Pichani:Ni Mtendaji Mkuu wa shule ya Vipaji ya Fountain Gate academy Bwana Thabiti Kandoro wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma.
Na Deborah Lemmubi - Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Hassan Abbas anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika Siku maalum ya Timu ya Wanawake ya Fountain Gate Accademy itakayofanyika tarehe 27/11/2022 inajuyojulikana kama a Princess Day.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa shule ya Vipaji ya Fountain Gate Bwana Thabiti Kandoro wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu siku hiyo maalum ya Timu ya Wanawake.
Aidha Bwana Kandoro amesema katika kusherehekea siku hiyo wameialika Timu kutoka Nchini Uganda ya Lady Dovu na imethibitisha kushiriki, pia kutakuwa na uzinduzi wa Jezi,kutambulisha malengo ya Msimu,Maendeleo na kutambulisha Wachezaji wa Timu ya Wanawake Fountain Gate kwa msimu wa 2022/2023.
Pia Kandoro amesema Fountain Gate kwa sasa inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi kuu ya wanawake [WPL] haya ni mafanikio makubwa wanayojivunia kutoka kwa vijana hawa wa shule yao.
Sambamba na hilo Kandoro amesema Pamoja na mambo mengine kituo hicho wamepokea watoto zaidi ya mia moja kutoka Mikoa mbalimbali Kwa ajili ya kuwapatia Elimu na kuwaendeleza vipaji vyao walivyonayo vya mpira.
Katika kuendelea na maandalizi ya kuadhimisha ya siku hiyo Timu ya Fourntain Gate na Uongozi mzima watatembelea watu wenye mahitaji maalum kama vile Vituo vya Wazee,Vituo vya kulelea Watoto,Hospital na Nyumba za kuwatunza watu walioathirika na Dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment