Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Sukari Tanzania,Prof.Kenneth Bengesi akizungumza Leo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo Pichani) Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Bodi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 Kutoka Dodoma |
SERIKALI kupitia Bodi ya Sukari Tanzania imesema kuwa Nchi haitakuwa na uhaba wa sukari katika kipindi Cha Miaka miwili ijayo ambapo uzalishaji utaongezeka kutoka Tani 380,000 za Sasa hadi kufikia Tani 756,000 ifikipo Mwaka 2025/2026.
Uhaba huo wa Sukari utaisha katika kipindi hicho kutokana na Mikakati mbalimbali iliyowekwa na bodi hiyo ya kuongeza viwanda vya ndani.
Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Sukari Tanzania,Prof.Kenneth Bengesi ameyaeleza hayo Leo mbele ya Waandishi wa Habari Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Bodi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.
Prof.Bengesi amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia suluhu hassan imedhamiria kuongeza uzalishaji wa sukari nchini kwa kujenga viwanda vingi ili kuongeza ajira kwa Watanzania.
Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa kwa sasa Serikali inatumia fedha nyingi kuagiza sukari kutoka nje ya nchi ambapo serikali inatumia zaidi ya dolla million 150 ambazo ni zaidi ya billion 300.
"Serikali inatumia zaidi ya dolla million 150 ambazo ni zaidi ya billion 300 kuagiza sukari nje ya nchi jambo ambalo linawezekana kuzuilika endapo tutadhamiria kwa pamoja kuongeza uzalishaji wa sukari nchini kwa kujenga viwanda vingi jambo ambalo pia litaongeza ajira kwa Watanzania,"Amesema Prof.Bengesi
Na kuongeza kuwa "sisi kama chombo cha udhibiti chenye ufanisi na kinachoweza kuhudumia na kusaidia tasnia ya sukari kufikia ushindani na uendelevu unaotakiwa tuna jukumu la kuisaidia serikali kupunguza gharama za uagizaji wa Sukari kutoka nje na ili tufanikiwe ni lazima tuwekeze kwenye ujenzi wa viwanda,"Prof.Bengesi
Bodi ya Sukari Tanzania kwa kuongozwa na kanuni za kutoa huduma kwa usawa, huduma bora na uadilifu, inalenga kuunda, kudumisha na kudhibiti mazingira ambayo yanawafaa wawekezaji wa sukari kuzalisha miwa, sukari na bidhaa zinazohusiana kwa ufanisi na kwa faida.
No comments:
Post a Comment