Na Lydia Lugakila,
Kagera
Ofisi ya waziri mkuu kupitia kitengo cha maafa imeanza kutoa mafunzo ya uokoaji kwa wavuvi kutoka wilaya ya Bukoba Misenyi ikiwa ni hatua ya kuwaongezea uwezo wa kufanya uokoaji wakati yanapotokea majanga.
Akifungua mafunzo hayo mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila amesema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la waziri mkuu alilolitoa baada ya kutokea ajali ya ndege precision Air iliyotokea Novemba 6 mwaka huu ndani ya ziwa Victoria na kusababisha vifo vya watun19 na 24 kunusurika.
Amesema kuwa anaishukuru ofisi ya Waziri Mkuu kitengo Cha maafa kuanza kutoa Mafunzo hayo yatakayosaidia kuongeza ujuzi na uhodari katika uokozi kwa vikundi vya wavuvi mkoani hapa huku akitoa wito kwa jamii ya Watanzania kuacha tabia ya kubeza juu ya juhudi zilizofanyika katika kipindi Cha ajali hiyo.
Naye mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya waziri mkuu, Luten Kanali Selestine Masalamado amesema kuwa wavuvi kutoka mkoani Kagera walioshiriki kufanya uokoaji wanashiriki mafunzo hayo maalumu kwa kipindi cha siku 7 ili waweze kuwapa mafunzo na uzoefu kutoka kwa wataalam ili kujua namna nzuri ya kuweza kumuokoa mtu anayepata ajali kwenye maji pamoja na utayari wa kukabiliana na majanga katika ziwa yanapotokea.
Ameongeza kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kupunguza athari zinazojitokeza ziwani, ikiwa ni pamoja na kuokoa maisha ya watu na kupunguza upotevu wa mali wakati wa ajali.
Aidha kwa upande wao wavuvi hao akiwemo Hashim Rashid na Taufic Shariff wameishukuru serikali kwa mafunzo hayo kwani yatawanufaisha mbali na kuokoa wameongeza ufanisi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao.
Wavuvi hao wamepata vifaa vya uokoaji vitakavyowasaidia kufanya kazi ya uokoaji kwa urahisi pamoja na kujifunza namna ya kuvitumia kuokoa watu ajali inapotokea ambapo
No comments:
Post a Comment