mwambelablog

Sunday, 30 October 2022

MAANDALIZI YA MATOKEO YA AWALI YA SENSA YAMKOSHA MAKAMO WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR

 




Na Mwandishi wetu-Dodoma.

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Mohamed Abdullah amesema ameridhishwa na hatua ya maandalizi ya uzinduzi wa matokeo ya awali ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ambayo yamefikia asilimia 85 na matarajio kufikia kesho jioni yatakuwa yamekamilika kwa asilimia zote.


Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Oktoba 31,2022 katika Uwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.


Mh Abdullah ameyasema hayo leo Oktoba 29,2022 jijini Dodoma alipotembelea uwanja wa Jamhuri ambako kutafanyika hafla hiyo kwa ajili ya kushuhudia maandalizi yanavyokwenda.


“Maandalizi yanaendelea vizuri na hali tuliyoiona tumefikia zaidi ya asilimia 85 kilichobaki ni kukamilisha mambo madogo madogo ambayo leo na kesho yatakuwa yamekamilika kwa asilimia zote kitakachobaki ni ile siku ya shughuli ya watanzania kuhudhuria kwa mujibu wa utaratibu,


Na kuongeza kuwa:”Rais Samia atazindua matokeo ya mwanzo ya sensa ya watu ya mwaka 2022 na tumejipanga vizuri na tunaamini kwamba uzinduzi huu utakuwa wa kisasa sana,"Amesema Abdullah


Amesema hafla hiyo itakuwa mubashara kupitia vyombo mbalimbali vya habari na watanzania watapata nafasi ya kuona na kusikia.


"Sensa ya mwaka huu ni ya kisasa na ya kipekee sababu imefanyikia kidigitali kuliko sensa za awamu Zote na takwimu hizi zitatusaidia katika maendeleo mbalimbali ya kiuchumi, haitatumika Tanzania pekee bali itatumika kwa nchi nyingi duniania kwakuwa tumekuwa tukishirikiana na nchi mbalimbali katika mambo tofauti tofauti"


Aidha ameongeza kuwa takwimu za matokeo ya sensa zitasaidia Kwa kiasi kikubwa shughuli za kiuchumi na kijamii ili kupanga maendeleo kwa maslahi ya Taifa.


Kwa mujibu wa Makamu huyo wa Rais amesema kuna vigezo ambavyo vinachukuliwa kimataifa vya ubora wa sensa na hayo yatatoka taarifa zake baada ya uzinduzi.


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Maandalizi ya hafla hiyo Rosemary Senyamule amesema maandalizi ya yanaendelea.


Amesema katika kuhakikisha kila kitu kinafanikiwa kwa weredi na wameunda kamati zipatazo 11 zinazoongozwa na Wakuu wa Wilaya .


Rosemary amesema kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa na vyombo vingine wamehakikisha suala hilo linapewa kipaumbele siku hiyo ya tukio.


"Kiujumla tuko vizuri tumeunda kamati 11 na zinaongozwa na wakuu wa Wilaya, kubwa zaidi ni kuhakikisha wanawahamasisha wananchi katika maeneo yao siku hiyo wafike uwanjani mapema kwa ajili ya kukamilisha zoezi Hilo"


Naye Mkuu wa Wilaya ya Kongwa ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya itifaki na mapokeze Remedius Mwema amesema kuwa mpaka sasa tayari mabalozi kutoka Nchi mbalimbali wamethibitisha kushiriki katika zoezi hilo.


Amesema bado wanaendelea kutoa mialiko ya viongozi watakao hudhuria na wageni kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwemo viongozi na wananchi zaidi ya 140.

No comments:

Post a Comment

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES

Zhang Ping'an, Executive Director of Huawei and CEO of Huawei Cloud, announcing Pangu Models 3.0. [Dongguan, China, July 7, 2023] The...