mwambelablog

Thursday, 9 February 2023

MUITUKIO WA WANAWAKE MAFUNZO YA UBAHARIA NCHINI, NI CHINI YA ASILIMIA MBILI


Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha DMI Dkt. Tumaini Gurumo wakati akizungumza na Waandishi Wahabari jijini Dodoma Februari 9,2023.
 


Na Deborah Lemmubi

Kutoka Dodoma.


Imeelezwa kuwa muitikio wa Wanawake na Vijana wa Kike ni kusuasua katika Mafunzo ya Ubaharia yanayotolewa na Chuo cha Bahari (DMI) kilichopo Dar es salaam.


Hayo yamesemwa mapema leo hii Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa Chuo hiki Dkt. Tumaini Gurumo wakati akizungumza na Waandishi Wahabari kuelezea utekelezaji wa majukumu,ambapo amesema wanafunzi wakike Chuoni hapo ni chini ya asilimia mbili.


Aidha Dkt Gurumo ameongeza kuwa sababu inayoweza kuchangia uchache wa wanafunzi hawa ni pamoja na dhana iliyojengeka katika jamii kuwa mafunzo yanawafa wanaume tu.


"Muitikio wa Wanawake na Vijana wakike katika kozi ya Ubaharia ni wa kusuasua ila tymekuwa tukiona tofauti, kuna wakati unaweza kuisha mwaka mzima hatujapata mwanafunzi wakike, hivyo wapo chini ya asilimia 2"


"Lakini nadhani pia sababu ya kuwa wachache inaweza kuwa ni dhana iliyojengeka katika jamii kuwa mafunzo haya yanatambulika kuwa ni wanaume tu, hivyo tunafanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuongea na Wazazi kuwaruhusu watoto wakike"


Pia amesema kuwa ili huduma ya elimu na mafunzo ya usalama wa vyombo vya usafiri na usafirishaji kwa njia ya maji, isogee karibu zaidi na wananchi, Serikali ya awamu ya sita imewezesha kupata maeneo mbalimbali ya kujenga matawi katika Mikoa ya Lindi na Mwanza.


 Ambapo amesema Matawi hayo yatakapo kamilika huduma ya elimu na mafunzo ya usalama wa vyombo vya usafiri na usafirishaji kwa njia ya maji itakuwa imesogezwa karibu zaidi na wananchi.


Dkt.Gurumo amesema kuwa DMI inatarajia kuboresha karakana ya mafunzo kwa kuongeza vifaa na maeneo ya kujifunzia kuwa ya kisasa zaidi ili kuendana na mabadaliko ya sayansi na teknolojia pamoja na soko la ajira.


"Ujenzi na ukarabati wa mifumo ya Tehama itasaidia kutoa fursa ya mafunzo kwa masafa marefu (Online) ili kuzalisha mabaharia wenye kuendana na teknolojia za sasa"



Dkt.Gurumo amesema kuwa maboresho hayo ya karakana yatasaidia wanafunzi wao kutokuwa wageni wa vifaa wanayokutana navyo wanapokwenda kwenye mafunzo kwa vitendo.


Ameongeza kuwa DMI imeanza utaratibu wa kujenga uhusiano na wamiliki wa meli ili kupata nafasi za ajira na mafunzo kwa vitendo kwa ajili ya mabaharia wa kitanzania nje na ndani ya nchi.


“Tayari DMI imefanikiwa kuwaunganisha na waajiri mabaharia 27 na kufanikiwa kupata ajira na mafunzo kwa vitendo"


Amesema kuwa matawi hayo yatawezesha vijana wengi zaidi kupata elimu na kupanua wigo wa ajira kwasababu soko la ajira ya ubaharia nchini linaendelea kuongezeka na katika ulimwengu ni kubwa kwasasa.


Vilevile amezungumzia mipango mingine ya Chuo hicho kuwa ni pamoja na kujenga vyombo vidogo vidogo vya usafiri majini ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo,kujenga miundombinu ya chuo kwa viwango vya juu mkabala na ufukwe wa bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam ilikukidhi mahitaji ya ongezeko la wanafunzi,walimu na kozi.


Pamoja na kupeleka elimu na mafunzo ya ubaharia katika maendeleo mengi zaidi ya nchi yetu ikiwemo Pemba na Kigoma.

No comments:

Post a Comment

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...