mwambelablog

Tuesday, 14 February 2023

NCC YAENDELEA KURATIBU UTATUZI WA MIRADI NCHINI.

 

Mtendaji Mkuu Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Dkt Matiko Mturi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Na Deborah Lemmubi -Dodoma.

Kutoka Dodoma.


Mtendaji Mkuu Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Dkt Matiko Mturi amesema kuwa Baraza limeendelea kuratibu utatuzi wa miradi ya ujenzi ambapo jumla ya mashauri 6 yametolewa huku mengine 31 yakiwa katika hatua mbalimbali za utatuzi.


Ameyasema hayo Jijini Dodoma, leo Februari 13,2023 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya baraza hilo kwa mwaka wa fedha 2022/2023.


Dkt.Mturi amesema kuwa wanatatua kumaliza migogoro hiyo ikiwa ni sehemu ya majukumu kama baraza linaloshughulika na sekta ya ujenzi.


“Baraza la Taifa la ujenzi linatoa huduma mbalimbali kwa wadau wa sekta ya ujenzi ikiwa ni pamoja na sekta,ushauri wa masuala yanayohusu sekta ya ujenzi,usuluhishi katika sekta ya ujenzi.


“Kutoa mafunzo kwa wadau wa sekta ya ujenzi, ukaguzi wa miradi ya ujenzi,utafiti,ukusanyaji,u waandishi wa habari za sekta ya ujenzi na miongozo mbalimbali ya gharama za ujenzi nchini"


Dkt.Mturi ameeleza kuwa kutokana na majukumu hayo wanayoshulika nayo katika kipindi cha Julai 1,2022 hadi Januari 31, 2023 NCC imetekeleza majukumu ya kupanga mipango ya gharama ya gharama za msingi za ujenzi wa barabara kwa kila mkoa wa Tanzania Bara na wasiwasi katika. kikao cha wadau wa ndani ya serikali ili kupata maoni na ushauri wao.


Pia ameeleza mipango ya utekelezaji kwa Februari 1, 2023 hadi Juni 30 ,2023 kuwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya ujenzi wa ujenzi kwa wadau wa sekta ya ujenzi hususan taasisi za umma kutekeleza miradi ya Miundombinu.


Pamoja na hayo Dkt.Mturi ameeleza kuwa lilihamasisha uundwaji wa usajili na vyama vya wadau wa sekta ya ujenzi likiwa na lengo la kutoa fursa kwa wataalam katika sekta ya ujenzi kutekeleza kazi zao kwa kuongozwa na utawala wa Serikali pamoja na kulinda taaluma katika sekta hiyo. hiyo

No comments:

Post a Comment

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...