Pichani: Naibu katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.Seif Shekalaghe Jijini Dodoma Katika wiki ya Kampeni ya kuzuia Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa za Antibiotiki
Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa agizo kwa taasisi na vituo vyote vya kutolea huduma za afya kutekeleza Mpango wa Taifa wa Kupambana na Usugu wa Dawa dhidi ya vimelea mbalimbali antimicrobial(2023-2028) huku akiwataka Matabibu kote nchini kuandika dawa kwa kufuata mwongozo wa matibabu wa mwaka 2021 na kutumia majina halisi ya dawa (generics) na kwa usahihi.
Agizo hilo limetolewa na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.Seif Shekalaghe Jijini Dodoma Katika wiki ya Kampeni ya kuzuia Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa za Antibiotiki ambapo ametoa ametaka Watoa dawa (Dispenser) kusoma na kuelewa maelekezo ya matabibu na kutoa maelekezo sahihi kwa wagonjwa.
Aidha kutokana na Ripoti iliyotolewa na
Benki ya Dunia mwaka 2017, imeonesha kuwa ifikapo mwaka 2050 uchumi wa Dunia utapungua kwa asilimia (3.8%) na kwamba kiasi cha dola za Marekani trilioni 3.4 zitapotea ifikapo mwaka 2030 kutokana na tatizo hilo.
''Aidha, ripoti hiyo imeeleza kuwa nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania zinaathirika zaidi ambapo
kiasi cha dola za Marekani bilioni tisa (9) zitatumika kila mwaka kupambana na
usugu wa vimelea dhidi ya dawa hizo''.Dkt Shekalaghe
Katika Hatua nyingine Dkt Shekalaghe amewaasa wananchi katika wiki hii ya maadhimisho kujifunza juu ya usugu wa vimelea dhidi ya dawa na ni kitu gani kinawapasa kufanya kuimarisha afya zao.
Njia nzuri na rahisi kuzuia na kutokomeza usugu wa vimelea dhidi ya dawa ni kwa jamii na wataalam wa Sekta ya afya ya binadamu, Wanyama na Mazingira kutimiza wajibu wetu katika kuhakikisha kuwa dawa sahihi inatolewa na kutumika tu pale inapohitajika.
No comments:
Post a Comment