERIKALI YAFUNGUA MIPAKA KWA KAMPUNI CHANGA ZA TEHAMA.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Jimmy Yonazi akitia saini hati ya makubaliano baina ya Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia na kampuni ya Tanzania startups Association (TSA).

Na.Mwandishi Wetu

 Kutoka Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Jimmy Yonazi amesema Wizara itaendelea kushirikiana na kampuni changa za TEHAMA, kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya ufanyaji kazi pamoja na kuwafungulia masoko.


Dkt.Yonazi amesema kuwa kwa Kuwezesha  kampuni changa za TEHAMA kuwataftia Masoko Itasaidia kuongeza uchumi wa Taifa na kuongeza ajira kwa vijana ambao watapata fursa ya kuonesha bunifu zao katika sekta ya Teknolojia.



Hayo yameelezwa leo Februari 14,2023 jijini Dodoma  wakati wa hafla ya utiaji saini kati ya Wizara ya habari , mawasliano na Taknologia ya habari na Tanzania Startup's Association (TSA) , kwa ajili ya uanzishwaji na uimarishaji wa Miongozo mbalimbali inayosimamia bunifu na kampuni changa Nchini.


Aidha Dkt.Yonazi ametanabainisha kuwa Wizara hiyo ina Sera na sheria rafiki zinazowezesha makapuni machanga kufanya kazi zao kwa uhuru hivyo ujio wa (TSA) utasaidia kupeleka uchumi wa makampuni machanga mbele ndani na nje ya nchi.



"Serikali ipo tayari kushirikiana na kampuni hizi changa na lengo letu sio tu kwamba tunaongeza uchumi kwa makampuni na taifa ila lengo letu ni kulikomboa bara la Afrika kwa upande wa TEHAMA kwani kwa sasa soko la dunia limehamia upande wa digitali,"amesema Dkt.Yonazi



Vilevile Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Startups Association (TSA) Zahoro Muhaji amesema kuwa bara la Afrika linakabiliwa na changamoto kubwa ya ajira hivyo TSA imeona hilo na kwa sasa inaendelea kufungua fursa za ajira kupitia TEHAMA.


"Tumeanza safari nzuri ya kufanya kazi na Serikali kupitia Wizara hii Mama ya mawasiliano na ahadi yetu kubwa ni ushirikiano wa kutosha wenye tija kwa taifa letu na jamii kwa ujumla,"amesema Zahoro

No comments:

Post a Comment

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...