Pichani. Mchungaji Msaidizi wa Kanisa la Victory Celebration Centre liliopo Jijini Dodoma Pasta Josephine Kihoza wakati akizungumza na wanahabari kuhusu ujio wa Kongamano
Na Deborah Lemmubi - Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la Wanawake na Mabinti linaloitwa MEGA LADIES TALK SHOW lililoandaliwa na umoja wa VCC Super Ladies kutoka Kanisa la VCC lililopo Jijini Dodoma, litakalo jumamosi 19/11/2022 lenye kubeba kauli mbiu isemayo: BORN TO WIN AND SHINE.
Hayo yamesemwa na Mchungaji Msaidizi wa Kanisa la Victory Celebration Centre liliopo Jijini Dodoma Pasta Josephine Kihoza wakati akizungumza na wanahabari kuhusu ujio wa Kongamano hilo lililolenga kuwa na mkusanyiko mkubwa wa mazungumzo ya Wanawake.
"Ndugu wana habari,Kanisa la VCC kupitia kikundi maalum kinachoundwa na wanawake na mabinti wajulikanao kama VCC Super Ladies tumeandaa kongamano kubwa sana la kihistoria hapa Dodoma litakalofanyika siku jumamosi tarehe 19/11/2022 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni Mabeyo Complex, Kongamano hili linaitwa MEGA LADIES TALK SHOW ikimaanisha Mkusanyiko mkubwa wa mazungumzo ya wanawake. Kwa kifupi Kongamano hili linaitwa MELA TALK au MELA - TALK SHOW"
Aidha Pasta Josephine amesema kuwa licha kongamano hili kuwalenga wanawake na mabinti lakini pia linawahusu wanawake wa dini na kabila zote wa umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kutoka ndani na nje ya Dodoma.
"Talk Show hii inawalenga mabinti na wanawake wa dini zote na umri wowote kuanzia miaka 18 na kuendelea ndani na nje ya Dodoma na Mgeni rasmi ambaye tayari amethibitisha ushiriki atakuwa Mhe Dkt Tulia Ackson Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wanenaji atakuwa Mchungaji Tony Kapola na Mtumishi wa Mungu Lilian Mwasha na mbeba maono Mchungaji Josephine atakayesimamia shughuli nzima"
"Na kuongeza kuwa kauli mbiu ya mazungumzo hayo ni: BORN TO WIN AND SHINE" kwa kiswahili tunasema "NITASHINDA NA KUNG'ARA"
Pia Pasta amesema Kongamano litakuwa ni endelevu na uhitaji ukiwa mwingi watafanya kwa mwaka mara mbili.
"Tunaamini baada ya jumamosi watu watasimulia kwa yote yatakayofanyika katika kongamano hili. Hivyo kongamano hili litakuwa ni endelevu na uhitaji ukiwa mwingi tunaweza kufanya kwa mwaka mara mbili kwani hii ni semina ya mabadiliko"
Nakuahidi kuwa watalifanyia kazi suala kwenda vijijini kufanya makongamano mana huko ndiko tunakotoka wote.
Mela Talk ni matokeo ya maono ambayo Mungu aliweka ndani ya moyo wa Josephine Kihoza, Mama Mchungaji na Mchungaji Msaidizi wa Kanisa la CAG - VCC Dodoma ya kuendesha semina,makongamano na mijadala mbalimbali ya kuwasaidia na kuwaweka watu huru ili wawe na maisha mema na yenye furaha kama alivyokusudia Mungu.
No comments:
Post a Comment