mwambelablog

Thursday, 3 November 2022

DC KALAMBO,MH.TANO MWERA AISHUKURU BENKI YA NMB KWA MSAADA WA MABATI

          Caption:
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mhe. Tano Mwera akiwa katika mkutano na Wananchi (hawapo pichani) wakati alipotembelea ukarabati wa Zahanati ya Kapozwa, ambayo benki ya NMB wamechanga mabati 600.

             Caption:

Muonekano wa jengo la Zahanati ya Kapozwa lililoezuliwa paa zake na upepo mkali hivi karibuni.


Kutoka Kalambo.

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo (DC), Mh.Tano Mwera ameishukuru benki ya NMB kwa msaada wa mabati 600 yaliyotolewa kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya  Zahanati Wilayani hapa.


Mhe. Tano Mwera ametoa shukrani hizo wakati alipotembelea ukarabati wa Zahanati ya Kijiji cha Kapozwa ambapo shughuli za ujenzi zinaendelea.


Amabapo amebainisha kuwa, alifika Kijijini hapo siku za nyuma katika ziara zake za kawaida za kutembelea Vijiji hivyo ndipo alipata kero hiyo ya Zahanati kuezuliwa paa na kwa upepo mkali.


"Nilifika hapa na kuchukua kero hii, na kuomba msaada kwa Benki ya NMB, NMB Wakapokea kilio hicho na kutoa msaada wa Mabati 600.


"Pamoja na Zahanati hiyo kukarabatiwa, bati hizo pia zitatumika kukarabati Zahanati za Vijiji vya Mambwekenye na Mpanga...Kazi Iendelee" Alisema Mkuu wa Wilaya, Mhe. Tano Mwera.


Aidha, Mhe.Tano Mwera amebainisha kuwa,  Serikali inatambua changamoto mbali mbali hivyo wataendelea kuzitatua kwa nguvu zote ikiwemo kushirikiana na wadau wa sekta binafsi ikiwemo Benki hiyo ya NMB na wadau wengine katika kusaidia utendaji bora wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



No comments:

Post a Comment

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...