Na Deborah Lemmubi -Dodoma.
Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini linalojishughulisha na Upingaji wa Ukatili wa kijinsia na Mimba za utotoni lililopo Jijini Mwanza Bwn Yassin Ally amesema kiwango kikubwa cha utekelezaji wa familia,Malezi na Migogoro ya ndoa ni sababu inayochangia uwepo wa kiwango kikubwa cha ukatili wa kijinsia,Mimba na Ndoa za utotoni kwa Mikoa ya kanda ya ziwa.
Bwan Yassin ameyasema hayo Jijini Dodoma katika Mkutano wa Kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Sekretarieti za Mikoa na wakuu wa Idara za Maendeleo ya jamii kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara na Uzinduzi wa Mwongozo wa Majadiliano ya Mila na Desturi.
Aidha amesema Takwimu zinaonesha kuwa Mikoa ya Kanda ya ziwa inaongoza kwa kiwango kikubwa cha ukatili wa kijinsia kutokana na tawimu za Taasisi ya Takwimu ya Taifa za mwaka 2015/2016.
"Ukichukua takwimu za Taasisi ya Takwimu ya Taifa ( Tanzania Demographical Health Survey ) ambazo tunazo mpaka sasa za mwaka 2015/2016 zinaonesha Mikoa ya kanda ya ziwa inaongoza kwa kiwango kikubwa cha ukatili ambapo mkoa wa Mara na Shinyanga inaongoza kwa asilimia 78,lakini utaona pia Mkoa wa Mwanza una asilimia 60,Kigoma asilimia 61 kwahiyo utaona mikoa hii yote. Lakini utaona pia Shinyanga inaongoza kwa mimba za utotoni, ndoa za utotoni asilimia 59 na Mwanza mimba za utotoni ni asilimia 28 hivyo utaona vitu hivi vina uhusiano"
Pia amesema Shirika la Kivulini wanacho fanya kwa sasa ni kuwajengea uwezo wanafunzi katika klabu zao kwa shule za msingi na sekondari ili kuwa na stadi za malez,kujitambua na kujilinda kutokana na kiwango kikubwa cha ndoa za utotoni na ukatili wa ulawiti kwa watoto wa kiume.
"Ambacho tumekifanya kwanza tumejenga uwezo kwa klabu za wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili kuwapa stadi za malezi,stadi za kujitambua na stadi za kujilinda kwasababu mikoa hii ina kiwango kikubwa cha ndoa na mimba za utotoni na ukatili"
"Na kuongeza kuwa ,lakini pia tumeshuhudia tukiwa tumewekeza nguvu kubwa kwa watoto wakike lakini wimbi la ulawiti kwa watoto wa kiume limekuwa na tatizo kubwa.
Ameongeza kuwa wanatoa elimu ili kuondokana na mfumo dume hasa kwa wanaume wanaoshindwa kuhudumia watoto kwa vifaa vya shule kama penseli na madaftari kwa kwenda kwenye starehe mara wanapopata mavuno,bila kujua mambo haya huleta athali kubwa.
Jina la Kivulini ambalo ni la Shirika pia, limebeba mikakati ya utatuzi wa changaomoto za ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto hata chini ya kivuli cha mti.
No comments:
Post a Comment