mwambelablog

Monday, 2 January 2023

MABORESHO YA BANDARI KUONGEZA MAPATO YA SERIKALI


mwandishi wetu Irene Atibu

Kutoka Tanga...



 Maboresho ya Bandari ya  Tanga yanayofanywa na serikali  yanatarajiwa kuongeza uwezo wa Bandari ya Tanga kupokea mizigo kutoka Tangi 750,000 kwa mwaka hadi tani 3 milioni.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Bandari Masoud Mrisha wakati akizungumza na waandishi wa habari za uchumi na biashara wanawake.



alisema kutoka na maboresho hayo mapato ya serikali na ajira zimeanza kuongezeka.

Naye  meya wa Jiji la Tanga Abdulraman Shiloo alisema upanuzi huo pia unatarajia kuongeza  mapato kwa jiji la Tanga.

Amesema maboresho hayo yamesababisha kuongezeka kwa shehena za mizigo jambo lililochangia upatikanaji wa mapato ambayo sehemu ya mapato hayo yamewezesha upatikanaji fedha katika jiji.

" Tunashukuru maboresho haya yametupatia pesa ambayo ni sehemu ya asilimia kumi ya  mapato ya Halmashauri na pesa hiyo tumeikopesha kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.

Akizungumza na wanahabari hao mmoja wa wanufaika wa upanuzi wa mradi huo Bi Mwanaidi Salim amepongeza na kushukuru kwa kupata ajira ya muda katika mradi kwani umemuwezesha kujiongezea kipato katika familia  kwa kusaidiana na mwenzi wao katika kutekeleza majukumu  ya familia Kama kulipa Kodi na kununua mahitaji ya shule kwa watoto wake.

  Mwanaidi Salimu aliongezea kwa kusema dhana ya kwamba wanawake wa Tanga ni wavivu haipo tena kwani kwa Sasa wanawake wanafanya kazi.


No comments:

Post a Comment

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...