Na Deborah Lemmubi - Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii na Mwenyekiti Kamati ya Kutangaza Tanzania Royal Tour Dkt.Hassan Abbasi amesema mapato ya utalii yameongezeka maradufu kutokana na watalii kuongezeka nchini ikiwa ni matunda ya Royal Tour, ambapo mapato ya jumla ya sekta ya utalii yameongezeka kutoka Trilioni 3.01 mwaka 2021 hadi Trilioni 5.82 na kuifanyaTANAPA na NCAA kuvunja rekodi ya mapato.
Dkt Abbasi ametoa Takwimu hizo Aprili 28,2023 Jijini Dodoma wakati akielezea mafanikio kumi ya mwaka mmoja tangu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alipozindua filamu ya Royal Tour jijini Arusha na hatimaye watanzania wengi kuiona kwa mara ya kwanza filamu ya “TANZANIA; THE ROYAL TOUR"
Aidha ameeleza jinsi ROYAL TOUR ilivyojenga hamasa kwa watalii na wawekezaji, sasa hamasa hiyo pia imekuwa na manufaa kwa sekta ya usafiri wa Anga kama takwimu za Manufaa kwa Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro pekee kama sampuli ya ndege za Kimataifa Zaongeza Ruti Tanzania Miruko ya jumla ya ndege za kimataifa KIA iliongezeka kwa asilimia 28 kutoka miruko 6,115 April 2021 hadi 7,850 April, 2023.
"kutokana na watalii kuongezeka nchini ikiwa ni matunda ya Royal Tour, mapato ya jumla ya sekta hii yameongezeka kutoka Dola za Marekani 1.310.34 (Sawa na TZS Trilioni 3.01) mwaka 2021 hadi Dola za Marekani,527.77 (sawa la TZS Trilioni 5.82) imefanya Tanapa na NCAA wamevunja rekodi ya mapato".
Dkt Abbasi Amesema Royal Tour sio mwisho ni mwanzo wa kuitangaza nchi kimataifa zaidi hivyo Kamati ya mwaka mmoja sasa, imepokea na inaendelea kuchambua “Royal Tours” nyingine zijazo na Maombi Kujitangaza Ligi Kubwa za Ulaya na Marekani Kutokana na hamasa ya Royal Tour klabu mbalimbali za Ligi Kubwa Duniani hasa Uingereza, Hispania na Marekani wapo katika mazungumzo nazo na wameshapokea ofa zao
Ushiriki wa Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika filamu ya Royal Tour umeleta mafanikio ambapo Novemba mwaka jana huko Dallas,Texas, USA, Taasisi ya Tuzo za Afrimma ilimtangaza Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Rais Mwanamke wa kwanza Afrika Kushinda Tuzo ya Mageuzi Katika Uongozi wakitamka bayana kuwa mojawapo ya vigezo na mafanikio ni ushiriki wake katika Royal Tour".
Mpaka kufikia Sasa kuna wastani wa takribani watu Bilioni 1.2 wamejihusisha na Royal Tour iwe ni kwa kuona,kusikia,kuangalia au kuambiwa na mtu mwingine habari za Makala hii ya Royal Tour.