Na Deborah Lemmubi - Dodoma.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetoa wito kwa Wananchi wote kufika katika Ofisi zao zilizopo Mtaa wa Njedengwa Jijini Dodoma ili kuweza kupata Elimu ya mpiga kura sambamba na kupata ufafanuzi juu ya maswali yanayowatatiza.
Wito huu umetolewa na Bi Rose Chilongozi ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Huduma za Sheria akiwa katika maonesho ya wiki ya utoaji wa Elimu ya Sheria yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square Jijini yenye kauli mbiu inayosema: Umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya Usuluhishi,katika kukuza Uchumi Endelevu,Wajibu wa Mahakama na Wadau.
Na kuongeza kuwa,Wananchi wajitokeze pia katika zoezi la uboreshaji Daftari la Mpiga kura ambalo litatangazwa na kuanza siku za hivi karibuni.
"Mimi wito wangu tunawakaribisha wananchi wote katika Ofisi zetu zilizopo Njedengwa,wafike waweze kupata elimu ya mpiga kura na kupata ufafanuzi juu maswali yanayowatatiza wasibaki kujiuliza tu huko pembeni, pia niwaombe wajitokeze katika zoezi la uboreshaji wa daftari la mpira kura mara tutakapo tangaza kuanza kwa zoezi".
Na kuongeza kuwa,kwa wale ambao hawataweza kufika Ofisini kwao wanaweza kupata Elimu na Ufafanuzi kwa kupiga simu au kutuma maswali yao kwa barua pepe na wao wata wapatia majibu kwani wamekuwa wakifanya hivyo pia.
Aidha Bi Rose ameeleza lengo la wao kuwepo katika maonesho haya ya wiki ya sheria kuwa ni kuujulisha Umma kuwa TUME ipo inafanyakazi na imesajiliwa Kisheria.
"Lengo la sisi kuwa hapa katika maonesho haya ni kutaka kuujulisha Umma kuwa TUME ipo,inafanya kazi na Imesajiliwa Kisheria hivyo watu waje kwaajili ya kupata Elimu".
Sambamba na hayo Bi Rose ameainisha shughuli zinazofanywa na TUME kwa kipindi cha kabla ya Uchaguzi,wakati wa Uchaguzi na baada ya Uchaguzi ambapo amesema mojawapo ni Uandaaji wa Bajeji,Marekebisho ya Sheria,Kanuni na Maelekezo,hivyo TUME iko kazini muda wote yani kwa hiyo mizunguko mitatu ya kabla,wakati na baada ya Uchaguzi.
"TUME inafanya shughuli zake kwa mizunguko mitatu yani kabla Uchaguzi,wakati wa Uchaguzi na baada ya Uchaguzi ikiwemo Uandaaji wa Bajeti,Uandaaji wa Kalenda ya Uchaguzi na mpango wa ufuatiliaji,Utoaji wa habari na elimu ya mpiga kura na Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura"
Mbali na hayo yote pia yapo Majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia matakwa ya ibara ya 74(6) na 78 katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 zikisomwa pamoja na kifungu cha 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na kifungu cha 86A cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa,Sura 292,moja ya Majuku ya Tume ni Kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika Uchaguzi Raisi na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano.