Kutoka kulia ni Mkurugezi wa Utafiti AREEN, Mha Evalio Mushimantwari Mkaguzi Mkuu wa masuala ya nishati Innocent Girukwishaka na Mkurugezi Mkuu wa AREEN Balthazar Nganikiye, Mkurugezi wa Petroli EWURA, Bw.Gerald Maganga ,Meneja Uchambuzi wa Mahesabu EWURA Bw. Msafiri Mtepa na Msaidizi wa Mkurugezi Mkuu EWURA, Bi Hawa Lweno wakati wakiagana na watendaji kutoka AREEN (Burundi) leo 13 Aprili 2023,makao makuu ya EWURA jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA ( wa tatu kutoka kulia) Dkt James Andilile katika picha ya pamoja na Mkurugezi Mkuu wa AREEN, Bw. Balthazar Nganikiye ( kushoto), Mkaguzi Mkuu wa masuala ya Nishati, Innocent Girukwishaka na Mkurugezi wa Utafiti wa AREEN,Mha Evalio Mushimantwari (kulia) mara baada ya ujumbe huo kuwasili makao makuu ya EWURA kilichofanyika Leo 13 Aprili 2023 jijini Dodoma.
Na.Mwandishi Wetu-DODOMA
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo 13 Aprili 2023, imepokea watendaji kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Sekta za Maji na Nishati Burundi (AREEN) kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwenye udhibiti.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt. James Andilie, wakati akiwakaribisha makao makuu ya EWURA jinini Dodoma, watendaji kutoka AREEN, alieleza kwamba, ni desturi ya EWURA kushirikiana na taasisi mbalimbali kwenye masuala ya udhibiti.
“Tumefarijika kuwapokea wenzetu kutoka Burundi kubadilishana uzoefu kwenye utendaji, hii imekuwa desturi yetu na tupo tayari wakati wote kutoa ushirikiano wa hali ya juu” alisistiza Dkt Andilile.
Mkurugenzi Mkuu wa AREEN; Bwana Balthazar Nganikiye ameishukuru EWURA kwa utayari wake wa ushirikiano na kueleza kuwa anajivunia kushirikiana na EWURA.
“Ni dhahiri kwamba, tumekuwa tukijifunza mengi kwa EWURA, hata kanuni tunayotumia kupanga bei, tulijifunza hapa” Amesisitiza Bw.Nganikiye.
Pamoja na mambo mengine, masuala yaliyojadiliwa kati ya EWURA na AREEN ni mfumo wa udhibiti wa sekta ya petroli na ukokotoaji wa bei za bidhaa za mafuta nchini.
Ujumbe kutoka Burundi umejumuisha Mkurugenzi Mkuu wa AREEN, Bw.Balthazar Nganikiye, Mkurugenzi wa Utafiti Mha. Evelio Mushimantwari na Mkaguzi Mkuu wa Nishati na Madini, Bwana Innocent Girukwishaka.
No comments:
Post a Comment