mwambelablog

Monday, 2 January 2023

POLISI WALAANI VITENDO VYA KIKATILI KWA WATOTO


Na Elizaberth Paulo,

Dodoma


Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limetoa rai kwa wazazi na jamii kwa ujumla kuwalea watoto katika malezi mazuri na maadili mema ili kuwa na Viongozi wazuri wa Taifa hapo baadae.


Hayo yamejiri juzi katika kampeni ya TULE NA TUNYWE NA WAHITAJI iliyofanyika Chigongwe family lililoandaliwa na Manyunyu foundation ikihudhuriwa na wadau wengine wakiwemo Wawakilishi wa Jeshi la Polisi.

SP.Dkt.Ezekiel D.Kyogo Alisema Jeshi la Polisi linajenga uhusiano na jamii ndo maana wamefika Kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya pamoja na watoto hao wenye uhitaji.


“Nitoe rai kwa wazazi kwamba wewe kama umekaa ukapanga kuona unamleta mtoto duniani basi uwe unawajibu wa kumuangalia, Yaani fikiri kuwa unamleta duniani na baadae unamwacha mtaani watu wengine wakulelee hiki ni kitendo kibaya kabisa”. Alitoa rai Kyogo


Alisema ili kutatua changamoto changamoto zinazojitokeza katika jamii zikiwemo za watoto wa mtaani au makundi mengine ya jamii lazima kuwepo na ushirikiano baina ya Polisi na jamii kwani Jeshi la Polisi haliwezi kutatua changamoto hizo pasipo ushirikiano na jamii.


Aidha alisema jeshi la polisi Linapobaini mzazi amemtelekeza mtoto mtaani kwa makusudi mpaka watu wa taasisi mbalimbali wamewachukua na kuwahifadhi lazima hatua kali Zitachukuliwa dhidi yake.


“Nitoe agizo lingine kwa wale kwa wale familia ambazo zinageuka kuwafanyia vitendo vya kikatili watoto ndani ya nyumba kiasi kwamba mtoto kwenye familia anaona hawezi kuishi anaona kero hivyo jamii ifumbue macho kwapamoja ukimuona mtoto wa jirani anafanyiwa vitendo viovu tutoe taarifa katika vituo vya polisi”Aliagiza 


ASP. Manase Dotto kamisheni ya polisi jamii makao makuu Dodoma Amewaasa watoto hao kuishi kwa kupemdana na kutoa taarifa kwa Viongozi wao pale Wanapoona wanatendewa vitendo viovu.


Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya watoto wengine Paulo Charles Lusinde Alisema wanafarijika sana wanapotembelewa na kasema kituo kinawalea vizuri na kuwafunza kilimo mbalimbali hata ufugaji wa samaki na mafunzo mengine, Pia ameiomba Jeshi la polisi kuchukua hatua kwa wale wote wanaotekeleza vitendo viovu kwa watoto kwani wakati mwingine hata polisi wamekuwa wakiwapiga watoto wakiwa mitaani.

No comments:

Post a Comment

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...