mwambelablog

Monday, 7 November 2022

WAANDISHI WA HABARI TOENI ELIMU YA UVIKO_19 KWA JAMII

 


Na Deborah  Lemmubi - Dodoma.


Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma wameombwa kuendelea kutoa elimu na hamasa juu ya umuhimu wa chanjo ya Uviko - 19 ili jamii kuondokana na imani potofu juu ya chanjo hii.


Ombi hilo limetolewa na Afisa Afya kutoka Ofisi ya Daktari wa Jiji Bwn Thobias Kigwinya wakati akitoa mafunzo ya kuwajengea uelewa Wanahabari Mkoa wa Dodoma namna ya kuripoti magonjwa ya mlipuko hasa Uviko - 19 yaliyoandaliwa na Taasisi ya Internews chini ya Mradi wa Boresha Habari yaliyofanyika Jijini Dodoma.


"Hapa niseme kuwa wananchi wanatakiwa kujua ni muhimu kupata chanjo ya Uviko 19 na hili linaweza kufanikiwa kupitia kwenu Wanahabari"


Aidha Bwn Kigwinya amesema kuwa chanjo haina madhara kama baadhi ya watu wanavyodhani ila kilichoharibu ni kutokana na ile imani ya kila mtu.


" bado kuna baadhi ya jamii ina imani potofu juu ya chanjo ya Uviko 19 kutokana na suala la imani zao, hivyo chanjo haina madhara kilichoharibu ni kutokana na imani ya kila mtu"


"Na kuongeza kuwa,chanjo sio kwamba inakukinga moja kwa moja ila inakupunguzia madhara mara upatapo Uviko 19 tofauti na mtu ambaye hajachanja"


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na mjumbe Bodi ya umoja klabu za Waandishi wa Habari Tanzania, ambaye pia ni mmoja wa wawezeshaji katika mafunzo haya Bwn Mussa Yusuph akizungumzia suala la maadili ya Uandishi wa habari magonjwa ya mlipuko hasa Uviko 19 amesema Mwandishi ni vema kuzingatia Uadilifu,Usahihi wa taarifa,Usiri wa vyanzo taarifa kama havikutaka kutajwa na kutotumia lugha zenye utata.


"Ukiwa Mwandishi wa Habari ili uripoti vizuri habari zako ni vema kuepuka mihemko binafsi, kuzingatia matumizi ya lugha iwe inayoeleka,Usiri,ujue hadhira inahitaji nini na Utoshelevu wa takwimu"


"Unakuta watu hawana uelewa kuhusu chanjo unaandika kichwa cha habari,wananchi wagomea chanjo badala ya kuandika,wananchi wahitaji elimu kuhusu chanjo. Hivyo ni vema kuzingatia Maadili ya Uandishi wa Habari"


Pia baadhi ya wawezeshaji wa chanjo ya Uviko 19 ambao nao ni waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma Bilson Vedastus na Bahati Msanjla wao wamesema ni vizuri kama mwandishi kutumia vyanzo vinavyoaminika katika habari za magonjwa ya mlipuko ili kutozua taharuki katika jamii.


"Katika suala la uandishi unapoandika habari za Uviko 19 na magonjwa ya mlipuko jitahidi sana kuangalia vyanzo vya kuaminika mfano: tovuti ya Wizara ya Afya,pia ni muhimu kuangali mambo kwa kina" Bilson.


"Ni muhimu kuepuka lugha za kuogofya na kuzingatia maudhui na panahitaji kuwepo kwa mjadala wa kuwajengea uelewa wananchi" Msanjila.

No comments:

Post a Comment

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...