Na. Andrew Chale
Bagamoyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Philip Mpango ameagiza Makumbusho ya Taifa kukusanya Ala za Muziki za mikoa yote hapa Nchini ili ziweze kuhifadhiwa kulinda tamaduni za Mtanzania.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt.Mpango ametoa kauli hiyo Novemba 11, 2022 wakati akizindua Tamasha la 41 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni linalofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Mkoani Pwani.
Ambapo ametembelea Banda la Makumbusho ya Taifa ambao wanashiriki tamasha hilo kwa kuonesha Ala mbali mbali za muziki za baadhi ya makabila ya hapa Nchini,
Pia maonesho ya picha jongefu za kale katika masuala ya Sanaa na Utamaduni,
Makamu wa Rais Mhe. Dkt.Mpango pia amepatiwa maelezo namna Makumbusho hiyo inavyofanya kazi zake kwa ukaribu na Wasanii.
Hata hivyo, akatoa agizo hilo, la kukusanya Ala za muziki kwa kila mkoa na hata kuvihifadhi kwani baadhi upotea kutokana na ukuaji wa teknolojia,
Makamu wa Rais Mhe Dkt.Philip ametaka Ala hizo zikipatikana zihifadhiwe angalau ziweze kukaa miaka 200, ili vizazi vijavyo wavijue na kuona umuhimu wa Ala hizo za Muziki wa Tanzania.
Baadhi ya Ala hizo za muziki ambazo zipo hapo ni Zeze, Ngoma, Marimba, manyanga na zingine nyingi.
No comments:
Post a Comment